We have 88 guests and no members online

×

Warning

JUser: :_load: Unable to load user with ID: 641

Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wapili kulia), akimkabidhi tuzo, Makamu wa Rais wa kampuni ya Acacia, (Anayeshughulikia kampuni), Deo Mwanyika, baada ya mgodi wa dhahabu wa North Mara unaomilikiwa na kampuni hiyo, kuibuka mshindi wa jumla wa mwaka 2014 wa tuzo ya Rais ya makampuni ya uchimbaji madini, yanavyotekeleza wajibu wa kampuni katika kusaidia jamii (CSRE). Hafla ya kutoa tuzo hizo ilikwenda sambamba na uzinduzi wa muongozo mpya wa makampuni hayo katika kutekeleza CSRE. Aanayeshuhudia ni Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene

Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla hiyo, wakipiga makofi

Makamu wa Rais, akimkabidhi tuzo, Meneja Ustawi wa Kampuni wa Mgodi wa North Mara, Abel Yiga, baada ya mgodi huo kuwa kinara katika migodi iliyomstari wa mbele katika kusaidia jamii, Kulia ni waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene.(Muro)

Posted On Wednesday, 22 April 2015 15:40

MZ1

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la China na Afrika ( Vice Chairman of China Africa Business Council, Bw. Huarong Zhang kabla ya mazungumzo yao Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam,Aprili 21, 2015.Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Tanzania – China Promotion Centre, Bw. Xian Ding. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MZ01

WAziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la China na Afrika ( Vice Chairman of China Africa Business Council, Bw. Huarong Zhang kabla ya mazungumzo yao Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam,Aprili 21, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu. (Muro)

Posted On Wednesday, 22 April 2015 08:12

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (Universal Communications Service Access Fund - UCSAF) Eng Peter Ulanga (Katikati) akiwa na Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa, Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka Ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma, CEO wa TTCL Dr. Kamugisha Kazaura wakiweka sahihi mikataba ya mabilioni kupelekea mawasiliano vijijini.

Afisa Mtendaji Mkuu WA Mfuko WA Mawasiliano kwa Wote (Universal Communications Service Access Fund - UCSAF) Eng Peter Ulanga (Kulia) akitia sahihi mikataba ya mabilioni kupelekea mawasiliano vijijini pamoja na CEO WA TTCL Dr. Kamugisha Kazaura.

Afisa Mtendaji Mkuu WA Mfuko WA Mawasiliano kwa Wote (Universal Communications Service Access Fund - UCSAF) Eng Peter Ulanga (WA pili kulia) akibidilishana mawazo na Waziri WA Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa baada ya kutia sahihi mikataba ya mabilioni kupelekea mawasiliano vijijini.

Posted On Wednesday, 22 April 2015 06:57

Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Mfuko wa LAPF, Yesaya Mwakifulefule (wa pili kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro, Christina Mndeme, msaada wa rangi zenye thamani ya sh. milioni 3 kwa ajili ya umaliziaji wa ujenzi wa maabara katika shule za Ulanga Mashariki.(Muro)

Posted On Wednesday, 22 April 2015 06:48

Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akitoa maelezo ya jinsi Tanzania inavyoboresha uchumi wake kwa Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa (IMF)kwa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara Bi. Antoinette Sayeh wa katikati. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile na kushoto ni Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu , akifuatiwa na Gavana msaidizi wa Benki kuu ya Tanzania Bi. Natu Mwamba.

Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya wa katikati akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania walipokutana na ujumbe wa shirikala fedha la kimataifa (hawapo kwenye picha ). Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile na kushoto ni Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu , akifuatiwa na Gavana msaidizi wa Benki kuu ya Tanzania Bi. Natu Mwamba.

Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akizungumza katika mkutano huo wa Changamoto za Milenia/Chamber of Commerce uliofanyika mjini Washington DC. Aliyeko nyuma ya Mhe Waziri ni Bw. Laston Msongole ambaye ni Mtendaji Mkuu wa mfuko wa milenia wa awamu ya pili.

Posted On Wednesday, 22 April 2015 06:37

Kutoka kushoto ni Mwanasheria wa Shirika Bima la Taifa (NIC) Verdiana Macha,Kaimu Mkurugenzi wa Shirika Bima la Taifa (NIC),Sam Kamanga,Mkurugenzi wa wakala wa majengo ya serikali,Bartazar Kimangano na Mkurugenzi wa utafiti na Maendeleo Asha Myanza wakisaini mikataba ya mauziano ya nyumba zilizopo eneo la Buhire wilayani Musoma leo jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga akimkabidhi mikataba ya mauziano ya nyumba zilizopo Buhire wilayani Musoma Mkurugenzi wa wakala wa majengo ya serikali,Bartazar Kimangano, katika ofisi za shirika hilo leo jijini Dar es Salaam.PICHA NA AVILA

Posted On Tuesday, 21 April 2015 18:24

Uwekezaji wa Kichina nchini Tanzania wamelalamikiwa kwa hatua yao kufanya biashara za reja reja hali ambayo inadaiwa kuwanyima fursa zaidi wenyeji wasio na uwezo wa biashara kubwa.

Katika maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam si ajabu kukutana na baadhi ya wachina wakiwa na biashara mikononi kama wafanyabishara wadogo nchini humo maarufu kama machinga hali inayozua mshangao na viulizo kwamba kweli hawa ni wawekezaji ama wamegeuka kuwa wafanyabiashara ndogo ndogo. Nilitembelea eneo la kibiashara la Kariakoo ili kujionea hali halisi.CHANZO:BBC

Posted On Monday, 20 April 2015 07:17

Bango la kumkaribisha rais Xi nchini Pakistan.

Rais wa China Xi Jinping ameanza ziara ya siku mbili nchini Pakistan hii leo.

Bwana Xi atazindua mpango wa uwekezaji wa kichina wa gharama ya dola bilioni 50 ambao Pakistan ina matumaini kuwa utasuluhisha tatizo lake ya nishati.

Mpango huo unaofahamika kama barabara ya uchumi ya China na Pakistan ni pamoja na barabara , reli na mabomba ya jumla ya umbali wa kilomita 3000 kutoka mji wa bandari wa Gwadar nchini Pakistan hadi mji wa ulio mashariki mwa China wa Kashgar.

Waandishi wa habari wanasema kuwa lengo la China ni kuongeza ushawishi wake wa kiuchumi kwa Pakistan ili kulegeza ule wa Marekani na India.CHANZO:BBC (Muro)

Posted On Monday, 20 April 2015 06:42

1

Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akimsikiliza kwa makini Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier walipokutana katika mikutano hii ya kipupwe inayoendelea hapa Mjini Washington DC.Wengine ni ujumbe kutoka Tanzania pamoja na timu ya wataalam kutoka Benki ya Dunia.

2

Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum akifuatilia kwa makini maswalialiyokuwa akiulizwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier hayupo kwenye picha. Kulia ni katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar.

3

Ujumbe wa Mkutano huo kutoka pande zote mbili yaani Tanzania na Benki ya Dunia, wakimsikiliza kwa makini Mchumi mwandamizi kutoka Benki ya Dunia.

Posted On Friday, 17 April 2015 15:42

Mkurugenzi wa JITENG Consultant Company Bw. Andrew Huwang akiongea jumuiya ya wafanyabiashara kutoka China waishio Tanzania kuhusu ushiriki wao katika masuala ya ukusanyaji kodi na kuendelea kuongeza ushirikiano kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa Semina iliyoandaliwa na Jumuiya ya wachina waishio Tanzania na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyolenga kuwaeleimisha kuhusu ukusanyaji na sheria mbalimbali za Kodi Nchini leo Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Bw.Yeremiah Mbaghi.

Afisa Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Rose Mahendeka akiongea na jumuiya ya wafanyabiashara kutoka China waishio Tanzania kuhusu faida za Mfumo mpya wa Uondoshaji Mizigo (TANCIS) unaosaidia kuongeza ufanisi katika uondoshaji wa Mizigo ya wateja na kuondoa malamiko ya ucheleweshwaji wa huduma hiyo pia kuondoa tatizo la upotevu na mizigo pindi inapoingizwa nchini, wakati wa Semina iliyoandaliwa na Jumuiya ya wachina waishio Tanzania na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyolenga kuwaeleimisha kuhusu ukusanyaji na sheria mbalimbali za Kodi Nchini leo Jijini Dar es Salaam.

Afisa Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Hamisi Lupenja akiwaeleza wafanyabiashara kutoka China waishio Tanzania kuhusu umuhimu wa kushiriki katika matumizi ya Mashine za Risiti za Kielektroniki (EFD) katika manunuzi na uuzaji wa Bidhaa mbalimbali ili kuiwezesha serikali kupata mapato stahiki bila udanganyifu wakati wa Semina iliyoandaliwa na Jumuiya ya wachina waishio Tanzania na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyolenga kuwaeleimisha kuhusu ukusanyaji na sheria mbalimbali za Kodi Nchini leo Jijini Dar es Salaam.

Posted On Friday, 17 April 2015 15:20

Meneja Ufundi Idara ya Petroli EWURA Ndugu Gerald Maganga akiwasilisha moja ya mada katika Semina kwa Wafanyabiashara wa Mafuta Mikoa ya Rukwa na Katavi katika ukumbi wa Moravian Centre Mjini Sumbawanga tarehe 15 April 2015. Kushoto ni Afisa Uhusiano EWURA Ndugu Wilfred Edwin. Miongoni mwa mada zilizowasilishwa katika Semina hiyo ni Udhibiti na Kanuni za Ukokotoaji wa bei za Mafuta, Ubora wa Miundimbinu, Usalama na Utunzaji wa Mazingira katika Sekta ya Mafuta ya Petroli, Faida za kutumia Mafuta yenye kiwango kidogo cha Sulphur na Sheria na Kanuni katika udhibiti wa Sekta ya Petroli nchini.

Afisa Biashara Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Ndugu Paul Nganyanyuka akichangia moja ya mada katika Semina hiyo ya EWURA na wafanyabiashara ya mafuta Mikoa ya Rukwa na Katavi iliyofanyika katika Ukumbi wa Moravian Centre mjini Sumbawanga tarehe 15/04/2015.

Sehemu ya wajumbe katika Semina hiyo ambao ni wafanyabishara wa vituo vya mafuta Rukwa na Katavi, Mtoa huduma Serikalini GPSA na Maafisa Biashara kutoka Mikoa ya Rukwa na Katavi.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)(Muro)

Posted On Thursday, 16 April 2015 13:40

01

Maafisa Waandamizi wa SMZ wakiwa katika viwanja vya Tiananmen Square Jijini Beijing China, wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Mhandisi Mwalim Ali Mwalim na aliyevaa tai ni Mhandisi wa Idara ya Nishati, Omar Saleh Mohamed na wengine mwenye traksuti ni Afisa Mdhamini WQizara ya Ardhi, Makaazi Maji na Nishati Pemba, Mhandisi wa Miamba, Hemed Salim.

02

Maafisa Waandamizi wa SMZ wakiwa viwanja vya Tiananmen Square wa mbele kabisa ni Mkurugenzi wa Usalama kazini, Mhandisi Suleiman Khamis kushoto ni Mwandishi wa habari Juma Mohammed na kulia ni Mhandisi wa Idara ya Nishati, Omar Saleh Mohamed.

04

Maafisa Waandamizi wa SMZ wakiwa katika viwanja vya Tiananmen Square Jijini Beijing China. Maafisa hao wanahudhuria mafunzo ya muda mfupi ya mafuta na gesi asilia.(Muro)

Posted On Thursday, 16 April 2015 08:04
Page 7 of 48

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi