habari

Mazishi Ya Winnie Mandela Yafanyika.

on

Mwanaharakati wa harakati za kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Winnie Madikizela-Mandela anazikwa leo Jumamosi.

Madikizela-Mandela, shujaa wa mapambano ya kudai uhuru wa Afrika Kusini na mke wa zamani wa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini Nelson Mandela, alifariki dunia Aprili 2 akiwa na umri wa miaka 81. Maelfu ya waombolezaji wamekusanyika katika uwanja wa mpira wa miguu wa Soweto ulio karibu na makazi ya Winnie Madikizela-Mandela.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, alitarajiwa kuhutubia katika mazishi hayo. Marais wa zamani Jacob Zuma na Thabo Mbeki pia nao walihudhuria, ambapo pia Viongozi wa kigeni wanaotarahiwa kuhudhuria mazishi hayo ni pamoja na rais wa Congo Brazzaville Denis Sassou Nguesso, waziri mkuu wa taifa jirani la Lesotho Pakalitha Mosisili; na wajumbe wengine kutoka serikali za afrika na vyama vya ukombozi.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *