We have 281 guests and no members online

BONDIA IBRAHIMU TAMBA KUPAMBANA NA BARAKA MWAKANSOPE

Published in Michezo

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Ibrahimu Tamba anapanda tena uringoni Novemba 22 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam kugombania mkanda wa ubingwa na bondia Baraka Mwakansope kutoka Mbeya kg 73 mpambano uho wa raundi kumi

unatalajiwa kuwa wa kisasi baada ya mara ya kwanza Tamba kumsambalatisha bondia Maisha Samsoni wa uko uko Mbeya hivyo mwakansope amekuja kwa ajili ya kulipiza kisasi cha kupigwa kwa mwenzake mpambano uliofanyika mwanzoni mwa mwaka huu

mratibu wa mpambano uho Jaffar Ndame ameongeza kwa kusema kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mawili ya ubingwa ambapo bondia Julius Kisalawe atapambana na Ramadhani Kumbele kg 51 ubingwa wa Taifa mpambano wa raundi kumi

mpambano mwingine utawakutanisha bondia Pius Kazaula wa Morogoro atakaepambana na Abdallah Luwanje wakati bondia chipkizi kutoka Super D Boxing Promotion Vicent Mbilinyi atakabiliana na Said Tampoo kutoka bagamoyo

aliongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya mabondia chipkizi mbali mbali pia kutakuwa na burudani za kutosha hivyo kawaomba wapenzi na mashabiki wa mchezo wa masumbwi kuwai ukumbini kwa michezo itanza rasmi kuanzia saa 11 jioni na kumalizika mnamo saa tano kasoro usiku

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile

Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha.(P.T)

STARS YAENDELEA KUJIFUA SAUZI

Published in Michezo

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Charles Boniface Mkwasa ameendelea na mazoezi ya kukinoa kikosi chake kujiandaa na mchezo dhidi ya Algeria Novemba 14 jijini Dar es salaam kuwania kufuzu kwa kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018.

Baada ya kufanya mazoezi kutwa mara mbili (asubuhi na jioni) kwa siku tatu, leo Ijumaa kocha Mkwasa amekiongoza kikosi chake kufanya mazoezi mara moja wakati wa jioni katika uwanja wa Edenvale.

Mkwasa amesema baada ya kufanya mazoezi ya kujenga mwili, stamina, na pumzi sasa kazi anayoifanya ni kutengeneza mfumo wa kikosi chake kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Mbweha wa Jangwani.(VICTOR SIMON)

Read more...

'FREESTYLE FOOTBALL CHAMPIONSHIP' KUANZA HIVI KARIBUNI

Published in Michezo

IMG_20151022_190217

Tanzania Freestyle football championship (TFFC2016) ambalo ni shindano la kutafuta/kusaka vipaji vya kuchezea mpira yaani freestyle soccer/Freestyle Football wengi hupenda kuita hivyo ambalo linatarajiwa kuendeshwa kama vile mashindano mengine ya kutafuta vipaji kwa njia mbalimbali ikiwemo ile ya TV show.

Waweza wasiliana nao kupitia anuani hapa +255 654 955 825/ +255 655 049 647

IMG_20151010_014924

IMG_20151010_022504

SCREEN MASTERS WALIPAMBA BASI LA MBEYA CITY

Published in Michezo

11218903_963430877028605_2270729444866256425_n

Wafanyakazi wa kampuni ya Screen Masters Limited ya jijini Dar wakiendelea kulipamba basi la Mbeya City. 

12079536_963430803695279_6917505578594463550_n

Basi la klabu ya Mbeya City FC baada ya kupambwa na kampuni ya Screen Masters Limited ya Dar es Salaam tayari kuanza shughuli ya kusafirisha wachezaji wa timu hiyo kwa safari za ndani na nje ya Mbeya kwenye mechi mbalimbali za Ligi Kuu Bara.

(PICHA: SAID MDOE)-GPL(P.T)

FASTJET KUISAFIRISHA TAIFA STARS KWENDA ALGERIA

Published in Michezo

 Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu timu ya taifa Taifa Stars kwenda nchini, Algeria kwa mchezo utakaofanyika Novemba 17 mwaka huu.

Katibu wa Kamati ya Timu ya Taifa Stars, Teddy Mapunda (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu timu hiyo kwenda nchini Algeria kushiriki  mchezo wa marudiano utakaofanyika Novemba 17  mwaka huu. Kampuni ya Ndege ya Fastjet imedhamini safari hiyo kwa kutoa ndege yake kwa kwenda na kurudi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati na Kushoto ni Mkuu wa Masoko wa Fastjet, Jan Petrie.

 Mkurugenzi Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati (katikati),akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kudhamini timu ya Taifa Stars kwenda na kurudi  nchini Algeria kwa ndege yake kushiriki  mchezo wa marudiano utakaofanyika Novemba 17  mwaka huu. Kulia ni Katibu wa Kamati ya Timu ya Taifa Stars, Teddy Mapunda na Mkuu wa Masoko wa Fastjet, Jan Petrie. 

 Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.

Mkutano ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Ndege ya Fastjet imetoa ndege kwa ajili ya kuisafirisha timu ya Taifa, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wake na timu ya Taifa ya nchi hiyo.Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi  Mkurugenzi Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati alisema hatua ya kuisaidia timu hiyo ni mwanzotu wa ushirikiano baina ya kampuni hiyo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

"Kampuni yetu imeanza ushirikiano na TFF katika kukuza michezo nchini na ndio maana tumeanza kuwasafirisha wachezaji hao kwenda nchini humo kwa ajili ya mchezo huo" alisema KibatiKatibu wa Kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda alisema safari ya kwenda nchini humo itakuwa Novemba 16 na kuwa mchezo huo utafanyika Novemba 17.

Alisema gharama za kusafiri na timu hiyo kwa mtu atakayependa kusafiri ni dola 800 kati ya hizo dola 640 ni kwa ajili ya safari na 60 ni malipo ya kodi ya uwanja wa ndege hapa nchini na Algeria.

Alisema safari hiyo itaanza asubuhi na kuwa ndege hiyo watakayosafiri nayo inabeba abiria zaidi ya 150.(P.T)

Blatter: Tulijadili kombe la dunia la Russia2018

Published in Michezo

Blatter amekiri kuwa katika kikao cha kamati ya FIFA mwaka wa 2010 urusi ilijadiliwa kama mwenyeji wa kombe la dunia la 2018Rais wa FIFA Sepp Blatter amekiri kuwa uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2018 wa Urusi ulijadiliwa hata kabla ya kura ya kutangazwa kwa wenyeji wa kombe la dunia.

Rais huyo ambaye kwa sasa amepigwa marufuku na kamati ya uadilifu ya FIFA ameiambia shirika la habari la Urussi TASS, kuwa jopo zima la kutoa uwenyeji wa fainali za kombe la dunia ulikaa na kujadili mwaka wa 2010 nia ya kuzishirikisha mataifa hasimu Urusi na Marekani katika maandalizi ya kombe la dunia.

''hata hivyo shinikizo kutoka kwa wadau ndio iliyobadilisha matokeo ya uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2022 kutoka Marekani na kwenda Qatar'' Alisema kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 79.

Rais huyo raia wa Uswissi anatumika marufuku ya siku 90 kwa pamoja na msaidizi wake ambaye ni rais wa shirikisho la soka la bara Ulaya Michel PlatiniRais huyo raia wa Uswissi anatumika marufuku ya siku 90 kwa pamoja na msaidizi wake ambaye ni rais wa shirikisho la soka la bara Ulaya Michel Platini.

Wawili hao wamekanusha madai yote dhidi yao.

Na alipoulizwa kama ilikuwa ni kosa kutoa uwenyeji wa kombe la dunia wa mwaka wa 2018 na 2022 kwa pamoja Blatter alisema

''Nia yetu ilikuwa kuandaa makala yajayo ya fainali za kombe la dunia katika mataifa mawaili yenye uwezo mkubwa duniani.''

''Nia yetu ilikuwa kuandaa makala yajayo ya fainali za kombe la dunia katika mataifa mawaili yenye uwezo mkubwa duniani.'' Blatter''Wanakamati walishauri kuwa ni bora fainali zijazo zichezwe Urusi kwa sababu fainali hizo hazijawahi kuandaliwa Mashariki mwa bara Uropa.''

''2022 tungerejea Marekani., ila kwa sababu moja au nyingine ushawishi ulisababisha kura 4 muhimu za wanakamati kutoka bara ulaya kuendea Qatar.''

Tayari utoaji zabuni za uwenyeji wa fainali hizo mbili zinachunguzwa na utawala wa Uswisi.BBC

MKWASA AITA 28 STARS KUIVAA ALGERIA

Published in Michezo

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza kikosi cha wachezaji 28 watakoingia kambini Jumapili jioni kujiandaa na mchezo dhidi ya Algeria Novemba 14 jijini Dar es salaam, na marudiano kufanyika Novemba 17 nchini Algeria.

Akiongea na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam, Mkwasa amesema kikosi chake hicho kitaweka kambi nchini Omani kwa takribani siku 10 kujiandaa na mchezo kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018 dhidi ya Algeria.

Katika kikosi hicho, Mkwasa amewaita wachezaji wapya sita wakiwemo Salim Mbonde, Jonas Mkude, Salum Abubakar, Elias Maguri, Ramadhani Kessy na Malimi Busungu na kufanya idadi ya wachezaji 28.

Wachezaji aliowaita ni Magolikipa ni Ally Mustafa (Yanga), Aishi Manula (Azam), Said Mohamed (Mtibwa Sugar), walinzi wa pembeni Kessy Ramadhani, Mohamed Hussein (Simba), Juma Abdul, Haji Mwinyi (Yanga) na Shomari Kapombe (Azam), Walinzi wa kati ni Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Hassan Isihaka (Simba), Kelvin Yondani na nahodha Nadir Haroub (Yanga).

Viungo ni Salum Telela (Yanga), Salum Abubakar, Himid Mao, Mudathir Yahya, Frank Domayo (Azam), Jonas Mkude na Said Ndemla (Simba), washambuliaji wa pembeni Farid Musa (Azam), Saimon Msuva (Yanga) na Mrisho Ngasa (Free State Stars – Afrika Kusini).

Washambuliaji wa kati ni John Bocco (Azam), Elias Maguri (Stand United), Ibrahim Hajibu (Simba), Malimi Busungu (Yanga), Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe – Congo DR).(P.T)

TWIGA KUCHEZA NA MALAWI NOVEMBA 7

Published in Michezo

Timu ya Taifa Tanzania ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars) inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Wanawake ya Malawi Novemba 7, 2015 jijini Dar es salaam.

Mchezo huo wa kirafiki ni sehmu ya kujipima kwa Twiga Stars inayonolewa na kocha Rogasian Kaijage, ambayo ilishiriki Fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) mwezi Agosti – Septemba nchini Congo – Brazzavile.

Awali Twiga Stars ilikua icheze mchezo huo nchini Malawi Oktoba 24, kabla ya chama cha soka nchini humo (FAM) kuahirisha mchezo huo, na sasa mchezo huo utacheza nchini Tanzania Novemba 07, 2015.(P.T)

Australia yatinga fainali za Raga dunia

Published in Michezo

Australia yaichapa Argentina mchezo wa Raga

Timu ya taifa ya Australia ya mchezo wa raga imetinga hatua ya fainali ya michuano ya kombe la dunia la mchezo huu.

Australia walishuka dimbani kukabiliana na timu ya taifa ya Argentina na kuibuka kidedea kwa pointi 29 dhidi ya 15 za wapinzania wao.

Mchezaji mahiri wa Australia Adam Ashley-Cooper, aliisaidia timu yake kupata alama 13 za kuongoza mchezo huu wa nusu fainali.

Australia itapamba na New Zealand katika mchezo wa fainali utakaofanyika Octoba 31 huku michezo ya mshindi wa tatu ikifanyika Octoba 30.BBC

MANCHESTER UNITED NA CITY ZATOKA 0-0 ENGLAND

Published in Michezo

Mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney akimruka beki wa Manchester City, Bacary Sagna katika mechi ya Ligi Kuu ya England jioni ya jana kwenye Uwanja wa Old Trafford. Timu hizo zimetoka 0-0 na kufanya ligi kuendelea kuwa na ushindani mkubwa (P.T)

MATOKEO LIGI YA MABINGWA ULAYA JANA

Published in Michezo

Mesut Ozil akipiga ngumi hewani baada ya kuifungia bao la Arsenal dhidi ya Bayern Munich PICHA ZAIDI GONGA HAPA

TIMU ya Arsenal imeichapa mabao 2-0 FC Bayern Munich usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya, uliofanyika Uwanja wa Emirates, London.

Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Olivier Giroud dakika ya 77 na Mesut Ozil dakika ya nne ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida za mchezo.

Huo unakuwa ushindi wa kwanza kwa Arsenal katika kundi hilo baada ya kufungwa mechi mbili za awali, lakini inaendelea kushika mkia wakati Bayern Munich inaendelea kukaa kileleni.

Mchezo mwingine wa kundi hilo, Olympiacos ya Ugiriki imeshinda 1-0 ugenini dhidi ya Dinamo Zagreb, bao pekee la Brown Ideye dakika ya 79 Uwanja wa Maksimir.

Kiungo wa Barcelona, Ivan Rakitic (kulia) akipongezwa na mchezaji mwenzake Jordi Alba baada ya kufunga mabao mawili dhidi ya BATE Borisov PICHA ZAIDI GONGA HAPA

Mabao mawili ya kipindi cha pili ya Ivan Rakitic dakika ya 48 na 64, yamewapa mabingwa watetezi, Barcelona ushindi wa ugenini wa 2-0 dhidi ya BATE Borisov Uwanja wa Borisov Arena katika mchezo wa Kundi E.(P.T)

Read more...

Pistorious aondoka gerezani

Published in Michezo

Pistorious aruhusiwa kuondoka gerezani

Mwanariadha mlemavu nchini Afrika Kusini Oscar Pistorius ameruhusiwa kuondoka gerezani mwaka mmoja tu baada ya kufungwa jela kwa kosa la kumpiga risasi na kumuuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Aliachiliwa huru Jumatatu usiku badala ya Jumanne kama wengi walivyotarajia. Baada ya kuachiliwa huru, alielekea kwa mjomba wake Arnold Pistorius.

Pistorius ameruhusiwa kukamilisha kifungo chake cha miaka 5, akiwa nyumbani kwake.

Kama sehemu ya msamaha huu bingwa huyo wa zamani wa mbio za walemavu atahitajika kukaguliwa kisaikolojia kila baada ya kipindi fulani

Mwanariadha huyo alipatikana hatia mwezi Octoba mwaka ya kumuua bila kukusudia mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Kama sehemu ya msamaha huu bingwa huyo wa zamani wa mbio za walemavu atahitajika kukaguliwa kisaikolojia kila baada ya kipindi fulani na hatawahi kuruhusiwa kumiliki bunduki.

Familia yake imekanusha madai kuwa ameachiliwa mapema ikisema kuwa japo hayumo gerezani angali anatumikia kifungo chake nyumbani.

Familia yake imekanusha madai kuwa ameachiliwa mapema ikisema kuwa japo hayumo gerezani angali anatumikia kifungo chake

Msemaji wa familia hiyo amesema kuwa hajapunguziwa kifungo na atatumikia kipindi hicho kwa uadilifu kulingana na sheria za taifa.

Hata hivyo bingwa huyo wa zamani anakabiliwa na hatari ya kurejeshwa gerezani iwapo kiongozi wa mashtaka atafaulu kubatilisha uamuzi wa mahakama ya chini iliyompata na hatia ya kuua bila kukusudia Steenkamp.BBC

Karibu Mjengwablog

Uchambuzi wa Soka

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA