michezo

Man United Yaelezwa Kuingiza Pesa Nyingi EPL Kuliko Man City.

on

Ripoti zinaonyesha kuwa klabu ya ManUnited ilipata pesa nyingi kuliko mabingwa wa ligi ya EPL Manchester City kutoka kwenye Ligi hiyo katika msimu uliomalizika, licha ya City kufanya vizuri zaidi na hata kuweka rekodi.

United, waliomaliza wa pili, walipokea £149.77m, £328,491 zaidi ya City.

United walilipwa pesa zaidi kwa sababu kuna mechi zao mbili zaidi ambazo zilionyesha moja kwa moja kwenye runinga Uingereza – hii ina maana kwamba pesa walizolipwa kutokana na uwanja wao na huduma nyingine zilikuwa £2.26m zaidi.

Kwa jumla, klabu za Ligi ya Premia zilipokea £2.42bn, £2.1m zaidi kuliko msimu uliopita.

United chini ya meneja wao Jose Mourinho mechi zao zilizoonyeshwa kwenye runinga Uingereza msimu huu zilikuwa 28, sawa na zilizooneshwa za Liverpool na Arsenal. Hata hivyo, zilizoonyeshwa za City zilikuwa 26.

Malipo ya jumla kwa klabu hutokana na mapato kutoka kwa haki za utangazaji wa mechi kwenye runinga Uingereza (ambayo asilimia 50 yake hugawanywa kwa njia sawa kwa klabu zote. Asilimia 25% ya mapato yaliyosalia hugawanywa kwa kuzingatia mechi ambazo zimeonyeshwa moja kwa moja kwenye runinga, na asilimia 25 kwa kuzingatia nafasi ya klabu kwenye jedwali), mapato kutoka kwa shughuli nyingine za kibiashara na mapato kutoka kwa haki za utangazaji wa mechi kimataifa.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *