We have 127 guests and no members online

×

Warning

JUser: :_load: Unable to load user with ID: 641

JUser: :_load: Unable to load user with ID: 644

003.NOKIA da1bc


Taarifa kwa vyombo vya habari
Wateja 70 waibuka washindi kwenye droo kubwa ya Promosheni ya Patapata na Nokia Ushinde'
Dar es Salaam, Januari 11, 2013 ... Washindi takribani 70 wamepatikana kupitia droo kubwa ya Patapata na Nokia Ushinde' ambayo imechezeshwa ikishirikisha wateja wote walionunua bidhaa hizo tangu kuanza kwa promosheni hiyo mnamo mapema mwezi Desemba mwaka 2012.

Posted On Friday, 11 January 2013 12:47

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa
Kimataifa wa Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo Perin L.Saint Ange,alipofika
Ikulu Mjini Zanzibar,akiwa na ujumbe wake.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]

 

Posted On Thursday, 10 January 2013 10:55

IMG-20130109-00250 22097

Posted On Wednesday, 09 January 2013 05:11

nyara1 2c6e0

,Miongoni mwa nyara za serekali zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye ghala maalumu kwenye nyumba ya mtuhumiwa Peter Lawrence zikionekana kwenye maboksi tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi.nyara2 1533e

Posted On Monday, 07 January 2013 13:36

 

DSC00792-1 3f5ed

Na: Albert Sanga, Iringa.

Nikiwa muhula wa mwisho kumalizia masomo ya shahada yangu ya kwanza, siku moja niliingia katika mjadala mzito sana na mama yangu mzazi. Mama yangu alikuwa akishusha pumzi kuona kuwa mwanae sasa ninaelekea kukamilisha ngwe ya elimu ya juu. Mawazo na kiu yake kubwa ilikuwa ni kuona natafuta ajira mapema kitu ambacho mimi nilitofautiana nae na hivyo kuzusha malumbano ya kihoja na kimtazamo.Wakati mama yangu akiamini mafanikio kupitia kuajiriwa, mimi niliamini (na ndivyo ninavyoamini na kuiishi imani hiyo) kuwa ukombozi wa kweli wa kiuchumi na kifedha (real financial freedom) utakuja kwa kuanza kujiajiri na hatimaye kuwa mwajiri wa wengine katika biashara ama shughuli zangu mwenyewe.

Posted On Monday, 07 January 2013 09:43

Head of Primary Medical Centre Bwa. Siwawi Konteh (wa pili kulia) ambaye pia ni mratibu wa mradi wa Tuunganishe Mikono Pamoja ili kuokoa Afya ya Mama na Mtoto akizungumzia Malengo Makuu ya mradi huo kuwa ni kuongeza kiwango na matumizi ya Huduma ya Afya ya Mama Mjamzito na Watoto na kushirikiana na kujifunza kuhusu Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto. Kutoka kushoto ni Acting Medical Director wa Aga Khan Hospital Dr. Ambrose Chanji, Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin Habib, Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Dr. Sebastian Ndege na Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu cha Hospitali hiyo Bw. Anis Nazrani.

Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Services Limited Dr. Sebastian Ndege (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa kukabidhi magari ya kubeba wagonjwa kwa hospitali ya Aga Khan ambapo amesema vifo kadhaa vinavyotokea katika hospitali nyingi kwa sasa vinawahusisha akinamama na watoto wasio na hatia ambao hukosa huduma za awali za haraka zikiwemo usafiri na hivyo katika kujali hilo wametoa magari hayo.

Aidha amesema Ndege Medics inashukuru kuwa sehemu ya mradi endelevu wa kujaribu kuokoa maisha ya akina mama na watoto ambao lengo lake ni kuchangia katika kuboresha afya ya uzazi wa mama na watoto wachanga katika mikoa ya Dodoma, Iringa, Mwanza, Mbeya na Morogoro.

Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin Habib (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Services Limited Dr. Sebastian Ndege wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa magari ya kubeba wagonjwa kwa Hospitali ya Aga Khan ikiwa ni katika mradi wa kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto Tanzania

Posted On Saturday, 05 January 2013 09:48

startimes 94ffc

KAMPUNI ya Star Media Tanzania Ltd (Startime) imewataka watu ambao wamenunua ving’amuzi na kubaini kuwa havifanyi kazi kuvirejesha kwenye ofisi zao ili wapatiwe vingine.
Vilevile wamewataka wale waliouziwa kwa bei ya kulangua wafike kwenye ofisi zao pamoja na risiti walizonunulia ili hatua zinazofaa ziweze kuchukuliwa.


Hatua hiyo inatokanana malalamiko ya wananchi siku chache tangu kuanza kutumika kwa mfumo wa dijitali wa kurusha matangazo ya runiga.

Malalamiko hayo yanayolalamikiwa na kampuni hiyo ni kuhusiana na kushindwa kuonekana kwa baadhi ya chaneli licha kufunga king’amuzi kwenye Televisheni

Posted On Saturday, 05 January 2013 09:44

529827 284858378265102 1162511215 n 1faab

Mnara wa shule ya sekondari ya ufundi Tanga (TTS)

 

Kipindi tupo watoto kulikuwa na usemi mmoja maarufu sana "Mwanangu kua uyaone", usemi huu ulikuwa unaniumiza sana kichwa na kuwa na hamu na shauku ya kukua ili niyaone hayao ya kuyaona. Niliamini kuwa jinsi

ninavyokua npyo ninavyozidi kuona na kujifunza mambo mengi zaidi, na ni kweli, sikukosea kwenye hili, kwenye njia ya ukuaji niliyopita, nimejifunza na ninaendelea kujifunza mengi hivyo ni wajibu wangu kugawana na

wanajamii angalau yanaweza kuwa na mchango.


Kipindi nipo mtoto nilitamani sana kuwa daktari, kwani sehemu tuliyokuwa tunaishi kulikuwa na daktari mmoja ambaye nilifanana naye kijina na kimuonekano alikuwa anaitwa Dk Babu, jamii iliyonizunguka, na umaridadi wa

Dk Babu ulinifanya nipende sana kuwa daktari.


Kwakuwa tulikuwa tunakaa karibu na uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere, hivyo kila siku ya mungu nilikuwa nikisikia na kuona midege mikubwa kwa midogo ikifungua matairi tayari kwa kutua. Kitendo kile kilinivutia sana

na tararibu nilianza kubadirika na kupenda kuwa pilot.Mama aliniambia ukitaka kuwa pilot inabidi ukazane kwenye hesabati, hivyo nilikazana sana na kujikuta nikiwa wa kwanza kwenye hisabati kila mwaka.

Matokeo yangu ya darasa la saba yalikuwa ni kaburi la ndoto zangu mbili, ingawa wengi walisherehekea na kunipongeza kwa kuchaguliw kwenda sekondari nzuri ya ufundi, ila binafsi kwa wakati ule nikajua kuwa sitoweza

tena kuwa rubani wala daktarik, hii ni kwa sababu enzi zile shule za ufundi hatukuwa tunafundishwa biolojia wala jiografia ambazo ni nyenzo kuu za fani nizipendazo.

Posted On Thursday, 03 January 2013 15:06
Tafsiri Yangu Wiki Hii

 

Tafsiri Yangu Wiki Hii

 

Tafsiri Yangu Wiki Hii...
Posted On Sunday, 30 December 2012 09:57

 

 Daktari mmoja aitwaye Mackod, alipitia makala nyingi za afya ili kuweza  kutambua visababishi vya vifo ambayo havitokani na umri au nasaba ya kiasili (genetic), na akagundua mambo tisa ambayo yanasabisha vifo ambavyo vingeweza kuzuilika. Mambo hayo tisa ni; uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe, ukosefu wa mazoezi, lishe duni, wadudu kama bakteria na virusi, ajali, tabia za ngono za kupita kiasi bila kinga,  vita na madawa ya kulevya.

Katika makala hii ningependa kuzungumzia juu ya ufanyaji wa wazoezi na hasa wakati bora wa kufanya mazoezi. Mazoezi ni muhimu sana kwa ajili ya kupunguza mafuta ya ziada mwilini, tafiti zinaonesha kuwa asiyefanya mazoezi, madhara anayopata ni sawa na mtu anayevuta tumbaku.

 

Utafiti uliofanywa na Dr. Jason na Nor Farah (2004) wa Chuo kikuu cha Glasgow, umeonesha kuwa unapofanya mazoezi kabla ya kifungua kinywa, wakati tumbo likiwa tupu, ni bora zaidi kuliko unapoweza kufanya mazoezi baada ya mlo wowote. Kufanya mazoezi ni jambo la maana kwa afya kuliko kutokufanya mazoezi ya mwili, lakini unaweza kupata  faida zaidi kama unaweza kufanya kabla hujala chochote.

Posted On Friday, 28 December 2012 09:11

 

Walenga walisema adhabu ya kaburi aijuaye maiti na ukiona aisifiaye mvua ujue imenyea. Misemo hii ni kweli kabisa kwani pilipili iliyo shamba haiwezi kukuwasha wewe mtu uliye mujini. Kuna siku za nyuma niliwahi kuandika makala nikielezea umuhimu wa tekinolojia, nilizungumzia mambo mengi sana likiwemo la kurahisisha maisha na sio kuongeza ugumu.

 

Tekinolojia inayofanya maisha yawe magumu sio tekinolojia inayokubalika katika ulimwengu wa leo, na tegemea kukimbiwa kama ukoma.Kuna usemi unaosema "IT Doesn't Matter" akimaanisha tekinolojia ya mawasiliano sio kitu, hapa hawamaanishi kuwa tekinolojia ni boya, bali kuwa na tekinolojia sio kitu kigeni, kitu kigeni ni manufaa yake.

Posted On Friday, 28 December 2012 08:16


Uvimbe kwenye mayai ya ya mwanamke (ovary)hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanaozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke. Uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai  ya mwanamke ndio unaojulikana kamaovarian cyst
Uvimbe huu hutokea kwa wanawake wa umri wowote ule na mara nyingi huonekana kwa wanawake waliokatika umri wa kushika ujauzito. 

Lazima nikiri ya kwamba shauku ya kuandika makala hii inatokana na swali la msomaji  wetu mmoja alilouliza “Nimepiga ultra sound nikaambiwa nina kitu cheupe kwenye ovar yangu moja je hili tatizo linaweza kunifanya nisishike mimba? na matibabu yake yakoje? na pia naumwa sana nyonga tiba yake ni nini. Nitashukuru kwa msaada wako.” Mwisho wa kunukuu. 

Posted On Friday, 28 December 2012 00:00
Page 47 of 48

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart