habari

Marufuku Ya Kupiga Adhana Nchini Rwanda Yapingwa na Baadhi Ya Waislamu.

on

Hatua ya kuzuia matumizi ya adhana katika tarafa ya Nyarugenge mjini Kigali nchini Rwanda, imeonekana kupingwa vikali na baadhi ya Waislamu nchini humo.

Hata hivyo Utawala katika tarafa hiyo ambako jamii kubwa ya Waislam wanapatikana, umebainisha kuwa kumekuwepo na maamuzi ya pamoja ya kubadili mbinu za kuwaita waumini bila ya matumizi ya njia hiyo ambayo inatajwa na viongozi wa tarafa hiyo kuwa inawasumbua wananchi.

Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC jijini Kigali John Gakuba wito huo wa Waislamu kuhudhuria maombi umetajwa kuwa kero miongoni mwa wananchi, ambapo tayari mkataba wa kuhakikisha kuwa mwafaka huo unaheshimiwa umetiwa saini kati ya viongozi wa msikiti na utawala wa eneo hilo.

Naye mshauri wa Mufti wa Rwanda shekh Mbarushimana Suleinam alisema kuwa hatua hii ya kuzuiliwa kwa matumizi ya adhana misikiti inafuatia operesheni inayoendela ya kufungwa kwa makanisa na vigango Zaidi ya mia saba ambavyo viliripotiwa kuwa havijatimiza kanuni za ujenzi na amri ilitolewa kwanza kutimiza matakwa ili zipewe tena idhini ya kufanya kazi.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *