habari

MBUNGE GULAMALI AELEZWA NAMNA CHUO CHA NIT KILIVYOJIPANGA KUWAPOKEA WATALAAM WA BOEING ILI KUWANOA ATCL

on

3
 Mbunge wa Manonga Seif Gulamali akikagua baadhi ya vifaa katika karakana chuoni hapo kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Zacharia Mginilwa.
4
Mbunge wa Manonga Seif Gulamali akiwa katika chumba cha uongozaji wa ndege katika chuo cha usafirishaji (NIT) mara baada ya kufanya ziara  Chuoni hapo.
Na Francis Daudi,
MBUNGE wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali amtembelea Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ambacho kimejidhatiti kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya Usafirishaji nchini Tanzania kwa kuzalisha wataalamu wengi zaidi ikiwa ni sehemu ya mkakati wao wa kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya tano katika kujenga Tanzania ya Viwanda.
Akizungumza leo chuoni hapo baada ya kupokelewa na Mkuu wa chuo hicho Profesa Zacharia Mginilwa, Gulamali amesema amefurahishwa na utendaji kazi sambamba na mikakati iliyopangwa katika kuhakikisha sekta ya usafirishaji inakua zaidi.Amesema kuwa amefurahi kuona chuo alichosoma kinaendelea kuzalisha wataalamu zaidi katika sekta ya usafirishaji ambayo inachangia uchumi wa Taifa kwa asilimia kubwa.
Pia chuo hichokinaonesha jitihada za kuunga mkono juhudi za Rais Dkt John Magufuli na amehaidi kutoa ushirikiano wa hali na mali pindi itakapohitajika.
Akiwa Chuoni hapo Gulamali alipata fursa ya kutembelea Shule ya usafiri wa anga (School of Aviation) yenye madarasa ya waendesha ndege, karakana maalumu za kutengeneza injini za ndege na baadaye alitembelea idara ya ukaguzi wa magari na kueleza kufurahishwa na utendaji kazi unaofanywa kwa kutumia teknolojia ya juu.
Akieleza historia ya Chuo hicho, Mkuu wa Chuo Profesa Zacharia Mganilwa amesema kilianzishwa mwaka 1975 na ni miongoni mwa vyuo vya mwanzo kabisa kuanzishwa na Rais wa Awamu ya Kwanza Mwalim Julius Nyererere kwa lengo la kuhakikisha vinakuza sekta ya usafirishaji nchini.
Profesa Mginilwa amesema mipango ya Chuo hicho na hatua walizofikia ni kuhakikisha kinakuwa Chuo Kikuu cha Usafirishaji nchini Tanzania na Afrika.Ameongeza kuwa chuo hicho kimepata fedha karibu Sh.bilioni 140 toka Serikali ya China ili kujenga majengo na kuimarisha miundo mbinu katika chuo hicho na Kuwa Chuo Kikuu cha Usafirishaji.
Profesa Mganilwa amefafanua wamejikita pia katika kuzalisha wataalamu bora zaidi ili kwenda na kasi ya Serikali katika kujenga miundombinu bora ya usafiri nchini.Pamoja na mambo mengine pia chuo hicho kimeanzisha kozi zinazoendana na uhitaji wa soko la ajira kama vile Shahada ya Marekebisho ya Ndege na Shahada ya Elimu katika Hisabati na Teknolojia ya Mawasiliano.
Ameongeza kuwa fani hizo ni sehemu ya fani nyingi zilizopo chuoni hapo ambazo hazipatikani katika Chuo chochote hapa nchini na kuongeza wamepeleka wataalamu katika nchi za China, Korea na Japan ili kuongeza ujuzi katika Uzamili na Uzamivu ili kuimarisha idara mbalimbali ndani ya Chuo cha NIT.
Chuo cha NIT kimepokea takribani Sh.milioni 400 kutoka Benki ya Dunia na Mashirika ya ndege duniani ili kusaidia kuzalisha zaidi wataalamu bora katika sekta ya usafirishaji hasa wa usafiri wa anga na kinatarajia kupokea wataalamu kutoka Shirika la Boeing ambao watatoa mafunzo kwa wataalamu na wafanyakazi wa Shirika la Ndege(ATCL).
Na hiyo inatokana na chuo hicho kuwa miundo mbinu na vifaa bora vya kufundishia masuala mbalimbali katika usafiri wa anga.Mkuu wa Chuo hicho amemshukuru na kumpongeza Gulamali kwa kuwa kijana mchapakazi na anayehamasisha maendeleo na kwamba amekuwa chachu kubwa kwa wanafunzi wa chuo hicho ambacho alisoma miaka 8 iliyopita.
Amemuomba asichoke kutembelea na kutoa mawazo yake katika kujenga na kuimarisha sekta ya usafirishaji nchini.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *