habari

Maonesho Nane Nane yasiwe nguvu ya soda- Dkt.Mwanjelwa

on

2

Mkuu wa Wilaya Ilemela, Mhe.Dkt. Severine Lalika akizungumza kwenye maonesho hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella

3

Mwenyekiti Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Ziwa Magharibi, Mathayo Masele akitoa taarifa ya maonesho hayo

4

Kaimu Katibu Tawala mkoani Mwanza, Mhandisi Warioba Sanya akitoa salamu zake kwenye maonesho hayo

IMG_0723

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt.Mary Mwanjelwa akijionea kikundi cha ngoma cha Bujora wakati kikitumbuiza kwenye maonesho hayo

IMG_0749

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt.Mary Mwanjelwa akipokea maelezo kuhusu zao la mpunga kutoka kwa Dkt.Rashid Lussewa (kushoto) ambaye ni mtafiti wa zao hilo Kanda ya Ziwa, Chuo cha Kilimo Ukiriguru

IMG_0813

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt.Mary Mwanjelwa alitoa rai kwa wataalam kutoka taasisi ya kilimo Ukiriguru pamoja na Bodi ya Pamba kuhakikisha wanatoa elimu kwa wakulima kuhusu namna bora ya kupambana na wadudu waharibifu wa zao la pamba kwani wakulima wengi wamepata hasara kutokana na wadudu hao.

IMG_0773
IMG_0782
IMG_0785
IMG_0788
IMG_0799
IMG_0803
IMG_0805

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt.Mary Mwanjelwa jana Oktoba 04, 2018 amefungua rasmi maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nane Nane Kanda ya Ziwa Magharibi yanayofanyika katika uwanja wa Nyamhongolo Jijini Mwanza.

“…Maonesho haya ya Nane Nane ambayo ndiyo ya msingi sana, yasiwe tu kama ni maonesho ya nguvu ya soda, tunataka tuone matokeo chanya kwa wakulima wetu. Na kwa maana hiyo ifike mahala basi tuwe na maonesho ya kimataifa…”. Alisisitiza Dkt.Mwanjelwa.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maonesho hayo, Mathao Masele alisema yalianza Oktoba Mosi na yatafikia tamati Agosti 08, 2018 ambapo hadi sasa kuna zaidi ya washiriki 300 kutoka taasisi na makampuni mbalimbali.

Hii ni mara ya kwanza maonesho ya Kanda ya Ziwa Magharibi yanayoshirikisha mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera kufanyika baada ya serikali kugawa mikoa ya Kanda ya Ziwa katika kanda mbili kwa ajili ya kushiriki maonesho ya Nane Nane. Kanda nyingine ni Kanda ya Ziwa Mashariki inayoshirikisha mikoa ya Mara, Simiyu na Shinyanga.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *