siasa

Makamba:kila dakika moja mita 100 za misitu hukatwa TZ

on

Na Mwandishi wetu Dodoma.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais, January Makamba amesema misitu inayofyekwa kwa dakika moja nchini ni sawa na uwanja wa mpira.

Makamba aliyasema hayo wakati  akijibu hoja zilizotolewa na wabunge wakati wakichangia makadirio ya Mapato na Matumizi ya ofisi ya Makamu wa Rais kwa mwaka wa fedha 2019/2020, bungeni leo Jumanne 16, 2019

Akitolea mfano zaidi alisema  15 ni sawa na viwanja vya mpira 15 na hiyo ni takwimu za chini ya misitu inayofyekwa na sehemu kubwa ni ukataji wa miti, kilimo kisichoendelevu na uzururaji wa mifugo na kadhalika.

Alieleza kuwa  misitu inathamani katika mifumo ya iokolojia na kwamba utajiri nchi hupimwa kwa mambo mengi ikiwemo utajiri wa watu, utajiri wa vitu na maliasili.

Hata hivyo alisema  nchi zilizoendelea nchi ambazo zinaongoza kwa utajiri wa maliasili Tanzania ni nchi moja kati ya nchi zinazoongoza.

Pamoja na hayo alieleza  ukombozi upo katika utunzaji wa miti iliyopo na sio upandaji wa miti kwasababu miti iliyopandwa ni asilimia nane tu ya miti iliyopo nchini.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *