We have 446 guests and no members online

LEICESTER-MANUNITED-MATCH

 

Manchester United wametoka Sare 1-1 huko King Power Stadium walipotoka 1-1 na Leicester City na matokeo haya kuiruhusu Man City kutwaa uongozi wa Ligi Kuu England.Leicester walitangulia kufunga kwa Bao la Jamie Vardy katika Dakika ya 24 na kumfanya avunje Rekodi ya Mchezaji wa zamani wa Man United, Ruud Van Nistelrooy, aliyoiweka Mwaka 2003 ya kufunga katika Mechi 11 mfululizo za Ligi Kuu England.

Man United walisawazisha katika Dakika ya 45 kwa Bao la kichwa la Bastian Schweinsteiger na walistahili kushinda kwenye Kipindi cha Pili kwa jinsi walivyotawala lakini tatizo lao sugu la kutokuwa na Wachezaji wenye kasi na Wafungaji liliwakisha.(VICTOR)

Read more...

KOCHA SUPER D AMNOWA BONDIA IBRAHIMU CLASS KING CLASS MAWE

Published in Michezo

 Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimfanyisha mazoezi ya nguvu  na kujenga misuli bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mpambano wake na Twaha Kassimu utakaofanyika katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro desemba 25 Picha na SUPER DBOXING NEWS

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akifundishwa jinsi ya kupiga ngumi za mkunjo wa chini 'UpCat' wakati wa mazoezi ya bondia huyo kujiandaa na mpambano wake na Twaha Kassimu utakaofanyika Desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri morogoro Picha na SUPER DBOXING NEWS.(P.T)

Read more...

Nani mkali

Published in Michezo

Beki wa zamani wa Simba avamiwa na majambazi

Published in Michezo

DSCN0201-FILEminimizer

Wilbert Molandi na Gladness Mallya-GPL

NAHODHA na beki wa kati wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa, siku kadhaa zilizopita alivamiwa na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi na kujaribu kuiba fedha.
Beki huyo, aliyevamiwa nyumbani kwake Mapambano, Sinza jijini Dar es Salaam, anakumbukwa kwa kuweka rekodi ya kuwatoa Zamalek katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2003.

Simba iliwatoa Zamalek kwa njia ya penalti baada ya mechi ya nyumbani kuwafunga bao 1-0 kabla ya kwenda kurudiana Cairo, Miri na kufungwa bao 1-0 kabla ya kwenda hatua ya penalti na kuwatoa baada ya Juma Kaseja kupangua penalti kisha marehemu Christopher Alex kufunga tuta la ushindi.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Pawasa alisema majambazi hao watatu walimvamia saa 11:30 alfajiri nyumbani kwake na kumtaka atoe fedha alizonazo.
Pawasa alisema, majambazi hao inavyoonekana kama walipewa taarifa za yeye kuwa na fedha nyingi alizopewa akaweke benki na mmoja wa wafanyabiashara wenzake aliyemtaja kwa jina moja (linahifadhiwa) siku moja kabla ya tukio hilo.

“Inavyoonekana kama dili vile limechongwa na watu flani waliokuwa wanajua nina fedha nyingi nilizotoka nazo ofisini na kurudi nazo nyumbani kwa ajili ya kuzihifadhi.
“Kwa sababu hao majambazi walipovamia tu nyumbani kitu cha kwanza kuniambia ni tumefuata fedha zetu, kwa maana ya zile nilizopewa na jamaa yangu ninayefanya naye biashara, kitu ambacho ni cha kweli lakini tayari nilikuwa nimeshazipeleka fedha hizo benki.

“Majambazi hao walikuwa watatu, kati ya hao wawili nilikuwa napambana nao mlangoni wakitaka kuingia ndani.

“Wakati napambana na majambazi hao wawili, mmoja alitoa bunduki na kunipiga na kitako chake na kunipasua usoni, bila kujali nilijaribu kupambana nao hivyohivyo kuhakikisha ninaokoa uhai wangu.

“Baada ya kuona nimewashinda walitoka nje na kukimbilia bodaboda waliyokuja nayo iliyokuwa imeegeshwa nje, mmoja alidondoka, nikafanikiwa kumkamata, muda huo tayari majirani walikuwa wameshasogea baada ya kusikia makelele.

“Tulivyomkamata majirani walimshambulia na baadaye kumpeleka kituo cha polisi kabla ya kupelekwa mahabusu Gereza la Segerea huku wenzake wakitafutwa.
“Baada ya purukushani hizo kumalizika nilienda Hospitali ya Palestina, Sinza kwa ajili ya matibabu, nimeshonwa nyuzi tatu ambazo nimetolewa juzi,” alisema Pawasa.(P.T)

LEICESTER KUITWANGA TENA MAN 5?

Published in Michezo

LEICESTER-MANUNITED

MSIMU uliopita, Manchester United waliongoza 3-1 huko King Power Stadium na kujikuta wakitandikwa 5-3 na Leicester City katika Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Septemba 21, 2014 na Jumamosi Timu hizi zinakutana Uwanja huo huo.

Safari hii, Leicester City, ndio Vinara wa Ligi Kuu England, wakiwa Pointi 1 mbele ya Man United iliyo Nafasi ya Pili.

Mwaka Jana, Straika wa Leicester, Jamie Vardy, alifunga Bao lake la kwanza kwenye Ligi na kutengeneza zote 4 walipoifunga Man United 5-3, na safari hi indie anaongoza kuwa Mfungaji Bora wa Ligi.

Safari hii, Leicester wapo chini ya Kocha Claudio Ranieri ambae mara ya mwisho alifukuzwa akiwa Kocha wa Greece baada ya Nchi hiyo kufungwa na Vibonde wa Ulaya Faroe Islands.(VICTOR)

Read more...

2308960_UltraWide

MAKIPA
Joe Hart (Man City)

Gianluigi Buffon (Juventus)

Manuel Neuer (Bayern)

Denys Bokyo (Dnipro)

MABEKI
David Alaba (Bayern)

Jerome Boateng (Bayern)

Dani Alves (Barcelona)

Javier Mascherano (Barcelona)

Gerard Pique (Barcelona)

Giorgio Chiellini (Juventus)

Leonardo Bonucci (Juventus)

David Luiz (PSG)

Thiago Silva (PSG)

Diego Godin (Atletico Madrid)

Sergio Ramos (Real Madrid)

Ricardo Rodriguez (Wolfsburg)

VIUNGO
James Rodrigues (Real Madrid)

Paul Pogba (Juventus)

Claudio Marchisio(Juventus)

Arturo Vidal(Bayern)

Marco Verratti (PSG)

Hakan Calhanoglu (Bayer Leverkusen)

Andres Iniesta (Barcelona)

Kevin De Bruyne (Man City)

Ivan Rakitic (Barcelona)

Eden Hazard (Chelsea)

Grzegorz Krychowiak (Sevilla)

Yevhen Konoplyanka (Sevilla)

WASHAMBULIAJI
Sergio Aguero (Man City)

Alexis Sanchez (Arsenal)

Gareth Bale (Real Madrid)

Cristiano Ronaldo (Real Madrid)

Thomas Muller (Bayern)

Robert Lewandowski (Bayern Munich)

Lionel Messi (Barcelona)

Luis Suarez (Barcelona)

Neymar (Barcelona)

Zlatan Ibrahimovic (PSG)

Antoine Griezmann (Atletico Madrid)

Alvaro Morata (Juventus)

Majina ya wachezaji hayo yamejuisha vilabu 13 kutoka kwenye ligi 6 tofauti na wachezaji 12 kati ya hao 40 wamewahi kuwepo katika kikosi hicho cha mwaka kwa miaka iliyopita.

Upigaji wa kura unafanyika katika mtandao wa Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA na kura zinatarajiwa kupigwa hadi Januari, 5 mwaka 2016 na kikosi kutangazwa Januari 8.

KLABU BINGWA ULAYA: Matokeo

Published in Michezo

blj

Ligi ya Mabingwa barani Ulaya imeendelea hapo jana Jumanne kwa michezo 8 katika viwanja tofauti tofauti na haya ndiyo matokeo ya michezo hiyo

Ratiba ya michezo ya leo jumanne Novemba 24 katika ligi ya mabingwa Ulaya UEFA

GROUP: E

BATE Borisov 1 – 1 Bayer Leverkusen

Barcelona 6 – 1 Roma

GROUP: F

Arsenal 3 – 0 Dinamo Zagreb

Bayern Munich 4 – 0 Olympiakos

GROUP: G

Porto 0 – 2 Dynamo Kyiv

Maccabi Tel Aviv 0 – 4 Chelsea

GROUP: H

Zenit St. Petersburg 2 – 0 Valencia

Lyon 1 – 2 Gent

Ratiba ya michezo ya leo Jumatano katika ligi ya mabingwa Ulaya UEFA

GROUP: A

Shakhtar Donetsk – Real Madrid 22:45 EAT

Malmo – Paris Saint German 22:45 EAT

GROUP: B

Manchester United – PSV 22:45 EAT

CSKA Moscow – Wolfsburg 20:00 EAT

GROUP: C

Astana – Benfica 18:00 EAT

Atletico Madrid – Galatasaray 22:45 EAT

GROUP: D

Juventus – Manchester City 22:45 EAT

Borussia Moenchegladbach – Sevilla 22:45 EAT

Kwa wazazi tufahamu watoto wetu tunawatia moyo sana tunapochukua muda kuona wanayofanya hata kwenye michezo..
Maggid,
Iringa.(P.T)

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI KUDHAMINI MICHUANO YA GOFU YA WAITARA

Published in Michezo

1b_4c0df.JPG

Katibu wa klabu ya Gofu ya Lugalo Kanali Mstaafu John Nyalusi akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam juu ya mashindano ya siku moja ya gofu ya kumuenzi Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara yatakayofanyika katika klabu ya Gofu ya Lugalo jumamosi hii. Kulia ni Meneja chapa (vileo vikali) wa Serengeti Breweries Limited, Shomari Shija ambao wanahusika na udhamini wa utoaji tuzo, vinywaji na burudani katika kipindi chote cha mashindano.

1c_34fcc.JPG

Meneja chapa (vileo kali) wa Serengeti Breweries Limited, Shomari Shija, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam kuhusiana na mashindano ya siku moja ya gofu ya kumuenzi Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara yatakayofanyika katika klabu ya Gofu ya Lugalo jumamosi. Kushoto ni katibu wa klabu ya Gofu ya Lugalo Kanali Mstaafu John Nyalusi. Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake kikali cha Johnnie Walker kitadhamini mashindano na kutoa zawadi mbalimbali kwa washindi wa mchuano huo.

31_e76fc.JPG

Mabalozi wa pombe kali ya Scotch Whisky “Johnnie Walker” wakionyesha aina mbalimbali za chapa za pombe hiyo wakati wa mkutano na waandishi wa habari juu ya mashindano ya gofu ya waitara ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi siku ya jumamosi katika viwanja vya Lugalo jijini Dar es salaam. Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia pombe hiyo kali ndio wadhamini wa mashindano hayo ambapo pia watahusika na utoaji tuzo, vinywaji na burudani katika kipindi chote cha mashindano.

18th Novemba 2015, Dar es salaam: Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia pombe yake kali ya Johnnie Walker imetangaza rasmi udhamini wa mashindano ya gofu ya Waitara ambayo yanatarajiwa kuanza siku ya jumamosi katika viwanja vya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.(VICTOR)

Read more...

Matokeo Ya Ajabu; Algeria Vs Germany 1982, Na Algeria Vs Tanzania 2015!

Published in Michezo

Ndugu zangu,

Nimeshuhudia mechi ya usiku wa jana tulipokuwa tukiangamizwa na Algeria. Mpaka naamua kuinuka kitini tulikuwa tumeshapigwa saba bila. Ukweli tulizidiwa, na kuna wakati nilimuuliza aliyekaa karibu yangu kama Mbwana Samatta yumo uwanjani au Kocha Mkwassa ameshamuweka benchi. Hapana, nilijibiwa kuwa yumo uwanjani!

Naam, hata nyota wetu Mbwana Samatta jana alikuwa wa kumtafuta kwa kuvaa miwani ya macho. Hakuonekana.

Nilichokiona kikubwa; Tanzania tunahitaji kuruhusu uraia pacha ili nasi tuweze kuwaleta vijana wetu wa Kitanzania wanaocheza ughaibuni na waliochukua uraia wa nchi hizo. Maana, kwa soka ya sasa, ni vigumu kwenda Kombe la Dunia kwa kuwa kikosini na akina Samatta wawili na waliobaki ni wa kutoka Ligi ya nyumbani.

Na hakika matokeo ya leo yalikuwa ni ya ajabu pia. Sikufikiri kwa soka ile tuliyocheza Dar tungekwenda Algeria kucheza ' mediocre football' na kutoka na matokeo yale. Nilitarajia tufanye miujiza, maana soka inayo ya kwake. Na Algeria wenzetu wamewahi kufanya miujiza dhidi ya taifa kubwa kisoka la Ujerumani.

Ndio, itakumbukwa Algeria iliwahi kufanya miujiza katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka 1982. Ni pale ilipowafunga Ujerumani kwa mabao 2-1 kwenye mechi ya ufunguzi katika kundi lao. Walikuwa wachezaji nyota wa Algeria kama vile Assad na Madjer walionyesha kandanda safi na la kuvutia.

Katika pambano hilo kipa wa Ujerumani Schumacher alitoka uwanjani akiwa ameinamisha kichwa. Maana alitamka kabla ya mechi, kuwa kama Algeria watawafunga Wajerumani, basi atafanya operesheni ya kubadili sura yake!

Pamoja na Algeria kuwafunga Wajerumani, njama zilifanyika kwa Ujerumani na Austria katika kundi lao. Kwa namna moja au nyingine matokeo yalipangwa ili Algeria isipate nafasi ya kusonga mbele. Ujerumani iliibuka mshindi kwa bao 1-0 matokeo ambayo yalizifanya Ujerumani na Austria kusonga mbele kwa pamoja kutoka kwenye kundi lao.

Jambo hilo lilidhihirishwa mara tu baada ya Ujerumani kupachika bao lao. Mpira ukaonekana 'kufa'. Wachezaji wa timu zote mbili walionekana kucheza wakisubiri kipenga cha mwamuzi cha kumaliza mchezo. Hakika hii yaweza kabisa kusemwa ni moja ya kashfa zilizopata kutokea katika historia ya fainali za Kombe la Dunia.

Kikabaki kimya hata baada ya matokeo hayo ya kushangaza. Hayakuandikwa mengi kwenye kurasa za michezo za magazetini. Kwenye moja ya magazeti ya Austria walitenga ukurasa mzima bila kuandika habari za mechi hiyo. Walichofanya ni kuandika orodha ya wachezaji waliocheza pambano hilo kwa pande zote mbili.

Kwa mchezo ule uliokuwa na matokeo ya ajabu na kutatanisha baina ya Ujerumani na Austria , Chama Cha Soka cha Algeria kiliitaka FIFA izitoe Ujerumani na Austria katika ushiriki wao wa mashindano hayo. Jambo hilo halikufanyika.

Maggid,(P.T)

STARS YAWASILI SALAMA ALGERIA

Published in Michezo

Mbwana Samatta (kushoto) pamoja na Thomas Ulimwengu (kulia)

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kimewasili salama nchini Algeria leo jioni majira yaa 10 jioni, kabla ya kuanza safari ya kuelekea katika mji wa Bilda.

Msafara wa Taifa Stars unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Athumani Kambi, ambapo jumla ya watu 40 wapo katika mji wa Bilda wakiwemo wachezaji 21 wanaojiandaa kwa mchezo wa marudiano.

Mara baada ya kufika katika uwanja wa ndege Algiers, Stars ilipokelewa na watanzania na wanafunzi wanaoshi nchini Algeria, na kuongozana na timu mpaka katika mji wa Bilda ilipofiki timu.

Stars inatarajiwa kufanya mazoezi kesho saa 1 jioni katika uwanja wa Mustapha Tchaker utakaotumika kwa mchezo wa marudiano siku ya Jumanne.

Katika mchezo wa awali uliochezwa jana jioni jijini Dar es salaam, Tanzania ilitoka sare ya mabao 2 – 2 dhidi ya Algeria, hivyo kuifanya Stars kusaka ushindi katika mchezo wa marudiano ili kuweza kusonga mbele.

Kocha wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema vjana wake wote wapo katik ahali, hakuna majeruhi na wapo tayari kwa ajili ya kusaka ushindi siku ya Jumanne, na kusema makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa jana wanayafanyia kazi yasijitokeze tena katika mchezo unaofuata.

Taifa Stars imefikia katika hoteli ya Ville Des Roses imetumia takriabn muda wa saa 1 kutoka katika uwanja wa Ndege wa Algiers mpaka katika hoteli hiyo iliyopo eneo la Bilda.

Namba ya simu ya Afisa Habari wa TFF aliyeambatana na timu nchini Algeria +213 558 465069 (P.T)

STARS YATOKA SARE YA BAO 2-2 NA ALGERIA LEO TAIFA

Published in Michezo

Maguli 1

Wachezaji wa Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ wakishangilia moja ya bao.

Maguli 4

Mashabiki wakishangilia.

Mbwana Samatta akishangilia goli lake alilofunga dhidi ya Algeria

Mbwana Samatta akishangilia goli lake alilofunga dhidi ya Algeria.

Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeeshindwa kuchomoza  na ushindi baada ya kulazimishwa sare ya kufungana magoli 2-2 dhidi ya timu ya taifa ya Algeria kwenye mchezo wa kwanza wa kuwania nafasi ya kupangwa kwenye makundi kwa ajili ya kuwania kufuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia itakayofanyika mwaka 2018 nchini Urusi leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Elius Maguli alianza kuifungia Stars bao la kuongoza dakika ya 43 kipindi cha kwanza akiunganisha kwa kichwa krosi ya mlinzi wa kushoto Hajji Mwinyi. Goli hilo likaipeleka Stars mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.

Algeria walisawazisha goli dakika chache baada ya kipindi cha pili kuanza mfungaji akiwa ni Slimani Islam bao ambalo limefungwa kutokana na uzembe wa walinzi wa Stars.

Dakika za mwanzo za kipindi cha pili Stara ilicheza mpira wa kasi na kufanikiwa kupata goli la pili dakika ya 54 lililofungwa na Mbwana Samatta baada ya kuichambua safu ya ulinzi ya Algeria kisha kufunga goli kwa ustadi wa hali ya juu.

Muda mfupi baada ya Stars kupata goli la pili kocha alifanya mabadiliko kwa kumpumzisha Elius Maguli na nafasi yake kuchukuliwa na Mrisho Ngassa wakati Said Ndemla aliingia kuchukua nafasi ya Muthir Yahya.

Dakika ya 71 kipindi cha pili, Slimani Islam alifunga goli la kwanza kabla ya kuisawazishia Aligeria dakika ya 74 goli lililotokana na kutoelewana kwa safu ya ulinzi ya Stars na kutoa mwanya kwa Slimani kuisawazishia timu yake.

Kikosi cha Stars: Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Haji Mwinyi, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Himid Mao, Thomas Ulimwengu, Mudathir Yahya, Mbwana Samatta, Elius Maguli na Farid Musa.

Walioanzia kwenye benchi: Ailishi Manula (GK) Salim Mbonde, Mohamed Hussein, Simon Msuva, John Bocco, Mrisho Ngassa na Malimi Busungu.GPL(P.T)

Karibu Mjengwablog

Uchambuzi wa Soka

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA