We have 236 guests and no members online

MCHEZAJI WA ZAMANI WA TAIFA STARS APONGEZA TAMASHA LA PASAKA

IMG_2026

Na Mwandishi Wetu

ALIYEKUWA beki wa kushoto wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Alphonce Modest amelipongeza Tamasha la Pasaka linaloandaliwa na Kampuni ya saa Promotions kwa sababu linawakumbuka wenye uhitaji maalum.

Akizungumza jana, Modest alisema Msama kupitia Tamasha la Pasaka anatenda kazi ya Mungu kwa sababu alikua na uwezo wa kuendelea na shughuli zake nyingine lakini anamkumbuka Mungu kwa kukusanya makundi ya waumini ambao wanamtaja Mungu kwa pamoja.

Modest alitumia fursa hiyo kwa wakazi wa mikoa ya Kanda ya ziwa linakofanyika Tamasha la Pasaka mwaka huu kujitokeza kwa wingi kwa lengo la kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa pamoja.

“Unajua wanapokusanyika idadi kubwa ya watu, tambua na Mungu pia yupo, hivyo Msama mara nyingi anatenda kazi ya Mungu, hivyo na wengine tumuunge mkono katika hilo,” alisema Modest na kuongeza.

“Nampongeza sana Msama kwa utekelezaji wake wa Tamasha la Pasaka, kwani ni wachache wenye moyo kama wake, kwani alikua na uwezo wa kuendelea kula bata kwa kidogo alichonacho, lakini muono wake ni kuwa karibu na Mungu mara kwa mara,” alisema Modest.

Naye Msama alitumia fursa hiyo kueleza kwamba tamasha la mwaka huu linatarajia kuanza Machi 26 mkoani Geita, Machi 27 jijini Mwanza na kumalizia Kahama Machi 28.

Msama alisema waimbaji mbalimbali wanatarajia kupanda jukwaani kwa lengo la kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii.(P.T)

Tuma Maoni


Security code


Anzisha upya


Karibu Mjengwablog

Uchambuzi wa Soka

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA