habari

Makao Makuu Ya Tume Ya Uchaguzi Libya Yashambuliwa. Zaidi Ya Watu 11 Wauawa.

on

Takribani watu 11 wameuawa Jumatano hii katika shambulizi linalodaiwa kutekelezwa na washambuliaji wa kujitoa mhanga dhidi ya makao makuu ya tume ya uchaguzi nchini Libya. Shambulizi hilo lilitokea katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli, vyanzo vya usalama vimesema.

Msemaji wa tume hiyo Khaled Omar amesema washambuliaji waliweza kuingia katika majengo ya tume ya uchaguzi.

“Niliona washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga wakisema kwa sauti kubwa Allah Akbar (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa),”.

“Mshambuliaji mmoja wa kujitoa mhanga alijilipua ndani ya majengo ya tume ya uchaguzi na wengine walichoma moto sehemu moja ya jengo hilo,” ameongeza.

Kulikuepo na ufyatulianaji risasi na vikosi vya usalama. Wafanyakazi waliweza kuondoka jengo hilo. Lakini wafanyakazi watatu waliuawa, pamoja na polisi wanne, Khaled Omar amesema.

Wizara ya Afya imetaoa ripoti ya watu 11 waliouawa na wawili waliojeruhiwa. Picha zilizorushwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha moshi mweusi ukiwa juu ya kata ya Tripoli ambapo tume ya uchaguzi inapatikana.

Shambulizi hili ni la aina yake mjini Tripoli kwa miaka kadhaa sasa. Vurugu katika mji mkuu hivi karibuni zililkua zilipungua na kulikua kukishuhudiwa mapigano kati ya makundi hasimu.

Tume inafanya kazi kwa orodha ya wapigakura kuelekea uchaguzi mpya, ambao Umoja wa Mataifa unatarajia utafanyika mwishoni mwa mwaka huu ambapo karibu wapiga kura wapya milioni moja wameorodheshwa.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *