We have 90 guests and no members online

Asilimia 94 ya madini katika sarafu ya sh. 500 ni chuma na asilimia 6 ni Nickel, ameeleza Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki katika Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Marcian Kobello.

Pia ndivyo ilivyoelezwa wakati wa uzinduzi wa sarafu hii mnamo mwezi Septemba mwaka jana kabla haijaingizwa katika mzunguko mwezi Oktoba 2014.

Bw. Kobello amesema hadi sasa sarafu zenye thamani ya sh. 1,162,000,000/- zimekwishasambazwa kote nchini na kwamba kuna kiasi cha kutosha cha sarafu hiyo endapo itahitajika.

Posted On Wednesday, 29 April 2015 17:43

PRIME MINISTER MIZENGO PINDA SPEAKING TO BRITISH AMERICAN TOBACCO OFFICIALS IN HIS OFFICE, DAR ES SALAAM, APRILI 28, 2015. FROM LEFT IS JOHAN VANDERMEULEN REDIONAL DIRECTOR AFRICA, MIDDLE EAST AND EUROPE FOR BRITISH AMERICAN TOBACCO, CHRIS BURREL REGIONAL DIRECTOR EAST AND CENTRAL AFRICA, TEDDY MAPUNDA BOARD MEMBER BRITISH AMERICAN TOBACCO KENYA, ENREST LE ROUX, REGIONAL MANAGER EAST AFRICA AND CONNIE ANYIKA CORPORATE AFFAIRS HEAD EAST AFRICA.

PRIME MINISTER, MIZENGO PINDA POSES FOR A GROUP PHOTO WITH BRITISH AMETICAN TOBACCO OFFICIALS AT HIS OFFICE IN DAR ES SALAAM ON APRILI 28, 2015. FROM LEFT IS ENREST LE ROUX, REGIONAL MANAGER EAST AFRICA- BAT AND CONNIE ANYIKA CORPORATE AFFAIRS HEAD EAST AFRICA, PM, CHRIS BURREL REGIONAL DIRECTOR EAST AND CENTRAL AFRICA, JOHAN VANDERMEULEN REDIONAL DIRECTOR AFRICA, MIDDLE EAST AND EUROPE FOR BRITISH AMERICAN TOBACCO AND TEDDY MAPUNDA BOARD MEMBER BRITISH AMERICAN TOBACCO KENYA.(Muro)

Posted On Wednesday, 29 April 2015 17:35

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mitambo ya ujenzi wa barabara ya Uhuru km 3 huku akiwa pamoja na viongozi wengine wa mkoa wa Dar es Salaam leo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mitambo ya ujenzi wa barabara ya Uhuru km 3 huku akiwa pamoja na viongozi wengine wa mkoa wa Dar es Salaam jijini Dar es Salaam leo.

Sehemu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika uzinduzi wa barabara ya Uhuru jijini Dar es Salaam leo.

Posted On Wednesday, 29 April 2015 17:17

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta (aliyesimama) akifungua Mkutano wa wafanyakazi wa Wizara hiyo mapema jana jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya hiyo Dkt. Shaaban Mwinjaka na kulia ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo Bwana Hassan Mabula.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka akimshukuru Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta mara baada ya kufungua rasmi mkutano wa wafanyakazi wa wizara hiyo na taasisi zilizo chini yaka.

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya hiyo Dkt. Shaaban Mwinjaka mapema jana jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa wafanyakazi wa Wizara hiyo.

Posted On Tuesday, 28 April 2015 05:53

Dr Abel Kinyondo & Invited Expert Innocent Bash from TEITI addressing the media .

Expert Mr Dennis Rweyemamu (Head - Policy and Research, UONGOZI INSTITUTE) answering questions.

January Makamba and Mujobu Moyo listening to participants.

Posted On Tuesday, 28 April 2015 05:42

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akimkaribisha Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini Bi. Liz Lloyd alipomtembelea Wizarani kwa ajili ya mazungumzo na Mhe. Maalim.

Mhe. Maalim akimtambulisha kwa Bi. Llyoid Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya.

Mhe. Dkt. Maalim akizungumza na Bi. Lloyd.

Posted On Friday, 24 April 2015 19:00

Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu shughuli za Maafa ofisi ya Waziri Mkuu, Brig.Jen. Mubazi Msuya (wa pili kulia) akifuatilia majadiliano wakati wa uwasilishaji wa Mkakati wa Mawasiliano wa kukabiliana na maafa kwa mkoa wa Mtwara tarehe 23 Aprili, 2015, kulia kwake ni Katibu Tawala Msaidizi (Uchumi na Uzalishaji) Mkoani Mtwara, Bw. Johansen Bukwari.

Baadhi ya washiriki wa warsha ya uwasilishaji wa Mkakati wa Mawasiliano wa kukabiliana na maafa kwa mkoa wa Mtwara wakifuatilia uwasilishwaji wa mkakati huo, uliofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa mkoani Mtwara tarehe 23 Aprili, 2015.

Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu shughuli za Maafa ofisi ya Waziri Mkuu, Brig.Jen. Mubazi Msuya (Walio kaa wa pili kushoto) akiwa na washiriki wa warsha ya Kuwasilisha Mkakati wa Mawasiliano wa kukabiliana na maafa kwa mkoa wa Mtwara mara baada ya kuwasilisha mkakati huo tarehe 23 Aprili, 2015, wa kwanza kulia kwake ni Katibu Tawala Msaidizi (Uchumi na Uzalishaji) Mkoani Mtwara, Bw. Johansen Bukwari.

Ofisi ya waziri Mkuu kupitia Idara ya Uratibu wa Shughuli za maafa imewasilisha Mkakati wa Mawasiliano wa kukabiliana na maafa kwa mkoa wa Mtwara. Mkakati huo umetayarishwa kwa ajili ya kuhakikisha kwamba kunakuwa na Mtiririko unaoeleweka wa taarifa za tahadhari kabla ya maafa, wakati wa maafa na baada ya maafa kutokea.

Posted On Friday, 24 April 2015 08:50

Meneja Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu uboreshaji wa ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri hiyo. Kulia ni Meneja Kodi Majengo, Stellah Mgumia na Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika wa Manispaa hiyo, Francis Luambano.

Meneja Kodi Majengo wa Manispaa hiyo, Stellah Mgumia akitoa ufafanuzi mbalimbali wa ukusanyaji wa mapato.

Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika wa Manispaa hiyo, Francis Luambano (kushoto), akizungumza na wanahabari katika mkutano huo.Picha na Emmanuel Massakai.(Muro)

Posted On Friday, 24 April 2015 05:50

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu( Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Mhandisi Christopher Chiza (Mb) akibadilishana mawasiliano na baadhi ya wafanyabiashara waliowasili Visiwa vya Comoro kwa ajili ya kushiriki katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Comoro, linalotarajiwa kufanyika tarehe 23 Aprili, 2015. Kushoto (mwenye miwani) ni Balozi wa Tanzania Visiwa vya Comoro Bw. Chabaka Kilumanga.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu( Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Mhandisi Christopher Chiza (mwenye tai) akishiriki kucheza ngoma ya asili ya Comoro mara baada ya kuwasili visiwani humo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Mhandisi Christopher Chiza (Mb) ahudhuria Kongamano Kubwa la Biashara kati ya Comoro na Tanzania, litakalofanyika tarehe 23 Aprili, 2015 Visiwani Comoro.

Lengo kuu la kongamano hilo ni "kuongeza kiwango cha biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Comoro kwa kutambua fursa zilizopo kati ya nchi hizi mbili na kurasimisha biashara ambayo kwa sasa hairatibiwi".

Kongamano hilo ambalo litawakutanisha viongozi, maafisa wandamizi wenye dhamana ya kuendeleza biashara kutoka Tanzania na Comoro pamoja na wadau wa Sekta Binafsi, litafungua rasmi fursa ya kutangaza na kuuza bidhaa zinazozalishwa Tanzania kwa wafanyabiashara watakaopenda kufanya hivyo kutokana na nafasi nyingi za biashara na uwekezaji zilizopo katika Visiwa vya Comoro.

Posted On Thursday, 23 April 2015 13:40

Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Dora Msechu (kushoto) amekutana na wafanyabiashara wa Sweden kwenye mkutano ulioandaliwa na Baraza la Biashara la Sweden na Afrika Mashariki(Swedish East Africa Chamber of Commerce).

Sehemu ya Wafanyabiara hao wa nchini Sweden wakiwa kwenye kikao na Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Dora Msechu.

Sehemu ya Wafanyabiara hao wa nchini Sweden wakiwa kwenye kikao na Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Dora Msechu.(Muro)

Posted On Thursday, 23 April 2015 07:54

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof. Adolf Mkenda akifungua kongamano kongamano la siku moja lililofanyika leo jijini Dar es salaam kuhusu masuala ya uwekezaji kati ya Tanzania na Korea ya Kusini ili kubadilishana uzoefu na kushirikiana katika kuinua uchumi wa nchi zote mbili kwa kushirikisha sekta ya Umma na sekta binafsi katika kujiletea maendeleo endelevu.

Baadhi ya wajummbe kutoka nchini Korea ya Kusini wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof. Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati alipokuwa fungua kongamano la siku moja lililofanyika leo jijini Dar es salaam kuhusu masuala ya uwekezaji kati ya Tanzania na Korea ya Kusini ili kubadilishana uzoefu na kushirikiana katika kuinua uchumi wa nchi zote mbili kwa kushirikisha sekta ya Umma na sekta binafsi katika kujiletea maendeleo endelevu.

Baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania wakifuatilia mjadala wakati wa kongamano la siku moja lililofanyika leo jijini Dar es salaam kuhusu masuala ya uwekezaji kati ya Tanzania na Korea ya Kusini ili kubadilishana uzoefu na kushirikiana katika kuinua uchumi wa nchi zote mbili kwa kushirikisha sekta ya Umma na sekta binafsi katika kujiletea maendeleo endelevu.

Posted On Thursday, 23 April 2015 06:41

Mkwawa

Mjumbe wa mkutano mkuu Taifa (CCM) kupitia mkoa mpya wa Njombe ,Hassan Mkwawa akizungumza na mwandishi wa habari David John.

MJUMBE wa mkutano mkuu Taifa (CCM) kupitia mkoa mpya wa Njombe ,Hassan Mkwawa amesema kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu watanzania watarajie mabadiliko makubwa ya viongozi na hasa wabunge , kwani kutakuwa na sura nyingi za vijana.

Amesema vijana wengi wameonesha nia na kiu kubwa ya kutaka mabadiliko hivyo kutokana na hali hiyo kutakuwa na changamoto za kutosha kutoka kwa vijana.

Kauli ya mjumbe huyo ameitoa jana jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake kuhusiana na mtazamo wake juu ya uchaguzi wa mwaka huu.

Posted On Wednesday, 22 April 2015 16:17
Page 6 of 48

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi