habari

Mamlaka ya viwanja vya ndege Zanzibar (ZAA) yajivunia ujio wa Airbus 2020

on

Mamlaka ya viwanja vya ndege Zanzibar (ZAA) imesema uwepo wa safari za ndege ya ‘’Air Bus 2020’’ ya shirika la ndege la Tanzania itaongeza fursa mbali mbali za kibishara ikiwemo utalii wa Zanzibar.

Hayo yamesemwa na Meneja uendeshaji wa shughuli za uwanja wa ndege kisiwani hapa Buheti Juma Sleiman alipokua akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ujio wa ndege hio.

Alisema hatua hio ni wazi kuwa itatanua fursa zaidi ikiwemo kuongeza utalii ndani ya Zanzibar na kwamba wananchi wengi wataweza kufaidika.

Hata hivyo alisema kwa upande wao wamejipanga na kupitia uwanja huo ndege yoyote hile inaweza kutua bila ya matatizo yoyote yale.

Pamoja na hayo alieleza kuwa harakati za kufanya utanuzi zaidi wa uwanja wa ndege zinafanyika kwa lengo la kutoa fursa zaid i kwa mashirika mbali mbali yaweze kuleta ndege zao.

Awali Rubani wa ndege hio ya Tanzania Air Buss 220 Kassim S.Soud alisema ndege hio imetengenezwa kwa mfumo wa kisasa na ni miongoni mwa ndege bora duniani.

Alisema tangu kuletwa kwa ndege hio hadi sasa haijawahi kutokea tatizo lolote lile ambalo lingeweza kuleta hitilafu na kwamba wananchi wasiwe na hofu na ndege hizo.

Awali makamo wa Rais wa kampuni ya Air Buss Hadi Akoum alisema ndege hio ni miongoni mwa ndege bora ulimwenguni na zilizotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu.

Pia alisema licha ya kufanya shughuli z auuzaji wa ndege lakini wanahakikisha wanampa mteja wao huduma mbali mbali ikiwmeo ushauri  elekezi kuhusua maswala ya wateja na wapi wanapaswa kuelekeza ndege zao.

Sambamba na hayo alisema wapo Zanzibar kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa maafisa wanaofanya biashara za ndege Africa kwa lengo la kuwajengea uwelewa zaidi na kuongeza uelewa zaidi ukizingatia ushindani uliopo katika sekta ya anga.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *