habari

Mhasibu Takukuru Kusherehekea Mwaka Mpya mahabusu

on

Kesi inayomkabili Mhasibu Mkuu wa zamani wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai, na wenzake watatu, imeahirishwa kusikilizwa ushahidi wa Jamhuri mpaka Januari 10, mwakani itakapotajwa.
Kwa mantiki hiyo, mhasibu huyo na wenzake watasherehekea Mwaka Mpya wa 2019 wakiwa mahabusu.
Gugai na wenzake, wanakabiliwa na mashtaka ya kutakatisha fedha na kumiliki mali zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 3.6 tofauti na kipato chake.
Kesi hiyo ilitajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Janeth Mtega, baada ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba, aliyepangiwa kusikilizwa kesi hiyo kwenda likizo.
Wakili wa Serikali, Peter Vitalis, alidai kuwa kesi hiyo imepangwa kwa ajili ya kutajwa kwa sababu hakimu anayeisikiliza amekwenda likizo.
Hakimu Mtega alisema kesi hiyo itatajwa Januari 10, mwakani na washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu.
Mbali na Gugai, washtakiwa wengine ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yassin Katera.
Katika kesi ya msingi, Gugai na mwenzake wanakabiliwa na mashtaka 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *