habari

Mfungwa Mwenye Miaka 83 Anyongwa.

on

Mfungwa aliyekuwa na umri wa miaka 83 Walter Moody, amenyongwa baada ya kutiwa hatiani kwa mauaji ya jaji wa Marekani na wakili kutumia mabomu ya paipu. Adhabu hiyo imetolewa na Serikali ya jimbo la Alabama nchini Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kituo cha taarifa za hukumu ya kifo, Moody ni mtu mwenye umri mkubwa kabisa kunyongwa nchini Marekani tangu nchi hiyo iliporuhusu tena adhabu ya kifo katika miaka ya 1970, akichukua nafasi ya John Nixon aliyenyongwa akiwa na umri wa miaka 77 mnamo 2005. Afisi ya gavana wa jimbo la Alabama, Kay Ivey, imesema katika taarifa kwamba Walter amenyongwa kwa mauaji ya jaji wa mahakama ya shirikisho Robert Vance.

Jaji huyo aliuliwa pamoja na mkewe wakati bomu lilipolipuka nyumbani kwao Birmingham, Alabama mnamo Desemba 1989. Wakili Robert Robinson aliuwawa kwa njia hiyo siku mbili baadaye mjini Savannah katika jimbo la Georgia.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *