We have 264 guests and no members online

Wajawazito kukosa Olimpiki Brazil

Published in Michezo

Wanawake wajawazito wameshauriwa kutosafiri kwenda Brazil kushuhudia mashindano ya Olimpiki mwaka 2016 kwa sababu ya hatari ya virusi vya Zika.

Serikali ya Brazil imesema kuwa hawashauri wanawake wajawazito kwenda kwenye michezo ya Olimpiki jijini Rio De Jeneiro mwezi Agosti

hatua hii imekuja punde baada ya shirika la afya duniani WHO kutangaza hali ya dharura kutokana na madhara yatokanayo na virusi vya Zika.

IMECHOTWA KUTOKA KWENYE MTANDAO WA BBC NA VICTOR SIMON

Washukiwa 50 wa al-Shahab wakamatwa Somalia

Published in Michezo

Washukiwa 50 wa al-Shahab wakamatwa Somalia

Kamanda wa jeshi la polisi wa mji wa Johar nchini Somalia ametangaza kuwa watu 50 wametiwa mbaroni wakishukiwa kuwa na uhusiano na kundi la al Shabab.

Sayad Ndje ameashiria vitisho vya kundi la al Shabab na kueleza kuwa, watu 50 wametiwa mbaroni wakishukiwa kuwa na uhusiano na kundi hilo. Watu hao wamekamatwa katika operesheni ya pamoja iliyofanywa na vikosi vya usalama vya Somalia na wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika katika mji wa Johar kwenye mkoa wa Shabelle ya Kati, huko kusini mwa Somalia.

Kamanda wa polisi wa mji wa Johar ameongeza kuwa vikosi vya usalama vya Somalia hivi sasa vimeimarisha usalama huko Shabelle ya Kati kwa kuzingatia kuweko wawakilishi wa gazi ya juu wa makundi mbalimbali ambao wanashiriki mkutano unaojadili kuundwa serikali mpya katika mkoa huo.

Kundi la al Shabab ambalo limepoteza maeneo mengi yaliyokuwa chini ya udhibiti wake, lingali linaendeleza mashambulizi yake nchini Somalia na katika nchi jirani ya Kenya.(VICTOR)

CHAN 2016: ZAMBIA, TUNISIA NJE, NUSU FAINALI YAKAMILIKA!

Published in Michezo

SAFU ya Nusu Fainali za 2016 African Nations Championship (Chan 2016), ambazo ni Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wachezao ndani ya Afrika, Rwanda, Leo imekamilika baada ya Mali na Guinea kushinda Mechi zao za Robo Fainali.Katika Mechi ya kwanza ya Robo Fainali iliyochezwa Stade Regional Nyamirambo, Mali iliyotoka nyuma kwa Bao 1 la Tunisia lililofungwa Dakika ya 14 na Mohamed Ali Monser, walizinduka na kupiga Bao 2 katika Dakika za 71 na 80 zilizofungwa na Aliou Dieng na kutinga Nusu Fainali ambako watacheza na Ivory Coast hapo Alhamisi.

Kwenye Mechi ya pili ya Robo Fainali iliyochezwa Umuganda Stadium, Guinea waliibuka kidedea kwa Matuta 5-4 dhidi ya Zambia kufuatia Sare ya 0-0 katika Dakika 120 za Mchezo.(VICTOR)

Read more...

WENYEJI wa Fainali za 2016 African Nations Championship (Chan 2016), ambazo ni Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wachezao ndani ya Afrika, Rwanda, wametupwa nje kwenye Robo Fainali huko Stade Amahoro Mjini Kigali baada ya kuchapwa 2-1 na Congo DR katika Mechi ya Robo Fainali iliyochezwa Dakika 120.Congo DR walitangulia kufunga katika Dakika ya 11 kwa Bao la Gikanji Doxa na Rwanda kusawazisha Dakika ya 56 Mfungaji akiwa Ernest Sugira.

Mabao hayo yalidumu hadi Dakika 90 kwisha na zikaletwa Dakika za Nyongeza 30 ambapo Congo DR walishinda 2-1 kwa Bao la Dakika ya 114 la Bompunga Padou.

Congo DR wametinga Nusu Fainali ambayo watacheza na Mshindi kati ya Zambia na Guinea ambao wanakutana Leo huko Umuganda Stadium.

Katika Mechi ya Pili ya Robo Fainali iliyochezwa Stade Huye Cameroun walitandikwa 3-0 na Ivory Coast ambao Bao zao zote zilifungwa katika za Dakika za Nyongeza za 30.

Bao hizo zilipachikwa Dakika za 95, 102 na 112 na Koffi Davy Mahinde Boua, Atcho Hemann Junior Djobo na Yao Serge Nguessan.

Kwenye Nusu Fainali, Ivory Coast watapambana na Mshindi kati ya Tunisia na Mali wanaocheza Leo.(VICTOR)

Read more...

Stadio Giuseppe Meazza huko Jijini Milan Nchini Italy Leo litakuwa dimba Mechi ya Ligi Serie A ambayo ni Dabi ya Jiji hili iliyobatizwa Derby Della Madonnina kati ya AC Milan na Inter Milan Timu ambazo zote huutumia Uwanja huo, maarufu kama San Siro, kama Uwanja wa Nyumbani.Safari hii, tofauti na Miaka ya hivi karibuni, Wapinzani hawa wa Jadi wamezinduka na sasa ni Wagombea wa Ubingwa na Mataji huko Italy.

Lakini, katika kipindi hiki, AC Milan, chini ya Kocha Sinisa Mihajlovic, huku wakimtegemea Andrea Bertolacci ambae ndie msukaji wa muvu zao zote za kwenda mbele, ndio wanaonekana ngangari kupita Inter Milan, iliyo chini ya Kocha Roberto Mancini, ambao wameporomoka kutoka Vinara wa Serie A na sasa kukamata Nafasi ya 4 huku Juzi wakitandikwa 3-0 na Juventus kwenye Mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya Coppa Italia.

Inter Milan wameshinda Mechi 1 tu kati ya 5 walizocheza mwisho.

Msimu uliopita kwenye Mechi kama hii Timu hizi zilitoka Sare 1-1.(VICTOR)

Read more...

Raga:Kenya yaicharaza Canada na Australia

Published in Michezo

Timu ya Kenya ya mchezo wa raga imeicharaza Canada na Ureno 37-7 na 26-5 ili kufika katika robo fainali ya Kombe la Wellington Sevens siku ya jumamosi nchini New Zealand.

Hatahivyo,Kenya ilipoteza mechi yake ya tatu kwa Australia baada ya kufungwa 17-12 katika mechi ya kundi Da.

Wachezaji wa kocha Benjamin Ayimba sasa watakabiliana na wenyeji New Zealnd mapema siku ya jumapili katika robo fainali ya taji kuu.

Australia awali ilikuwa imeishinda Ureno 19-12 na Canada 26-22.

Trai za Collins Injera na Billy Odhiambo, konvashon iliofungwa na Biko Adema iliisaidia Kenya kuongoza dhidi ya canada 12-0 ifikiapo kipindi cha mapumziko.(VICTOR)

LIGI KUU KUENDELEA JUMAMOSI HII

Published in Michezo

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo saba kuchezwa katika viwanja tofauti, ikiwa katika mzunguko wa 16 kwa kila timu kusaka pointi 3 muhimu katika raundi hiyo ya lala salama.

Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Jumamosi hii, Simba SC watawakaribisha African Sports, JKT Ruvu watawakaribisha Majimaji FC uwanja wa Karume, huku Mtibwa Sugar wakiwakaribisha Stand United kwenye uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.

Jijini Tanga, Wagosi wa Kaya Coastal Union watakua wenyeji wa Young Africans uwanja wa Mkwakwani, Mwadui FC watakua wenyeji wa Toto Africans uwanja wa Mwadui Complex, huku wakata miwa wa Kagera Sugar wakicheza dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumapili kwa mchezo mmoja ambapo Maafande wa Mgambo Shooting watawakaribsiha Ndanda FC kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.(P.T)

TIMU ZA ,MAFUNZO NA JKU ZAKABIDHIWA VIFAA VYA MICHEZO

Published in Michezo

dk1

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Vifaa vya Michezo Nahodha wa Timu ya Mafunzo Mpira wa Miguu (Football) Haji Ramadhan Mwambe katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Unguja jana,timu hiyo itashiriki mashindano ya klabu bingwa Afrika kwa kupambana na Timu ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) kwenye Uwanja wa Amaan tarehe 13 Februari, 2016 (katikati) Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Bi.Sharifa Kahamis,[Picha na Ikulu.]

dk2

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Vifaa vya Michezo Nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu JKU Ponsiana Malik Joseph katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Unguja jana,timu ya JKU ambayo inashiriki Kombe la Shirikisho itapambana na timu ya Gaborone United ya Botswana katika uwanja huo huo  wa Amaan Studium tarehe 14 Februari,2016.[Picha na Ikulu.)(P.T) 

SAM

Mbwana Samata amewasili nchini Ubelgiji na kusaini mkataba wa miaka minne na Club  mpya ya FC Genk ili kucheza katika ligi kuu ya nchi hiyo, Ubelgiji  imekuwa moja ya nchi zinazotoa wachezaji wakubwa  ulaya na kikosi cha timu ya Taifa ya nchi hiyo ni moja kati ya timu kali duniani.

Mbwana amesema katika ukurasa wake wa Instagram kuwa anamshukuru Mungu kwa fursa hii na ataitumia vyema ili kujiletea mafanikio na kuleta mafanikio kwa taifa lake pia.
Meneja wa mshambuliaji huyo, Jamal Kisongo, alisema amewasiliana na Samatta na kumweleza kwamba amefika salama na ameanza kufuata taratibu zote ili aweze kufanya kazi nchini humo.

Samatta ambaye alitwaa tuzo ya kuwa Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani, alikubali kujiunga na timu ya KRC Genk na kugomea ofa zilizotolewa na klabu za Nantes na Olympique Marseille za Ufaransa

SAM2

Uganda watupwa nje michuano ya Chan

Published in Michezo

Diarra

Zambia na Mali zimefuzu kwa robo fainali ya michuano ya kombe la taifa bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani baada ya kutoka sare mechi iliyochezwa Jumatano.

Chipolopolo tayari walikuwa wamefuzu kabla ya mechi hiyo nao Mali walijihakikishia nafasi ya kufuzu kwa kupata alama hiyo moja kwa kutoka sare tasa uwanjani Rubavu.

Katika mechi nyingine ya Kundi D, Zimbabwe walitoka sare na Uganda, baada ya Cranes kusawazisha dakika ya 93.

William Manondo alikuwa ameweka Zimbabwe kifua mbele lakini Geofrey Serunkuma akasawazisha dakika za mwisho.

Uganda walihitaji kuishinda Zimbabwe nao Mali washindwe na Zambia ndipo wapate nafasi ya kufuzu.

Kwenye Kundi hilo, Zambia walimaliza kileleni na alama 7, Mali wa pili na alama 5, Uganda tatu na alama 2 nao Zimbabwe wakashika mkia na alama 1.

Mechi za robofainali zitachezwa Jumamosi na Jumapili, mechi inayosubiriwa sana ikiwa kati ya wenyeji Rwanda na majirani wao DR Congo Jumamosi uwanjani Amahoro.(VICTOR)

MABINGWA Watetezi wa Kombe la Mfalme wa Spain liitwalo Copa del Rey, Barcelona, Jana huko Nou Camp walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuichapa Athletic Bilbso 3-1 na kutinga Nusu Fainali wakati Atletico Madrid ikipigwa 3-2 na Celta Vigo na kutupwa nje.Barcelona, ambao walishinda 2-1 Ugenini, Jana walijikuta wako nyuma 1-0 hadi Haftaimu pale Inaki Williams alipoipa Athletic Bilbao Bao lakini Kipindi cha Pili walizinduka na kuitwanga Bilbao Bao 3 kupitia Luis Suarez, Dakika ya 53, Gerard Pique, 81 na Neymar, 90.

Hivyo Barca wametinga Nusu Fainali kwa Jumla ya Mabao 5-2.

Huko Vicente Calderado, Atletico Madrid iliikaribisha Celta Vigo ambayo ilitokanayo 0-0 katika Mechi ya kwanza lakini Jana wakatwangwa 3-2 Nyumbani kwao na kutupwa nje ya Copa del Rey.(VICTOR)

Read more...

Katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya Coppa Italia iliyochezwa huko Juventus Stadium Mjini Torino Nchini Italy, Mabingwa wa Italy Juventus waliichapa Inter Milan Bao 3-0.Bao la kwanza la Mechi hii ambayo Klabu hizi zikikutana huitwa Derby d’Italia lilifungwa kwa Penati ya Dakika ya 36 ya Alvaro Morata.

Penati hiyo ilitolewa baada ya Cuadrado kuangushwa ndani ya Boksi na Murillo mbae alipewa Kadi ya Njano.

Juve walipiga Bao lao la pili Dakika ya 63 Mfungaji akiwa tena Alvaro Morata na kupata mwanya zaidi pale Murillo, katika Dakika ya 70, kulambwa Kadi ya Njano nyingine na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu na kuipa Juve nafasi kupiga Bao jingine 1 katika Dakika ya 83 kupitia Paulo Dybala na kushinda 3-0.

Timu hizi zitarudiana huko San Siro na Mshindi wa Mechi hizi mbili kuingia Fainali.

Katika Mechi nyingine ya Nusu Fainali iliyochezwa Jumanne Usiku, AC Milan walishinda Ugenini 1-0 dhidi ya Alessandrio kwa Bao la Penati ya Dakika ya 43 iliyopigwa na Mario Balotelli.(VICTOR)

Read more...

Karibu Mjengwablog

Uchambuzi wa Soka

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA