habari

Mganga Mfawidhi Hospitali Ya Wilaya Kakonko-Kigoma Akutwa Amejinyonga.

on

Mejo Banikira (43) Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kakonko, mkoani Kigoma, amekutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia taulo yake.

Taarifa za tukio hilo zimebainishwa leo May 29 na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala wakati akizungumza na wanahabari, ambapo amesema uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea ili kubaini chanzo cha daktari huyo kujiua.

“Mwili wa Dk Banikira  umeondolewa nyumbani alikojinyongea  na kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Kibondo wakati jeshi la polisi likiendelea na uchunguzi,” amesema.

Amesema taarifa za kujinyonga zimepatikana asubuhi baada ya mke wake anayeishi kwingine, kupiga simu kwa muda mrefu bila kupokelewa, na kwamba alipoona simu haipokelewi, aliwapigia simu majirani ambao walikwenda na kukuta milango imefungwa, ndipo waliporipoti polisi na polisi ndiyo waliobaini mwili wake.

“Watu wasichukulie kujinyonga kuwa suluhisho la matatizo katika familia bali waeleze masahibu yao kwa marafiki na viongozi waweze kusaidiwa na kurejea maandiko ya misikitini au makanisani,”amesema Ndagala.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Joseph Tutuba amesema marehemu alikuwa akiishi peke yake katika nyumba za kupanga mjini Kakonko na alikuwa amewasili kituoni hapo miezi minane iliyopita akitokea wilayani Simanjiro.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *