habari

Masauni avunja ukimya dhidi ya Polisi na dawa za kulevya Z’ba

on

š

Mohamed Khamis,Zanzibar

Naibu waziri wa mambo ya ndani Yussuf Masauni amesema haridhishwi na kasi ya jeshi la polisi visiwani Zanzibar katika jitihada za mapambano ya dawa za kulevya.

Masauni ameyasema hayo jana kisiwani hapa wakati  akizungumza na waandishi wa habari katika  ukimbi wa makao makuu ya jeshi la polisi Ziwani.

Amesema kisiwani cha Zanzibar kutokana na udogo wake haiwezekani hadi leo hii jeshi la polisi lishindwe kupata mafanikio ikiwemo kuzuia madawa ya kulevya na kuwaacha vijana wengi wakitumiw dawa hizo hatimae kukosa mwelekeo.

Hata hivyo Masauni amesema anazo taarifa wapo baadhi ya watendaji wa jeshi la polisi wamekua wakijihusisha na kuwaficha wauzaji au wasambazaji wa dawa za kulevya na kwamba wizara yake haitawavumilia.

Pamoja na hayo amesema tayari anayo majina ya baadhi ya maafisa hao na wanaoshirikiana nao ingawa hakua tayari kuwataja kwa madai ya kuharibu ushahidi.

“Munaiona hii karatasi ina kurasa tatu na zote zina majina ya watuhumiwa wanaouza madawa ya kulevya wengine wametoka Dar es salam na wengi hapa Zanzibar” ameongezea.

Sambamba na hayo amewaonya baadhi ya watendaji wa jeshi la polisi wanaojihusisha na matendo hayo na kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.


 

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *