We have 475 guests and no members online

ARSENAL, CHELSEA ZASONGA ULAYA!

Published in Michezo

SAFU ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, imekamilika Jana na Timu za England, Arsenal na Chelsea, zilishinda hapo Jana na kutinga Mtoano.

Timu hizo zinaungana na Chelsea iliyofuzu mapema ikiwa na Mechi 2 mkononi.

Juzi Man United ilitolewa UCL na kutupwa UEFA EUROPA LIGI baada ya kumaliza Nafasi ya 3 kwenye Kundi B.

Man United sasa itacheza Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya Kombe hilo.

Droo za kupanga Mechi za Raundi ya Mtoano ya UCL na ile ya EUROPA LIGI itafanyika Desemba 14.

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Hali ilivyo hadi sasa:

Washindi wa Makundi: Real Madrid, Wolfsburg, Atletico Madrid, Manchester City, Barcelona, Bayern Munich, Zenit, Chelsea (VICTOR)

Read more...

FIFA KOMBE LA DUNIA KWA KLABU KUANZA LEO JAPAN

Published in Michezo

20151121154033Logo for Japan 2015 FIFA Club World Cup

KOMBE LA DUNIA kwa Klabu linaanza huko Japan Alhamisi Desemba 10.Washiriki wa Mashindano haya ni Barcelona, Mabingwa wa Ulaya, River Plate, Mabingwa wa Marekani ya Kusini, America ambao ni Mabingwa wa Nchi za Marekani ya Kati na Kaskazini na Visiwa vya Carribean, Mabingwa wa Afrika TP Mazembe, Guangzhou Evergrande, Mabingwa wa Asia na Bingwa wa Kanda ya Oceania.

Pia wapo Sanfrecce Hiroshima, Klabu Bingwa ya Japan, inayoshiriki kama Wenyeji wa Mashindano.

Wakati Barcelona wakiwa ndio wanategemewa kutwaa Kombe hili wakijivunia Kikosi chenye Masupasta Lionel Messi wa Argentina, Nahodha wa Brazil Neymar na Straika wa Uruguay Luis Suarez, Tanzania itaikodolea macho TP Mazembe yenye Mastraika Wawili mahiri kutoka Nchi hiyo, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.(VICTOR)

Read more...

Matokeo Ligi ya Mabingwa Ulaya

Published in Michezo

man utd

Wachezaji wa Manchester United baada ya kipigo cha 3-2 kutoka kwa Wolfsburg na kuyaaga mashindano hayo.

Kundi A

Paris Saint Germain 2 – 0 Shakhtar Donetsk
Real Madrid 8 – 0 Malmoe FF

Kundi B

PSV Eindhoven 2 – 1 CSKA Moscow
Wolfsburg 3 – 2 Manchester United

Kundi C

Benfica 1 – 2 Atletico Madrid
Galatasaray 1 – 1 FC Astana

Kundi D

Manchester City 4 – 2 Borussia Moenchengladbach
Sevilla 1 – 0 Juventus (P.T)

HUKO England, Wachambuzi na Mashabiki, wamepigwa na butaa kuiona Leicester City wapo kileleni mwa Ligi Kuu England baada ya Mechi 15.

Msimu huu, Leicester City, chini ya Kocha Claudio Ranieri, wameshinda Mechi 9, Sare 5 na kufungwa moja tu.

Katika Mechi zao zote 25 zilizopita Leicester wamefungwa Mechi 2 tu na hizo ni chache kupita Timu yeyote ya Ligi Kuu England.

Baada ya kutoka Sare 1-1 na Man United Uwanjani King Power na kufuatia kuichapa Swansea City 3-0 Ugenini Majuzi Jumamosi na kutwaa uongozi, sasa kazi ngumu kwa Leicester inaanza Mwezi huu Desemba kwa Mechi 4 mfululizo za Ligi dhidi ya Vigogo wa England.

Wachambuzi wanadai hapo ndio tutajua mbivu au mbichi za Leicester City ambayo imeng’ara mno kwa mchango mkubwa wa Straika wao Jamie Vardy ambae ndie Mfungaji Bora wa Ligi Kuu England kwa sasa akiwa na Mabao 14.

Jumatatu Usiku, Leicester watakuwa wenyeji wa Mabingwa Watetezi Chelsea na kisha watapiga tripu mbili mfululizo kucheza huko Merseyside na Everton na Liverpool ikifuatiwa Mechi ya Nyumbani na Man City.

Mwanzoni mwa Januari watacheza na Bournemouth na kufuatia safari ya huko London kuivaa Tottenham.(VICTOR)

Read more...

FA CUP: LEO DROO YA RAUNDI YA 3, WAKUBWA KUANZA RAUNDI HII!

Published in Michezo

DROO ya Raundi ya 3 ya Kombe kongwe Duniani, FA CUP, ambalo sasa linaitwa Emirates FA Cup kwa sababu za kiudhamini, itafanyika Leo na kuzihusisha Klabu za Ligi Kuu England na Daraja la Championship ambazo huanzia hapa.

Droo ya Leo, ambayo itafanyika huko Sport Wales National Centre Mjini Cardiff, itahusisha Timu 64 na Mechi zake kuchezwa kati ya Ijumaa Januari 8 na Jumatatu Januari 11.

Arsenal ndio Mabingwa Watetezi baada ya kulitwaa Kombe hili kwa mara ya pili mfululizo Mwezi Mei Mwaka huu.(VICTOR)

Read more...

SIR ALEX FERGUSON ni Lejendari aliewika na kuleta mafanikio makubwa katika Historia ya Manchester United lakini sasa matunda ya mafanikio yake yanatapakaa kila sehemu baada ya Wachezaji wake wasiopungua 28 kushika nyadhifa za Umeneja katika Klabu mbalimbali.Mchezaji mwingine wa zamani wa Man United ambae ataongezeka kwenye Listi hii ni Gary Neville ambae Jana alianuliwa rasmi kuwa Kocha Mkuu wa Valencia inayocheza La Liga huko Spain.

PATA LISTI HIYO:

28. Mike Phelan

MENEJA: Norwich

Ndie alikuwa Msaidizi wa mwisho wa Sir Alex Ferguson wakati anastaafu kama Meneja wa Manchester United.

Sasa ni Msaidizi Hull City.

27. Gabriel Heinze

MENEJA: Godoy Cruz

Beki wa zamani wa Argentine na Mwezi Juni alichukua wadhifa wa Klabu ya Nchini kwao na kutimuliwa Mwezi Septemba.(VICTOR)

Read more...

ADEBAYOR ALIPWA £100,000 KILA WIKI BILA KUICHEZEA SPURS

Published in Michezo

Emmanuel Adebayor bado analipwa Pauni Laki 1 kwa Wiki, takriban Shilingi 323, 853,238/=, na Tottenham licha ya kutoichezea tangu Machi 15.

Ikiwa hatajiunga na Klabu yeyote Mwezi Januari wakati Dirisha la Uhamisho litakapofunguliwa, Adebayor ataendelea kulipwa na Spurs Fedha ambazo zitafikia Jumla ya Pauni Milioni 5.25 ifikapo Juni Mwakani wakati Mkataba wake na Spurs utakapokwisha.

Straika huyo alitemwa na Tottenham Mwezi Septemba baada ya Meneja Mauricio Pochettino kutomsajili katika Vikosi vya Timu kwa ajili ya Ligi Kuu England na UEFA Europa Ligi.

Uamuzi huo ulimfanya Adebayor akatae kufanya Mazoezi na Kikosi cha Kwanza cha Spurs na kumshangaza kila Mtu kuamua kufanya Mazoezi na Timu za Vijana za Spurs.(VICTOR)

Read more...

FIFA-LOGO

Belgium imebaki Nambari Wani kwenye FIFA Listi ya Ubora Duniani iliyotolewa Leo huku Tanzania ikipanda Nafasi 3.Mabingwa wa Dunia Germany wameshuka Nafasi 2 na sasa wapo Nafasi ya 4 wakati Argentina wakipinda Nafasi 1 na kushika Nafasi ya Pili na Spain kupanda Nafasi 3 na kukamata Nafasi ya 3.

Brazil nao wapo Nafasi ya 6 baada kupanda Nafasi 2.

Tanzania sasa ipo Nafasi ya 132 baada ya kupanda Nafasi 3 toka Mwezi uliopita.

Kwa Afrika, Timu ya juu kabisa kwenye Listi ya Ubora ni Ivory Coast ambayo ipo Nafasi ya 19 baada ya kupanda Nafasi ikifuatiwa na Algeria ambayo ipo Nafasi ya 28 baada ya kuporomoka Nafasi 2.(VICTOR)

Read more...

LEJENDARI WA MAN UNITED GARY NEVILLE KOCHA MPYA VALENCIA!

Published in Michezo

MCHEZAJI wa zamani wa Manchester United na England Gary Neville ameteuliwa kuwa Kocha Mkuu mpya wa Valencia ya Spain hadi mwishoni mwa Msimu huu.Neville, mwenye Miaka 40, ataendelea kuwa mmoja wa Makocha wa Timu ya Taifa ya England wakati akiendelea na wadhifa huu wake mpya huko Spain.

Uteuzi huu wa Neville umekuja kirahisi kwani Mmiliki wa Valencia, Peter Lim, Raia wa Singapore, pia ana Hisa kwenye Klabu ya huko Manchester, Salford City, ambayo pia Neville ni mmoja wa Wamiliki wake.

Ndugu wa Gary Neville, Phil Neville, aliteuliwa kuwa Kocha Msaidizi wa Valencia tangu Mwezi Julai.

Neville, ambae mara baada ya uteuzi huu wa huko Valencia amejitoa kuwa mmoja wa Wachambuzi wa TV ya Sky Sports, atatambulishwa rasmi Kesho Alhamisi na Rais wa Valencia Layhoon Chan.(VICTOR)

Read more...

KENYA, NIGERIA, SOUTH AFRICA ZAJIUNGA CHAMA CHA LIGI DUNIANI!

Published in Michezo

Kenya, Nigeria na South Africa zimeungana na Ligi nyingine kubwa za Soka la Kulipa kuunda WAL, World Association of Leagues, Chama cha Ligi za Dunia, kufuatia Mkutano uliofanyika huko Paris hapo Jana.Nchi hizo 3 za Afrika zimeungana na Ligi nyingine 18, zikiwemo Ligi kubwa za England, France na Spain, kuunda chombo hicho ambacho kitafanya kazi sambamba na FIFA.

Kwa mujibu wa Rais wa LFP, Ligi ya France, Frederic Thiriez, Chombo hiki kitaanza kazi zake rasmi Mwezi Januari na kitajumuisha zile Ligi ambazo zinaendeshwa huru na si na Vyama vya Soka vya Nchi.

Washiriki wa Mkutano huo wa Paris wamesema umuhimu wa WAL unatokana na ukweli kuwa Ligi ndizo hudhibiti Asilimia 90 ya Soka na wao wanataka kushiriki katika maamuzi yeyote ya Soka yanayofanywa na FIFA na pia kutoa msukumo kuiunda upya FIFA yenyewe ambayo sasa ipo kipindi cha mpito kufuatia skandali kubwa za rushwa.(VICTOR)
Read more...

MBIO ZA KILIMANJARO HEALTH RUN 2015 ZAFANYIKA MKOANI KILIMANJARO

Published in Michezo

Washiriki wa Mbio za Kilimanjaro Health Run KM 10 wakianza mbio hizo katika eneo la nje ya uwanja wa Majengo mjini Moshi. 

Washiriki wa Mbio za Km  5 zilizowashirikisha zaidi watoto wanao lelewa katka ituo mbalimbali mjin Moshi.

Mkurugenzi wa Zara Tanzania na Zara Charity,Zainab Ansel akishiriki mbio hizo pamoja na mdogo wake Rahma wakikimbia mbio za Km 5.

Mshindi wa mbio za KM 10 kwa wanaume ,Lameck Msiwa akimaliza mbio katika uwanja wa Majengo mjini Moshi.(P.T)

Read more...

CAPITAL ONE CUP: LEO NI ROBO FAINALI!

Published in Michezo

ROBO FAINALI za Kombe la Ligi huko England, ambalo hujulikana kama Capital One Cup, zitachezwa Leo na Kesho Jumatano.

Hii Leo zipo Mechi 3 ambazo zinahusisha Timu za Madaraja ya chini kucheza na Timu za Ligi Kuu England.

Middlesbrough, ambao wapo Daraja la Championship, wapo kwao Riverside Stadium kucheza na Everton ya Ligi Kuu England wakati Stoke City wakiwa kwao kuikaribisha Sheffield Wednesday na Vinara wa Ligi Kuu England, Man City, wapo Nyumbani Etihad kucheza na Hull City iliyoshuka kutoka Ligi Kuu England Msimu uliopita.

Kesho ipo Mechi moja wakati Timu za Ligi Kuu England pekee zitakapocheza na ni kati ya Southampton na Liverpool.(VICTOR)

Read more...

Karibu Mjengwablog

Uchambuzi wa Soka

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA