We have 204 guests and no members online

YANGA YAZIDI KUPAA, TAMBWE HAKAMATIKI

Published in Michezo

Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe (katikati) akipongezwa na wachezaji wenzake Mwinyi Haji (nyuma) pamoja na Deus Kaseke

Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe (katikati) akipongezwa na wachezaji wenzake Mwinyi Haji (nyuma) pamoja na Deus KasekeHamisi Tambwe ameendeleza kasi yake ya ufungaji mara baada ya jana kutupia bao mbili nyavuni wakati Yanga ikichomoza na ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa taifa.

Tambwe alianza kupasia nyavu kipindi cha kwanza akiutendea haki mpira uliopigwa na Simon Msuva ambaye alimzidi mbio beki wa kushoto wa Mbeya City Hassan Mwasapili kisha kuachia krosi ambayo ilimkuta Tambwe akapachika mpira wavuni.

Kipindi cha kwanza kilimalizika huku Yanga wakiwa mbele kwa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City ambao muda mwingi wa kipindi cha kwanza walicheza kwa tahadhari kubwa huku kukiwepo na matukio kadhaa ya kuchelewesha muda.

Kipindi cha pili Tambwe akapachika bao lake la pili kwenye mchezo huo akiunganisha krosi kwa kichwa na mpira huo kumshinda mlinda mlango wa Mbeya City Juma Kaseja kisha kutinga wavuni.(P.T)

Read more...

Oh! Oh! Juma Pondamali Amemkaribisha John Kwenye Mazoezi Yanga..!

Published in Michezo


..Nimemwambia Pondamali, kuwa hata Yanga waje na folk lift, hawataweza kumbeba mwanangu akachezee Jangwani! Pichani tulipokuwa na Jumapondamali, leo mchana. Pamoja na kuwa mimi ni Simba, Juma Pondamali ni golikpa niliyemkubali na ninayeamini kuwa alipokuwa uwanjani aliheshimu kazi yake.
Marry Xmas

Wachezaji wa Barcelona wakishangilia baada ya kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Dunia kwa mara ya tatu baada ya kuwafunga River Plate ya Argentina kwa mabao 3-0

Wachezaji wa Barcelona wakishangilia baada ya kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Dunia kwa mara ya tatu baada ya kuwafunga River Plate ya Argentina kwa mabao 3-0

Lionel Messi amerudi tena kwa kasi ya aina yake kutoka majeruhi na kufunga goli murua huku Barcelona ikiwatungua River Plate ya Argentina kwa 3-0 na kuchukua ubingwa wa Club World Cup kwa mara ya tatu.

Messi alifunga goli lake mnamo dakika ya 36, kabla ya Muruguay Luis Suarez kuongeza mengine miwili  mnamo dakika za 49′, 68′ katika mchezo uliopigwa kunako huko Yokohama.

Neymar, Luis Suarez na Lionel Messi wakishangilia baada ya kupata bao la kwanza lililofungwa na Messi.(P.T)

Jose Mourinho atimuliwa kazi Chelsea

Published in Michezo

Jose Mourinho 2

Jose Mourinho.

Meneja wa Klabu ya Chelsea ya Uingereza, Jose Mourinho amefutwa kazi baada ya klabu hiyo kufululiza kwa matokeo mabovu.

The Blues walishinda Ligi Kuu England msimu uliopita lakini msimu huu mambo yamekuwa kinyume, na wapo nafasi moja tu juu ya eneo la kushushwa daraja kwenye ligi hiyo.

Bodi ya klabu hiyo ilikutana jana kujadili hatma ya Mourinho chini ya mmiliki wa klabu hiyo, Mrusi Roman Abramovich.

Mourinho-Lampard-City-513573

Mreno huyo mwenye umri wa miaka 52 amekuwa Chelsea kwa kipindi cha pili, kilichoanza Juni 2013.

Chelsea walimaliza ligi wakiwa kileleni msimu uliopita na kutwaa taji pamoja na Kombe la Ligi lakini mwaka huu wameanza vibaya, wakishindwa mechi tisa kati ya 16 mpaka sasa.

Mechi ya mwisho kwa Mourinho ilikuwa Jumatatu walipochapwa na viongozi wa ligi hiyo, Leicester City 2-1.

Pep Guardiola, Guus Hiddink, Brendan Rodgers na Juande Ramos na miongoni mwa wanaopigiwa upatu kumrithi Jose.GPL(P.T)

KAMUSOKO AIPANDISHA YANGA KILELENI VPL

Published in Michezo

Kiungo wa Yanga Thabani Kamusoko

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Thabani Kamusoko

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Thabani Kamusoko ndiye aliyeibuka shujaa mkoani Tanga baada ya kuisadia timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya African Sports ‘wanakimanu-manu’ wa jijini Tanga kwenye mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani.

Iliwalazimu Yanga kupata bao dakika ya mwisho (90+5) kutokana na ugumu wa mchezo huo ambapo kwa muda wote Africans Sports walikuwa wamewabana Yanga vilivyo huku kila mtu akiamni mchezo huo utamalizika kwa sare ya bila kufungana.

Mzimbabwe Thabani Kamusoko aliipatia Yanga bao safi akiunganisha kwa style ya ‘bicycle kick’ pasi ya kichwa iliyopigwa na mshambuliaji Donald Ngoma na kuipa Yanga pointi tatu muhimu.

Yanga ambayo ilibanwa mbavu na Mgambo JKT kwenye mchezo wa Jumamosi, imefanikiwa kukusanya pointi nne kwenye mkoa wa Tanga baada ya kucheza mechi mbili. Mchezo wa kwanza Yanga ililazimishwa sare ya bila kufungana na Mgambo ikajikuta ikiambulia pointi moja lakini jana imepata pointi tatu dhidi ya African Sports.

Matokeo hayo yanaifanya klabu hiyo ya Jangwani kufikisha ponti 27 baada ya kucheza michezo 11 na kukaa kileleni mwa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ikiiacha Azam ikiwa nafasi ya pili kwa ponti zake 26 ikiwa imecheza michezo 10.

Shaffihdauda.com(P.T)

CHELSEA CHALI, LEICESTER JUU, YAREJEA KILELENI!

Published in Michezo

LIGI KUU ENGLAND

Matokeo:

Jumatatu Desemba 14

Leicester 2 Chelsea 1

+++++++++++++++++++++++

Leicester City wamerejea kileleni mwa Ligi Kuu England baada ya kuichapa Chelsea 2-1 kwenye Mechi iliyochezwa Walkers Stadium.

Jamie Vardy aliipa Leicester Bao la kuongoza katika Dakika ya 33 alipounganisha Krosi ya Riyad Mahrez na hilo ni Bao lake la 15 kwa Msimu huu.

Leicester waliongoza 2-0 katika Dakika ya 48 kwa Bao la Riyad Mahrez alieufunga baada kuinasa Krosi ya Albrighton.

Chelsea walipata Bao lao moja Mfungaji akiwa Loic Rémy Dakika ya 77 kufuatia Krosi safi ya Pedro.

Kipigo hiki cha 9 kwa Mabingwa Watetezi Chelsea ambacho kimewaacha wakiwa Nafasi ya 16 wakiwa Pointi 20 nyuma ya Vinara Leicester.(VICTOR)

Read more...

JOSE MOURINHO: ‘WACHEZAJI ‘WANASALITI’ KAZI YANGU!’

Published in Michezo

MENEJA wa Chelsea Jose Mourinho amesema anahisi ‘kazi yake inasalitiwa’ mara baada ya Jana Usiku kuchapwa Bao 2-1 na Leicester City kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.Kipigo hicho kwa Chelsea ambao ni Mabingwa Watetezi ni cha 9 kwao katika Mechi 16 na kimeipa mwanya Leicester City kuongoza Ligi wakiwa Pointi 20 mbele ya Chelsea ambao wako Nafasi ya 16 wakiwa Pointi 1 tu juu ya zile Timu 3 za mkiani ambazo zipo eneo hatari la kuporomoka Daraja.

Akiongea mara baada ya kipigo hicho, Mourinho alisema: “Moja ya sifa zangu bora ni kuusoma Mchezo kwa ajili ya Wachezaji wangu na sasa nahisi kazi yangu inasalitiwa. Moja ya uwezekano ni kuwa Msimu uliopita nilifinya kazi nzuri sana na kuwafikisha Wachezaji eneo la juu ambalo si lao na hawawezi kulidumisha.”

Msimu uliopita ambao Chelsea walitwaa Ubingwa walifungwa Mechi 3 tu za Ligi na kutwaa Ubingwa wakiwa Pointi 8 mbele ya Manchester City.

Jumamosi ijayo Chelsea watakutana na Sunderland ambao wako Nafasi ya Pili toka mkiani.(VICTOR)

Read more...

EUROPA LIGI: MAN UNITED WAPANGWA NA KLABU YA DENMARK MIDTJYLLAND

Published in Michezo

LEO huko Nyon, Uswisi, UEFA EUROPA LIGI imefanyika Droo ya kupanga Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 kwa kujumuisha Timu 24 zilizofuzu kutoka Makundi ya Mashindano haya na Timu 8 zilizomaliza Nafasi za 3 kwenye Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.Kwenye Droo hiyo Manchester United, baada ya kutolewa hatua za Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, imepangwa kucheza na Klabu ya Denmark Midtjylland.

Tottenham, ambao walishiriki Mashindano haya kutoka hatua ya Makundi, wamepangiwa Klabu ya Serie A Fiorentina wakati Liverpool, ambao pia walikuwemo Makundi ya EUROPA LIGI, watacheza na Klabu ya Germany Augsburg.

Valencia ya Spain, ambayo ipo chini ya Mchezaji wa zamani wa Man United Gary Neville, watacheza na Rapid Vienna ya Austria wakati mtanange mkali wa Raundi hii ni ule wa Borussia Dortmund na FC Porto.(VICTOR)

Read more...

DROO ya Raundi ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, imefanyika Leo huko Nyon, Uswisi ni kuzibua mitanange mikali.Mabingwa Watetezi Barcelona watavaana na Arsenal wakati Paris Saint-Germain wakikutana na Chelsea hukuJuventus wakicheza na Bayern Munich.

Mechi nyingine za mvuto ni ile ya AS Roma na Real Madrid huku Dynamo Kyiv wakikutana na Manchester City.

Raundi hii itachezwa Februari 16-17 na 23-24 huku Marudiano ni Machi 8-9 na 15-16.

Washindi watasonga Robo Fainali.(VICTOR)

Read more...

LEO huko Nyon, Uswisi, UEFA EUROPA LIGI inafanya Droo ya kupanga Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 kwa kujumuisha Timu 24 zilizofuzu kutoka Makundi ya Mashindano haya na Timu 8 zilizomaliza Nafasi za 3 kwenye Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI mojawapo ikiwa Manchester United.Pamoja na Man United kwenye Droo hiyo zipo pia Liverpool na Tottenham ambao walifuzu kutoka Makundi ya EUROPA LIGI.

Timu 8 zilizotoka UEFA CHAMPIONZ LIGI ni Man United, Bayer Leverkusen, Olympiacos, Porto, Shakhtar Donetsk, Galatasaray, Sevilla na Valencia.

Kwenye Droo, Timu hizo 32 zimegawanywa kwenye Vyungu Viwili vya Timu 12 kila kimoja huku Chungu Namba 1 kikiwa na Timu zilimaliza Washindi wa Makundi yao pamoja na zile ambazo ziko juu kwenye Listi ya Ubora ya UEFA.

Timu iliyo Chungu Namba 1 itapangwa kucheza na Timu iliyo Chungu Namba 2 isipokuwa Timu za Nchi moja hazitakutanishwa na zile zilizokuwa Kundi moja hazitapangwa kukutana.(VICTOR)

Read more...

EURO 2016: DROO YA FAINALI KUFANYIKA LEO

Published in Michezo

DROO ya kupanga Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, itafanyika Jumamosi Desemba 12 huko Paris Nchini France ambako Fainali hizo zitafanyika.

Droo hiyo itakuwa na Timu 24 ambazo zimegawanywa katika Vyungu Vinne vyenye Timu 6 kila kimoja kulingana na Nafasi zao za kwenye Listi ya Ubora.

Fainali za EURO 2016 zitachezwa Mwakani kuanzia Juni 10 hadi Julai 10 huko France.(VICTOR)

Read more...

Platini apoteza rufaa ya kupinga marufuku

Published in Michezo

Platini

Rais wa Shirikisho la Soka Ulaya Uefa Michel Platini ameshindwa katika rufaa yake ya kutaka marufuku ya siku 90 dhidi yake iondolewe.

Alikuwa amewasilisha rufaa akitaka marufuku ya kutojihusisha na soka kwa miezi mitatu iondolewe kumuwezesha kuendelea na kazi lakini hilo limekataliwa na Mahakama ya Mizozo ya Michezo.

Platini, 60, alisimamishwa kazi pamoja na rais wa Fifa Sepp Blatter mwezi Oktoba huku uchunguzi wa madai ya rushwa dhidi yao yakiendelea kuchunguzwa.

Wote wawili wamekanusha tuhuma hizo.(VICTOR)

Karibu Mjengwablog

Uchambuzi wa Soka

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA