michezo

Man City Watangazwa Mabingwa EPL Wakiwa Na Mechi 5 Mkononi.

on

Kipigo cha 1-0 walichopata Manchester United dhidi ya West Brom, kimeipa rasmi Manchester City ubingwa wa Premier League.

Man City yenye jumla ya pointi 87 huku ikiwa na mechi tano zilizosalia kukamilisha ligi kuu EPL, Manchester United pekee ndiyo ingeweza kuzifikia iwapo ingeshinda mechi zake zote zilizosalia huku City ikitakiwa kupoteza zote.

 kunako dakika ya 73, United waliruhusu bao pekee kupitia kwa Jay Rodriguez wa West Brom, ambalo lilidumu mpaka mchezo huo ulipomalizika.

Kwa matokeo hayo United yenye michezo 33 inabakiwa na pointi 71 na kama itashinda mechi zake tano zilizosalia itajikusanyia pointi 86.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *