We have 447 guests and no members online

TFF YATUMA RAMBIRAMBI COASTAL UNION

Published in Michezo

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetuma salam za rambirambi kwa mwenyekiti wa klabu ya Coastal Union, Dr Twaha Ahmed kufuatia kifo cha mchezaji Mshauri Salim aliyefariki jana jioni jijini Tanga.

Katika salam hizo za Rais wa TFF Jamal Malinzi kwenda kwa uongozi wa klabu ya Coastal Union, amewapa pole wafiwa ndugu jamaa na marafiki pamoja na uongozi wa klabu hiyo na kusema TFF wako nao pamoja katika kipindi hichi cha maombelezo.

Marehemu Mshauri Salim alikuwa mchezaji wa kikosi cha vijana (U20) cha Coastal Union, alifariki jana jioni wakati akipelekwa hospitali baada ya kuanguka uwanjani wakati wa mchezo wa utangulizi wa timu yake dhidi ya timu ya Eagle Academy ya jiji humo.

Kabla ya umauti kumfika, Mshauri aligongana na mchezaji wa timu ya Eagle Academy na kutolewa nje kwa matibabu, ambapo aliweza kurudi uwanjani na kuendelea na mchezo huo kabla ya kuanguka peke yake tena uwanjani na kufariki akiwa njiani kupelekwa hospitalini.(P.T)

VPL: YANGA 2-0 SIMBA, DAKIKA 90 ZIMEKWISHA

Published in Michezo

SIMBA YANGA (3)

Kikosi cha timu ya Yanga

SIMBA YANGA (4)

Kikosi cha timu ya Simba.(P.T)

Read more...

BARCA YATULIZWA LA LIGA, YAPOKEA KIPIGO CHA MBWA MWIZI

Published in Michezo

Messi vs Celta Vigo

Barcelona wamechpwa bao 4-1 na Celta Vigo kwa mara ya kwanza msimu huu kwenye mechi za ligi ya Hispania marufu kama La Liga mchezo uliochezwa Jumatano usiku.

Nalito alianza kuifunga timu yake ya zamani na kuipa Celta Vigo bao la kuongoza huku akimtengenezea Iago Aspas mabao mengine mawili kwenye mchezo ambao safu ya ulinzi ya Barcelona inayoongozwa na Gerard Pique ikionekana kuyumba.

Shuti la Lionel Messi liligonga mwamba mapema mwa kipindi cha pili huku mlinda mlango wa Celta Vigo Sergio Alvarez akiokoa michomo kadhaa kabla hajafungwa na Neymar wakati wenyeji Celta wakikamilisha ushindi wao wa goli 4-1 kwa goli la dakika za lala salama lililofungwa na John Guidetti aliyeingia akitokea benchi.

Ushindi huo kwa Celta unawafanya wafikishe pointi 13 kwa mechi tano ambazo wamecheza hadi sasa katika msimu huu wakati kichapo hicho kwa upande wa Barcelona kinakuwa ni cha kwanza kufuatia kuanza ligi vyema kwa ushindi wa michezo minne iliyopita.

Celta walianza vyema mchezo huo lakini Barcelona walitengeneza nafasi dakiza za mwazo za kipindi cha kwanza. Iniesta alikimbia na mpira kabla ya kumuwekea Messi pasi murua lakini shuti lake liliokolewa na golikipa wa Celta Sergio Alvarez.(P.T)

HATIMAYE LIGI DARAJA LA KWANZA YAPATA MDHAMINI

Published in Michezo

Mkurugenzi mkuu wa Star Times Llao Lan Fang (kuhoto) na Rais wa TFF Jamal Malinzi wakisaini mkataba wa udhamini wa ligi daraja la kwanza Tanzania bara

Mkurugenzi mkuu wa Star Times Liao Lan Fang (kuhoto) na Rais wa TFF Jamal Malinzi wakisaini mkataba wa udhamini wa ligi daraja la kwanza Tanzania bara

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limesaini mkataba wa udhamini wa ligi daraja la kwanza (FDL) na kampuni ya Star Times Media wenye thamani ya shilingi milioni miatisa za kitanzania kwa muda wa miaka mitatu ili kusaidia gharama za uendeshaji wa ligi hiyo.

Utiaji saini huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa Kisenga Millennium Towers, Makumbusho kati ya TFF na Star Times.

Llao Lang Fang akibadilishana mkataba na  Rais wa TFF Jamal Malinzi

Liao Lang Fang akibadilishana mkataba na Rais wa TFF Jamal Malinzi

Rais wa TFF Jamal Malinz ameishukuru Star Times kwa kukubali kudhamini ligi hiyo ili kuzisaidia timu shiriki  kujikimu pamoja na bodi ya ligi kuwalipa waamuzi pamoja na garama nyingine za uendeshaji wa ligi hiyo ambazo zimekuwa zikibebwa na TFF kwa miaka yote.(P.T)

Read more...

CAPITAL ONE CUP-KUENDELEA LEO

Published in Michezo

CAPITALONECUP-CHELSEA2015

RAUNDI ya 3 ya Kombe la Ligi, sasa huitwa CAPITAL ONE CUP, itarindima Jumanne na Jumatano huko England nah ii ndio Raundi ambayo Vigogo wa Ligi Kuu England huanzia.

Ingawa baadhi ya Timu za Ligi Kuu England zilianza Raundi ya Pili, wale Vigogo, wakiwemo Mabingwa Watetezi, huanzia Raundi ya 3.

Jumanne zipo Mechi 16 za Raundi hii na Jumanne zipo 8 na baadhi yao ni ile Dabi ya Jiji la Birmingham kati ya Aston Villa na Birmingham City.(VICTOR)

Read more...

WADAU WA MICHEZO WATAKIWA KUISAIDIA SERIKALI KUKUZA MICHEZO

Published in Michezo

unnamedH

KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mushi (Kulia) akikadhi cheti cha Tuzo kwa mdau, Abbas Ally wa Kampuni ya Isere Sports inayouza vifaa vya michezo aliyeshiriki kufanikisha mkoa wa Dar es Salaam kutwaa ubingwa wa jumla katika mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) ysaliyofanyika mkoa wa Mwanza mapema mwaka huu na DAr es Salaam kutwa ushindi wa jumla kwa kujikusayia medali 26.

WADAU wa Michezo mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kujitokeza kuisaidia Serikali kukuza michezo na kufufua vipaji vya wachezaji katika fani mbalimbali katika shule za msingi na Sekondari.(VICTOR)

Read more...

MAKUNDI MATANO YATINGA FAINALI YA DANCE100%‏

Published in Michezo

MAJOKELI: Baadhi ya Vijana wanaounda kundi la Majoker Crew la Msasani Wilaya ya Kinondoni, wakikongo nyoyo za mashabiki wakati wa nusufainali ya shindano la Dance 100% 2015 lililoandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania lilifanyika kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Ambapo makundi matano(5)yaliingia fainali itakayofanyika mwezi wa kumi.

MAKOLOKOCHO; Wasanii wa Kundi la Makolokocho jijini Dar es Salaam, wakionyesha umahiri wao wa kusakata dansi wakati wa Nusu fainali ya shindano la Dance 100% 2015 lililoandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania lilifanyika kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Ambapo makundi matano(5)yaliingia fainali itakayofanyika mwezi wa kumi.

CUTE BABYS: .Wasichana wanaounda kundi la cute Babies kutoka Keko wilaya ya Ilala wakionyesha mbwembwe zao wakati wa Nusu fainali ya shindano la Dance 100% 2015 lililoandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania lilifanyika kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Ambapo makundi matano(5)yaliingia fainali itakayofanyika mwezi wa kumi

Vijana wanaounda kundi la The Winner Crews kutoka Kiwarani jijini Dar es Salaam, wakikonga nyoyo za mashabiki waliojitokeza kwenye onyesho la Nusufainali ya shindano la Dance 100% 2015, wakati wa Nusu fainali ya shindano la Dance 100% 2015 lililoandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania lilifanyika kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Ambapo makundi matano(5)yaliingia fainali itakayofanyika mwezi wa kumi.(P.T)

Read more...

SIMBA WAICHAPA KAGERA SUGAR 3-1

Published in Michezo

TIMU ya Simba SC jana imeibuka kifua mbele baada ya kuichapa Kagera Sugar mabao 3-1 katika mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara iliyopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mabao yote ya Wekundu wa Msimbazi yamewekwa kimiani na mshambuliaji raia wa Uganda, Hamis Kiiza aliyepiga 'hat trick' na kuondoka na mpira wake baada ya mechi.

Bao pekee la Kagera Sugar limefungwa na Mbarak Yusuf.

Kwa matokeo ya jana, Simba wamefikisha jumla ya pointi 9 wakiwa wamecheza michezo mitatu.(P.T)

WASHINDI NDONDO CUP WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

Published in Michezo

Kutoka kulia: Mke wa Dr. Mwaka (Mrs. Mwaka) na Shaffih Dauda (wapili kutoka kulia) wakimkabidhi katibu mkuu wa Faru Jeuri (kushoto) kiasi cha shilingi milioni tano wakiwa ndio mabingwa wa Ndondo Cup msimu huu

Kutoka kulia: Mke wa Dr. Mwaka (Mrs. Mwaka) na Shaffih Dauda (wapili kutoka kulia) wakimkabidhi katibu mkuu wa Faru Jeuri (kushoto) kiasi cha shilingi milioni tano wakiwa ndio mabingwa wa Ndondo Cup msimu huu

Waandaaji na wadhamini wa michuano ya Dr. Mwaka Sports Extra Nondo Cup iliyomalizika hivi karibuni, clinic ya Foreplan kwa kushirikiana na chini ya Dr. Mwaka na Sports Extra ya Clouds FM jana wamekabidhi zawadi kwa washindi wa michuano hiyo pamoja na zawadi binafsi kwa washindi wa zawadi hizo.

Zawadi hizo zimekabidhiwa kwa washindi kwenye ofisi za Clouds Media Group majira ya saa tano asubuhi baada ya taratibu zote za utoaji zawadi hizo kukamilika kwa asilimia zote.

Ashindi wa michuano hiyo timu ya Faru Jeuri imejichukulia kitita cha shilingi milioni tano, washindi wa pili timu ya Kauzu FC wametwaa shilingi milioni tatu huku washindi wa tatu timu ya Makumba FC wao wakipata shilingi milioni mbili kwa kuibuka washindi wa tatu.

Zawadi nyingine zilitolewa kwa kikundi bora cha ushangiliaji ambayo imekwenda kwa kikundi cha Kauzu FC, mfungaji bora akiwa ni Idd Mbaga, mwamuzi bora na golikipa bora wote wakijinyakulia vitita vya shilingi laki tano (500,000) kila mmoja.(P.T)

CHELSEA YAILAZA ARSENAL BAO 2- 0

Published in Michezo

2C81337500000578-3241084-image-a-72_1442668448161

Mchezaji wa Chelsea, Kurt Zouma akifunga bao la kwanza dakika ya 53 kipindi cha kwanza dhidi ya Arsenal katika Uwanja wa Uwanja wa Stamford Bridge, London. Chelsea wameshinda bao 2-0 dhidi ya Arsenal.

2C81359600000578-3241084-Kurt_Zouma_rose_highest_to_latch_on_to_Cesc_Fabregas_inch_perfec-a-67_1442668284503

2C8136BC00000578-3241084-image-a-70_1442668305338

...Wachezaji wa Chelsea wakishangilia.

2C80B00400000578-0-image-a-16_1442664358705

Mchezaji wa Chelsea, Alexis Sanchez (katikati) akiwatoka wachezaji wa Chelsea.(P.T)

Read more...

Leo Nimefanya Jogging Kupanda Mlima Gangilonga..!

Published in Michezo

Iringa inapendeza sana kutoka juu mlimani.
Maggid.

Mchezaji wa timu ya soka ya wasichana ya Ilala Rukia Annaph (kushoto) akichuana vikali na mchezaji wa timu ya Temeke Christina Daudi katika mchezo wa nusu fainali ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Temeke ilishinda 2-1

Mchezaji wa timu ya soka ya wasichana ya Ilala Tumaini Michael (Kulia) akimtoka mchezaji wa timu ya Temeke Shamimu Hamis katika mchezo wa nusu fainali ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Temeke iliibukana na ushindi wa magoli 2-1

Mchezaji wa timu ya soka ya wasichana ya ya Ilala Jackline Albert (Kushoto) akimtoka mchezaji wa timu ya Temeke Shamimu Hamis katika mchezo wa nusu fainali ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Temeke ilishinda 2-1.

Karibu Mjengwablog

Uchambuzi wa Soka

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA