We have 254 guests and no members online

C1C: LIVERPOOL, EVERTON KUZIMUDU STOKE NA CITY

Published in Michezo

Liverpool na Everton zinatinga kwenye Mechi za pili za Nusu Fainali ya Kombe la Ligi huko England liitwalo C1C, CAPITAL ONE CUP, huku zikiwa zimeshinda Mechi zao za kwanza.Liverpool walipata ushindi wa Ugenini wa Bao 1-0 walipoifunga Stoke City huko Britannia Stadium kwaBao la ushindi la Jordon Ibe katika Dakika ya 37 akitokea Benchi kumbadili Philippe Coutinho alieumia Msuli wa Pajani

Kwenye Mechi hii ya pili, Liverpool watakuwa kwao Anfield Jumanne Usiku.

Nao Man City watacheza kwao Etihad Jumatano Usiku wakisaka kupindua kipigo cha 2-1 walichopewa huko Goodison Park katika Mechi ya kwanza.

Katika Mechi hiyo, Everton walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 46 la Funer Mori na City kusawazisha kwenye Dakika ya 76 kwa Bao la Jesus Navas.

Lakini Everton walinyakua ushindi kwa Bao la Dakika ya 78 la Romelu Lukaku.

Washindi wa hizi Nusu Fainali watakutana Fainali itakayochezwa hapo Februari 28.

+++++++++++++++++++++++

Nusu Fainali-Kanuni Muhimu:
-Kwenye Mechi za Nusu Fainali, ikiwa Jumla ya Magoli kwa Mechi 2 ni sawa baada ya Dakika 90 za Mechi ya Marudiano, Nyongeza ya Dakika 30 itachezwa.

-Ikiwa Gemu ni Sare baada ya hiyo Nyongeza ya Dakika 30, Mshindi atapatikana kwa kuhesabu Goli la Ugenini kuwa mara mbili.

-Ikiwa Gemu bado itakuwa sawa hata baada ya kuhesabu Goli za Ugenini ni mara mbili, basi Mshindi atapatikana kwa Mikwaju ya Penati 5 kama Sheria za Soka zinavyotamka.(VICTOR)

MAN UTD YAKWAMA TENA OLD TRAFFORD

Published in Michezo

United vs South 2

Klabu ya Manchester United imeshindwa kutamba kwenye uwanja wake wa nyumbani baada ya kujikuta ikigaragazwa kwa bao 1-0 dhidi ya Southampton kwenye mchezo wa ligi kuu England uliochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford.

United vs South 3

Ilimchukua dakika saba na sekunde 43 tu, Charlie Austin kuiandikia bao Southampton akitokea benchi dakika ya 79 kuchukua nafasi ya Mane. Austin aliweka mpira wavuni dakika ya 87 akiunganisha kwa kichwa krosi ya James Ward-Prowse na kuipa ushindi timu yake ikiwa kwenye uwanja wa ugenini.

United vs South 5

Kipigo cha leo kinaifanya Man United kuendelea kubaki nafasi ya 5 katika msimamo wa Ligi, ikiwa na point 37 katika michezo 23. Huo ni mchezo 6 kwa Man United kupoteza toka kuanza kwa msimu wa 2015/2016.(P.T)

Read more...

TOTO AFRICANS WAWANG’OA MAJIRANI ZAO PAMBA

Published in Michezo

Wachezaji wa Toto Africans (Jezi za Njano) wakisalimiana na wachezaji wa Pamba, kabla ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) uliochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza jana. Katika Mchezo huo Toto wamewatupa nje ya michuano hiyo majirani zao Pamba kwa jumla ya magori 4-1.

Magoli ya Toto yamefungwa na Miraji Athuman Madenga aliefunga magoli mawili, Eddo Christopher pamoja na Waziri Junior Shentembo huku bao la Pamba likifungwa na James Sungura.

Kwa matokeo hayo, Pamba wametupwa nje ya Michuano hiyo na Toto wameweza kusonga mbele na kutinga hatua ya 16 bora.

Kamisaa wa mchezo akiwa katika picha ya pamoja na Waamuzi pamoja na Makeptaini wa timu za Pamba na Toto.

Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoani Mwanza (Katikati) akiwa pamoja na viongozi wengine wakifuatilia mchezo kati ya Toto na Pamba

Shambulizi langoni mwa Timu ya Pamba.(P.T)

Read more...

Nyota wa kikapu wa Malawi kuzikabili timu za Dar

Published in Michezo

Mratibu wa Sprite BBall Kitaa Karabani Karabani akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar-es- Salaam kuhusu mechi za kirafiki zitakazochezwa Jumamosi na Jumapili katika uwanja wa BBK Park na timu kutoka Malawi. Wa kwanza kulia waliokaa ni mkurugenzi wa ufundi chama cha mpira wa kikapu Malawi Obed Nyirongo, wengine ni wachezaji wa timu ya Bricks na Brave Hearts.

Mkurugenzi wa ufundi chama cha mpira wa kikapu Malawi Obed Nyirongo  kiongeana waandishi wa  wa habari leo jijini Dar-es- Salaam kuhusu  mechi za kirafiki zitakazochezwa Jumamosi na Jumapili katika uwanja wa BBK Park na timu kutoka Malawi wa Sprite BBall Kitaa. Wa kwanza kushoto waliokaa ni mratibu wa Sprite BBall Kitaa Karabani Karabani na wengine ni wachezaji wa timu ya Bricks na Brave Hearts.

Miamba miwili ya mpira wa kikapu kutoka nchini Malawi imewasili jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya mfululizo wa mechi za kirafiki za kimataifa dhidi ya timu za bigwigs Jogoo, East Zone One, Mbezi na West Zone Three. Mechi hizo zenye hamasa ya aina yake zitachezwa kwenye uwanja Bball Kitaa Park, karibu na Ukumbi wa Gymkhana.

Kulingana na ratiba iliyotolewa na mratibu wa Bball Kitaa Karabani Karabani pazia la michezo hiyo litafunguliwa kesho ambapo East Zone One watakipiga na Bricks, mchezo unaotabiriwa kuwa ni mgumu na wa kusisimua. Siku hiyo hiyo Mbezi watacheza na Associate Team, mchezo ambao pia unatazamiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Michezo hiyo bado itaendelea kuwateka wakazi wa jiji la Dar es Salaam, ambapo West Zone Three watapambana na Bricks kabla ya Jogoo kuwakaribisha Associate team. “Tuna furaha kubwa kuandaa michezo hii ya kirafiki. Ni moja ya sehemu muhimu katika kudumisha mahusiano, vile vile kuendeleza vipaji vinavyochipukia”, Karabani alisema.

Ujio wa Bricks na Associate teams jijini Dar es Salaam imeonekana si jambo geni baada ya timu za East Zone One na West Zone Three kwenda Malawi mwaka jana. Zikiwa nchini humo, timu hizo zilishinda mechi zao kadhaa.

Karabani ambaye michuano yake ya mpira wa kikapu iko chini ya udhamini wa Sprite, amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuibua na kukuza vipaji  vya vijana kwa kipindi cha miaka mitatu ambapo michuano hiyo imekuwa ikifanyika. Vilevile michuano hii inatoa fursa ya kuendeleza ushirikiano baina ya maeneo mbalimbali ya ndani ya nje ya nchi.

 “Lengo letu ni kuanzisha michuano ngazi ya kanda mwishoni mwa mwaka huu, ambapo mabingwa kutoka Tanzania, Malawi, Zambia na Zimbabwe”, Karabani alisema na kuongeza kuwa uzinduzi wa michuano hiyo utafanyika nchini Malawi

Kwa upande wake, Meneja Biashara wa Coca-Cola nchini, Maurice Njowoka alisema anajisikia furaha kubwa kutokana na heshima waliopewa kuisapoti michuano hiyo hapa nchini na kusisitiza kuwa kampuni yake itaendeleza ushirikiano wake na wadau wa mchezo wa kikapu kuzidi kuutangaza mchezo huo.

 “Sote tunafahamu kuwa mpira wa kikapu ni moja ya michezo maarufu na yenye nguvu nchini, hasa miongoni mwa vijana ambao wanahitaji aina hii ya msaada ili kuhamasika na kuweza kuendeleza vipaji vyao”, Njowoka alisema.(P.T)

Habari njema kwa mashabiki wa Chelsea, inamhusu Ivanovic

Published in Michezo

Ivanovic

Branislav Ivanovic.

Na Rabi Hume, Modewjiblog

Mashabiki wa Chelsea popote duniani watakuwa na furaha baadaya beki wa klabu hiyo, Branislav Ivanovic kuongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia timu hiyo yenye makazi yake London, Uingereza.

Mkataba wa awali wa Ivanovic ulikuwa ukimalizika mwishoni kwa msimu huu na baada ya kuongeza mkataba wa mwaka mmoja anataraji kuendelea kuichezea Chelsea mpaka mwishoni kwa msimu wa 2017.

Kabla ya kuongeza mkataba na Chelsea tayari kuna baadhi ya klabi zilikuwa zimeanza kuonyesha nia ya kuhitaji kumsajili beki huyo ambapo baadhi ya klabu hizo ni AC Milan na Inter Milan ambazo zote zilikuwa zimeanza kuonyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo.

Ivanovic alisajiliwa na Chelsea mwaka Januari 2008 akitokea klabu ya Lokomotiv Moscow na ameshaichezea michezo 341 na kufunga magoli 32 huku akiwa ameshinda mataji mawili ya ligi kuu ya Uingereza, Kombe la FA mara nne, Kombe la Capital One mara moja na Kombe la Europe na ligi ya mabingwa Ulaya yote mara moja moja.(P.T)

Prof. Elisante Ole Gabriel akutana na Makamu wa Rais wa FIFA

Published in Michezo

PICS 1

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel kulia akiongea na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Bw. Salman Bin Ebrahim Al Khalifa katikati kuhusiana na maendeleo ya michezo nchini, kushoto ni Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania Bw. Jamali Malinzi. (Picha na Benjamin Sawe-WHUSM).

PICS 3

Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Bw. Salman Bin Ebrahim Al Khalifa katikati akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel kulia kuhusiana na maendeleo ya michezo nchini, wa kwanza kushoto ni Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania Bw. Jamali Malinzi.(P.T)

Mbwana Samatta shujaa wa soka la Afrika anayetokea Tanzania

Published in Michezo

CYPvOH3WsAAObgi

Mbwana Samatta akipokelewa uwanja wa ndege usiku wa kuamkia leo mara baada ya kuwasili akitokea Nigeria, mwenye suti ni Baba mzazi wa Mbwana Samatta, Mzee Samatta.  Aliwasili usiku huo akitokea Nigeria kwenye tukio la utoaji wa tuzo za mwanasoka bora wa Afrika wa mwaka 2015 . Mbwana alifika katika uwanja huo wa JNIA majira ya saa nane usiku.

Na Andrew Chale,Modewjiblog

Tuna kila sababu ya kujivunia Mbwana Samatta kama alama ya Tanzania. Hata hivyo tayari kumekuwa na hali ya kutoeleweka kwa sasa dhidi ya taarifa tata zikiwemo zile za mitandao ya nje kumtambulisha Mbwana Samatta kama raia wa Congo pia wapo walioandika Mbwana Samatta raia wa Tunisia na nchi zingine, lakini pia hata mitandao mingine kushindwa hata kumtaja kama anatokea Tanzania.

Hata hivyo hali hiyo iliamsha hasira za haraka kwa mashabiki na watanzania wengi ambao walichukizwa kwa kushindwa kumtambulisha vyema Mbwana Samatta. Lakini hilo sio ‘issue’ kubwa sana ila kuna hili la ujio wake wa usiku wa manane.

Shujaa wetu wa Afrika, Mbwana Samatta ameweza kuwasili nchini salama kabisa hilo la kumshukuru Mungu. Hata hivyo wengi wa watanzania kupitia mitandao ya kijamii wamelalamikia ujio wake huo wa usiku wa manane wakikosa nafasi ya kumpokea kwa wingi kama wafanyavyo mashujaa wengine wanapowasili kwenye viwanja vya ndege.

Hilo la ujio wa usiku wa manane tusiumize sana vichwa huenda ndio ratiba sahihi ya ndege licha ya watu kudai kuwa  TFF ama serikali ilikuwa na uwezo wa kumbadilishia ndege na akaingia mapema ziadi ya hapo lakini yote kwa yote shujaa wetu amefika salama na amekuja Tanzania na sio Congo ama Tunisia ama huko wanakosema wengine ambao hawamjui vyema Mbwana Samatta.

Kuna hili la kutokuwapo viongozi wakubwa wa Kiserikali wakiwemo waziri ama Katibu mwenye dhamana kushindwa kutokea uwanja wa ndege  najua hilo ni tatizo kwa baadhi ya wananchi waliolalamikia hilo hasa wale waliofika uwanja wa ndege huku kwenye mitandao ya kijamii kukiwa na gumzo kwa nini hawakufika kumpokea ?…. Ok Karibu nyumbani Mbwana Samatta.

CYQ8hjGUkAAA0bF

Mbwana Samatta akipata picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari waliofika kumpokea. Katikati aliyeshika tuzo hiyo ya Mbwana Samatta, Mhariri wa Tanzania Daima, Tullo Chambo akipata picha ya ukumbusho.

12487217_740077572792887_1490024430609475200_o

Baadhi wanahabari wa New Habari wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Dimba na Sport Starehe wakipata picha ya ukumbusho na Mbwana Samatta.(P.T)

KAIJAGE AJIUZULU TWIGA STARS

Published in Michezo

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars), Rogasian Kaijage amejiuzulu nafasi hiyo kuanzia jana baada ya kuomba kwa uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF).

Kaijage aliiongoza Twiga Stars kwenye fainali za michezo ya Afrika (All Africa Games) zilizofanyika nchini Congo Brazzavile Septemba mwaka jana, baada ya kuiondoa timu ya taifa ya Zambia katika hatua ya mtoano.

TFF imesikitishwa na taarifa za kujiuzulu kwa kocha huyo mwenye leseini A ya CAF, ambaye amekuwa akizinoa timu za taifa za wanawake ya wakubwa (Twiga Stars) pamoja na timu ya wanawake wenye umri chini ya miaka ya 20 (Tanzanite) tangu mwaka 2013.

Kufuatia kujiuzulu kwa kocha Kaijage, TFF inaendelea na programu za maendeleo ya soka kwa wanawake, ikiwemo kuendesha ligi ya wanawake (Tanzania Women League).

TFF inamtakia kila la kheri kocha Rogasian Kiajage katika shughuli zake.

Aidha maandalizi ya mchezo kati ya Twiga Stars dhidi ya Zimbambwe yataendelea chini ya kocha atakayeteuliwa kuchukua nafasi yake, mchezo utakaochezwa mwezi Machi mwaka huu na mshindi kucheza na Zambia.

TFF itaendelea kupambania kwenye maendeleo ya soka la wanawake.(P.T)

YULE MWAMUZI ALIYEKATAA BAO LA MTIBWA VS AZAM IMEKULA KWAKE

Published in Michezo

Waam,uzi wa mchezo wa Azam FC vs Mibwa Sugar wakitolewa uwanjani chini ya ulinzi mkali wa jeshi la Polisi

Waam,uzi wa mchezo wa Azam FC vs Mibwa Sugar wakitolewa uwanjani chini ya ulinzi mkali wa jeshi la Polisi

Mwamuzi wa pembeni Dalila Jaffar Mtwana aliyechezesha mechi kati ya Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi watakaoendelea kuchezesha mashindano ya Mapinduzi Cup kufuatia kulikataa bao la Mtibwa Sugar kwenye mchezo uliochezwa siku ya Jumapili January 3, 2015.

Mwamuzi huyo alilikataa bao halali lililofungwa na Kichuya wa Mtibwa Sugar kipindi cha pili cha mchezo huo ambalo lingeipa ushindi timu ya Mtibwa Sugar kwenye mcheo huo ambao ulimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Kukataliwa kwa bao hilo kulizua tafrani kati ya waamuzi waliochezesha mchezo huo dhidi ya wachezaji wa Mtibwa na bechi zima la ufundi hali iliyolazimu jeshi la polisi kuwatoa waamuzi hao uwanjani wakiwa chini ya ulinzi mkali.

Katibu wa kamati ya ZFA Hashim Salum Hashim amemwandikia barua ya kumwondoa kwenye mashindano ya Mapinduzi mwamuzi huyo kutokana na kutokuwa makini kwenye mchezo kati ya Azam FC vs Mtibwa Sugar.

Hapa chini kuna barua kutoka kwa katibu wa ZFA ya kumwondoa kwenye mashindano mwamuzi Dalila Jaffar Mtwana. Shaffihdauda.com(P.T)

Na Magreth Kinabo- MAELEZO

Serikali imepiga marufuku tabia ya baadhi ya hospitali au taasisi binafsi za afya kuwapima wagonjwa wanaotoka hospitali za Serikali vipimo ambavyo hawakuagizwa kuvipima na madaktari kutoka hospitali hizo kwani kufanya hivyo ni kuiongezea Serikali gharama zisizo la lazima.

Tamko hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangala wakati alipofanya ziara ya kutembelea leo kwenye Taasisi ya Saratani ya Ocean Road iliyopo jijini Dares Salaam.

Waziri Kingwangala alitoa agizo hilo baada ya kukutana na mgonjwa ambaye alitakiwa kufanya kipimo cha MRI katika hospitali moja ya binafsi jijini Dar es Salaam, lakini hospitali hiyo ilimpima mgonjwa huyo vipimo vingine ambayo havikupaswa kupimwa.

Alisema fedha zilizotumika kulipia vipimo hivyo vya ziada vingetumika kununulia dawa na vifaa tiba ambavyo vingetumika kuwahudumia wananchi wengi zaidi.

Aidha Naibu Waziri huyo aliwataka watendaji wa afya kutumia utaalamu na ujuzi wao kuaanda mipango ya kuweza kukabaliana na changamoto za sekta ya afya nchini.

“Ni lazima tutumia utaalamu tulioupata katika kupunguza shida za watu katika sekta ya afya. Tumumie elimu tuliyoipata shuleni na vyuoni ili kuboresha maisha ya Watanzania na tumsaidie Rais John Pombe Mafuguli tusisubiri hadi tuambiwe tufanye nini,”alisisitiza.

Mgonjwa huyo ambaye matibabu yake yanalipiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Kitendo cha hospitali hiyo kilionesha kumsikitisha Naibu Waziri huyo kwa kuwa fedha za Serikali ndizo zinazotumika kugharamia vipimo ambavyo, taasisi hiyo haikumwandikia mgonjwa huyo.

“ Hospitali hii imetumia nafasi hiyo ya kupima mgonjwa huyo vipimo ambayo hakuandikiwa na daktari aliyemwona katika taasisi hii. Chakushangaza baadhi ya vipimo ambayo amepimwa vipo katika taasisi hiyo. Hospitali hii imetumia vibaya mfumo wa mfuko huo kwa kumpima mgonjwa huyo vipimo vya ziada,alisema Naibu Waziri Kigwangala.

Aliwataka watendaji wa afya kuhakikisha wanawapeleka wagonjwa wanaotakiwa kupimwa vipimo vya MRI na CT- Scan katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) kwa kuwa hospitali hiyo ina vifaa vya kisasa na vinafanya kazi vizuri kwa gharama nafuu.

Naibu Waziri huyo aliagiza uongozi huo kusitisha malipo ya vipimo hivyo vya ziada kwa kushirikiana na mfumo huo wa NHIF.

“Sitisheni malipo ya vipimo vya ziada katika hospitali hiyo, mgonjwa ni wa taasisi hii anaigiliwa na taasisi nyingine kwa kupimwa vipimo vingine ambavyo havikupaswa kupimwa, hivi ni vijipu vidoovidogo vinatumbuliwa hapahapa,” alisema Waziri huyo.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo alielezwa kwamba taasisi hiyo inakabiliwa na changamoto ya vipimo vya ugunduzi wa saratani na tiba ya satarani, dawa, ambapo alisema atashirikiana na uongozi ili kuweza kukabiliana na matatizo hayo.Pia aliutaka uongozi wa taasisi hiyo na watendaji wa afya pamoja na wizara kufanya kazi kama timu ili kuweza kutatua changamoto zilizopo.(P.T)

Twite apewa cheo kipya Yanga

Published in Michezo

MBUYUTWITE

Kiungo wa Yanga Mbuyu Twite.

Hans Mloli,Dar es Salaam-GPL

UONGOZI wa benchi la ufundi la Yanga umempa cheo cha unahodha, kiungo wa timu hiyo Mbuyu Twite baada ya Haruna Niyonzima kutemwa klabuni hapo.

Awali kabla ya Niyonzima ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda kupewa wadhifa huo cheo hicho kilikuwa mikononi mwa Twite, hivyo hii ni mara ya pili kwa kiraka huyo kuchukua nafasi hiyo.

Twite anatazamiwa kutumia nafasi hiyo kuiongoza Yanga kwenye michezo yote ya Kombe la Mapinduzi na ile ya awali baada ya kurejea kwa Ligi Kuu Bara kutokana na nahodha mkuu, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kuwa majeruhi.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, ameliambia Championi Jumatatu kuwa, cheo hicho kipo kwa Twite kwa muda tu kwa kuwa bado benchi la ufundi chini ya Mholanzi, Hans van Der Pluijm, halijachagua nahodha msaidizi mpaka sasa.

“Twite kwa sasa ndiye anaongoza timu kama nahodha msaidizi baada ya Niyonzima kutemwa, ila atafanya hivyo kwa muda maana bado hajateuliwa nahodha mpya msaidizi atakayesaidiana na Cannavaro,” alisema Saleh.(P.T)

Karibu Mjengwablog

Uchambuzi wa Soka

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA