habari

Marekani Yafanya Shambulizi Dhidi Ya Syria.

on

 

Katika hotuba yake kutoka White House Ijumaa mwendo wa saa tatu usiku saa za ukanda wa Mashariki mwa Marekani, Rais wa Marekani Donald Trump alisema kuwa Marekani kwa kushirikiana na nchi za Uingereza na Ufaransa, zimeamua kuchukua hatua hiyo kama njia ya kuzima uwezekano ya mashambulizi mengine ya kutumia gesi ya sumu.

“Muda mfupi uliopita nimeamuru jeshi la Marekani kushambulia maeneo yaliyohusika na shambulizi la silaha za kemikali lililotekelezwa na utawala wa Bashar al-Assad,” alisema Trump na kuongeza kuwa marekani haitakubali mashambulizi ya kemikali.

Naye waziri wa ulinzi Jenerali Jim Mattis akihutubia waandishi wa habari kwenye makao makuu ya kijeshi ya Marekani, Pentagon, alitoa maelezo zaidi kuhusu mashambulizi hayo, na kusema kuwa yalilenga vituo vitatu, kikiwemo kimoja cha utafiti na kingine cha kuhifadhi gesi ya sumu.

“Mashambulizi hayo ni makubwa zaidi ya mara mbili na yale tuliyoyafanya nchini Syria mwaka jana…na ni makubwa,” alisema Mattis.

Kituo cha televisheni cha CNN kimeripoti kwamba milipuko mikubwa ilisikika mjini Damascus punde baada ya rais Trump kutoa hotuba yake.

Aidha, katika hotuba yake, Trump alieleza masikitiko yake kwamba licha ya rais wa Russia Vladmir Putin kuahidi kuchukua hatua za kuangamiza uwezo wa Syria wa kutumia silaha za kemikali, Russia bado haijafanya hivyo.

“Ni sharti Russia iamue kama itaendelea kwenye barabara hiyo au itajiunga na nchi zinazotafuta amani,” alisema rais huyo.

Wakati huo huo, kituo hicho kiliripoti kwamba vikosi vya Syria vilikuwa vinakabiliana na vile vya muungano wa nchi hizo tatu kufuatia shambulizi hilo.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *