We have 437 guests and no members online

Yahya Jammeh aondoka Gambia, nakuacha hazina tupu

Yahya Jammeh aondoka Gambia, nakuacha hazina tupuMshauri maalumu wa Rais wa Gambia Adama Barrow amesema zaidi ya dola za Kimarekani milioni 11 zinaaminika kutoweka katika hazina ya serikali, kufuatia kuondoka madarakani kwa mtawala wa muda mrefu Yahya Jammeh.

Mia Ahmad Fatty amewaambia Waandishi wa habari katika mji mkuu wa Senegal Dakar kwamba wataalamu wa masuala ya fedha wanatathmini kujua ni kiasi gani kwa sasa kimepotea.

Amesema Gambia kwa sasa ina tatizo kubwa kifedha kwa hazina yake kutokuwa na kitu.

Kwa sasa Rais Barrow amekuwa akifanya kazi na timu ya wataalamu wa masuala ya fedha na wengine kutoka Benki kuu ya nchi hiyo kupata kiasi halisi kilichopo.

Habari zinasema magari ya kifahari na mali nyingine zilionekana zikipakiwa katika ndege ya mizigo ya Chad kwa niaba ya Rais Jammeh siku alipoondoka nchini humo.

Maelfu ya watu walikusanyika katika Ikulu ya nchi hiyo jana jioni wakiyaangalia majeshi ya Senegal yakiingia kwa ajili ya kuweka usalama kabla ya kurejea nchini kwa Adama Barrow.

Adama Barrow akiwa Dakar, Senegal Januari 20, 2017

Adama Barrow, (katikati), amesema anapanga kuchunguza tuhuma za ukiukaji wa haki za kibinadamu zilizotekelezwa wakati wa utawala wa Jammeh

Rais Barrow yupo nchini Senegal na bado haijulikani ni lini hasa atarudi Gambia na kuingia ofisini.

Alisema atarejea tu baada ya kuhakikishiwa usalama wake.

Wanajeshi wa Senegal wakishika doria karibu na ikulu ya rais mjini Banjul Jumapili

Wanajeshi wa Senegal wakishika doria karibu na ikulu ya rais mjini Banjul Jumapili.  BBC

UOK

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa Jamhuri ya Watu wa China zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea hundi ya shilingi milioni 70 kutoka kwa  Balozi wa China nchini Mhe. Dk. Lu Youqing iliyotolewa na Taasisi pamoja na Jumuiya ya Wachina wanaoishi Tanzania kuchangia shule ya msingi ya Chato iliyopo mkoani Geita wakati wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa kichina zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni wengine waalikwa pamoja na wasanii waliotumbuiza wakati wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa kichina zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam.

Sehemuya watu waliohudhuria sherehe za mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa China nchini Mhe. Dk. Lu Youqing wakati wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Tanzania itaendelea kudumisha,kuimarisha na  kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na China kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande hizo MBILI.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam katika sherehe ya maadhimisho ya mwaka mpya wa Kichina hapa nchini sherehe ambazo zimehudhuriwa na mamia ya raia wa China na Tanzania.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa China imekuwa mshirika na mdau mkubwa wa maendeleo hapa nchini na hali hiyo inatokana na mahusiano mema na mazuri yaliyopo kati ya nchi hizi Mbili.

Makamu wa Rais amemhakikishia Balozi wa China hapa nchini Dkt Lu Youqing kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli itakuwa bega kwa bega na serikali ya China hasa katika uimarishaji wa sekta za biashara, utamaduni, elimu, afya  na masuala ya kijeshi kwa ajili ya maslahi na ustawi wa wananchi wa Tanzania na China.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa Tanzania itaendelea kujifunza mambo mengi kutoka China ili kuharakisha shughuli za maendeleo za wananchi kutokana na Taifa la China kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo.

Amehimiza ubadilishanaji wa wataalamu kati ya Tanzania na China katika sekta mbalimbali kama hatua ya kuongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi nchini.

Kwa Upande wake, Balozi wa China hapa nchini Dkt Lu Youqing amepongeza hatua zinachukuliwa na serikali ya Tanzania katika kupambana na rushwa na ufisadi.

Dkt  Lu Youqing amesema serikali ya China na raia wake wanafurahishwa na hatua hizo kwa sababu zinalenga kuondoa na kukomesha rushwa na ufisadi kwani tabia hizo zikiachwa ziendelee zinachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha utoaji wa huduma bora na za msingi kwa wananchi.

Akizungumzia mwaka mpya wa Kichina hapa nchini Balozi huyo amesema maadhimisho hayo ni muhimu kwa sababu raia Wachina na Tanzania wanajumuika pamoja katika kubadilisha mawazo na kutakiana heri na mafanikio kwa mwaka 2017.

Balozi huyo wa Tanzania hapa nchini Dkt  Lu Youqing pia amewashukuru wananchi wa Tanzania kwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Mnazi Moja katika kusheherekea sikukuu ya Mwaka mpya wa Kichina sherehe ambazo inapambwa na michezo mbalimbali ikiwemo sarakasi na vikundi vya ngoma asili kutoka China na maonyesho.

Katika Maadhimisho hayo, Balozi wa China nchini Tanzania Dkt  Lu Youqing amemkabidhi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mfano wa hundi ya shilingi milioni 70 fedha ambazo zitatumika katika ujenzi kwenye shule ya msingi Chato iliyopo mkoani Geita.(P.T)

ZIARA YA MAJALIWA MKOANI NJOMBE

Published in Jamii

NJO

Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Iwawa wilayani  Makete wakimwimbia Waziri mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipokwenda shuleni hapo kufungua madarasa   yao Januari 21, 2017.

OG

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Iwawa iliyopo Makete kabla ya kufungua madarasa  ya shule hiyo Januari 20,1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

OG 5

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Iwawa ya Makete,  Novatus Msivala  kwenda kufungua madarasa  ya shule hiyo Januari 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

OG 3

Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa  akifungua madarasa  ya shule ya Sekondari ya Iwawa  iliyopo Makete Januari 21, 2017.. (Picha na Ofisiya Waziri Mkuu)

NJO 1

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka wakiwa wameketi kwenye madawati ya moja kati ya madarasa mawili mapya yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu katika shule ya sekondari ya Iwawa iliyopo Makete Januari 21, 2017.  Katikati ni Mbunge wa Makete, Norman Sigala., (Picha na Ofisi ya  Waziri Mkuu)

OG 2

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole  Sendeka (kulia kwake ) na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Njombe, Deo Sanga kukagua maeneo ya shule ya sekondari ya Iwawa wilayani Makete  baada ya kufungua madarasa ya shule hiyo Januari 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

OG 1

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na walimu wa shule ya sekondari ya Iwawa iliyopo Makete baada ya kufungua madarasa  ya shule hiyo Januari 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

OG

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa  Njombe wakati alipokagua ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Njombe katika eneo la Wikichi katika  Wilaya  ya Njombe Januari 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

NJO

 Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Iwawa wilayani  Makete wakimwimbia Waziri mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipokwenda shuleni hapo kufungua madarasa   yao Januari 21, 2017. (Picha na ofisi  ya Waziri Mkuu

NJO 1

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka wakiwa wameketi kwenye madawati ya moja kati ya madarasa mawili mapya yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu katika shule ya sekondari ya Iwawa iliyopo Makete Januari 21, 2017.  Katikati ni Mbunge wa Makete, Norman Sigala., (Picha na Ofisi ya  Waziri Mkuu)(P.T)

media

Rais wa Rwanda, Paul Kagame aelezea mafanikio yaliyofikiwa na nchi yake katika sekta ya Intaneti kupitia ushirikiano wa sekta binafsi kama mshirika katika uvumbuzi na sera ya uwekezaji ya maendeleo ya kidijitali nchini Rwanda.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) limeitaja Rwanda kama moja ya mifano ya mafanikio ya maendeleo katika Intaneti barani Afrika. Rwanda kwa sasa ni moja ya nchi zinazoongoza katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) barani Afrika.

Katika Kongamano la Kiuchumi Duniani lililofanyika mjini Davos, nchini Uswisi, kuanzia Januari 17 hadi 20, 2017, Irina Bokova, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu Sayansi na Utamaduni (Unesco) aliitaja Rwanda kama moja ya mifano ya mafanikio katika maendeleo ya intaneti duniani, kwa mujibu wa RFI na Shirika la Habari la Ecofin. Kiongozi huyo alitolea wito nchi nyingi ambazo bado zina kiwango cha chini kwa matumizi ya Intaneti kuiga mfano wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki kwa kuungana na kuboresha mazingira ya maisha ya watu bilioni 3.9 ambao bado hawafajafikia hatua hii.

Irina Bokova alikuwa akiongea katika kikao maalum cha Tume kuhusu masafa marefu kwa ajili ya Maendeleo Endelevu, kiliyoandaliwa na Muungano wa Kimataifa kwa ajili ya Mawasiliano, kikao ambacho kilifanyika tarehe 17 Januari 2017. Katika kikao hicho, Rais wa Rwanda Paul Kagame, mmoja wa viongozi wa Tume hiyo, alielezea mafanikio yaliyofikiwa na nchi yake katika sekta ya Intaneti kupitia ushirikiano wa sekta binafsi kama mshirika katika uvumbuzi na sera ya uwekezaji ya maendeleo ya kidijitali nchini Rwanda. Kampuni ya Korea Telecom Networks Rwanda (KTRN), inayotoa huduma ya Intaneti kwa kiwango kikubwa na kwa bei nafuu, na ambayo kwa sasa imeanza kusambaza mitambo yake nchi nzima, imechangia pakubwa katika sekta hiyo.

Katika kata kunakofanyika shughuli za biashara mjini Kigali.

"Ushirikiano wa sekta ya umma na ile ya kibinafsi ni muhimu kwa maendeleo ya teknolojia ya kidijitali, kwa kuzingatia kwamba kutoa huduma ya Intaneti katika maeneo ambapo haipo, inaleta maendeleo makubwa. Kutoa huduma ya Intaneti kwa idadi hii kubwa [ya watu] inachangia mapato. Kama washirika, tuna nafasi ya kutafakari kazi inayovutia bila kujali gharama kubwa ambayo ingeweza kuzorotesha upatikanaji wa huduma hiyo, "alisema Rais Kagame. Alibaini kwamba Rwanda imefikia 30% kwa kutoa huduma ya Intaneti kati ya mwaka 2003 na 2016 kutokana na kushiriki kwa sekta binafsi katika mkakati na mipango ya kitaifa ya maendeleo ya kiteknolojia.

Itafahamika kwamba washirika wakubwa wa KTRN ni Tigo, MTN, Airtel, ISCO, Popconn, ISPA, Tnsp, G-MAX,...

Watumiaji wengi wa Intaneti barani Afrika hutumia simu ya mkononi.

Mwezi Januari mwaka huu Waziri wa Vijana na Teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT), alisema Rwanda inalenga kutoa huduma ya 92% ya mtandao wa masafa marefu wa (4G) wenye kasi kubwa mwaka huu.

Jean Philbert Nsengimana, Waziri wa Vijana na Teknolojia wa Habari na Mawasiliano (ICT), aliwaambia waandishi wa habari kwamba nchi hiyo inataka mtandao wa 4G usambazwe katika maeneo ya vijijini, kinyume na kile kinachofanyika leo mjini Kigali.

"tunataka kila Mnyarwanda apate huduma ya Intaneti yenye kasi na yenye kuaminika kwa shughuli zake za kibiasharana shughuli nyingine zinazohitaji Intaneti," Bw Nsengimana alisema.RFI

Picha ya Maggid Mjengwa

Ndugu zangu,

Utajua tu kuwa wewe ni Mtanzania ukianza mambo kama yafuatayo;

1. Kukumbuka matunda na vyakula ambavyo ulipokuwa nyumbani Bongo hata rafiki zako walikuwa hawajui kama ni mpenzi wa vitu hivyo. Mfano, Mtanzania akiwa ughaibuni ataanza kukumbuka mabungo, ukwaju, ubuyu, mapera, kungu na mengine . Ataanza kuzikumbuka mboga kama mlenda wa maboga na nyanya chungu, kisamvu cha nazi na dagaa wa kuungwa kwa mafuta ya mawese...

Hapo utajua kama wewe Mtanzania pale utakaposikia kuna Mtanzania mwenzako anakuja Ulaya Marekani au Asia. Cha kwanza kumuagizia ni vitu kama hivyo!

Ukiona nawe umeanza kutamani hivyo hapo juu, basi, ustie shaka na Utanzania wako. Wewe Ni Mtanzania Halisi!

Je, vingine ni vipi vinavyokusaidia kujua kuwa wewe ni Mtanzania? 
Mwenyekiti wenu nimechokoza mjadala...!

Maggid.(P.T)

Donald Trump ahadi kuirejeshea Marekani hadhi yake

Published in Jamii

media

Katika hotuba yake, Donald Trump ameahadi, kama katika kampeni yake ya uchaguzi "kuifanya Marekani kuwa ni nchi yenye nguvu zaidi. "

Donald Trump ameapishwa Jana Ijumaa, Januari 20 kama rais 45 wa Marekani katika sherehe iliofanyika katika majengo makuu ya Bunge la Congress, Capitol Hill saa 05:46 saa za Washington (sawa na saa 01:46 jioni saa za Afrika ya Mashariki).

Baada ya kufyatua mizinga 21 hewani, Donald Trump alitoa hotuba yake ya kwanza kama rais. Donald Trump ameahadi kuwapa nafasi kubwa wananchi wa Marekani katika madaraka, akisema kuwa wamewasahau kwa muda mrefu sana. "Siku hii ya leo ni yenu na Marekani ni nchi yenu," amesema Obama.

Akiweka mkono wake wa kushoto juu ya Biblia mbili, huku akiinua mkono wake wa kulia, Donald Trump amekula kiapo mbele ya Rais wa Mahakama Kuu John G. Roberts Jr. Na kuwa rasmi rais wa 45 wa Marekani.

Donald Trump ametoa kanuni mbili ambazo zitaongoza sera yake ya siasa "kununua vifaa vya Marekani, kuajiri Mmarekani."

Katika hotuba yake, Donald Trump amesema anajutia kuona Marekani ilitajirisha nchi za nje kwa gharama za Marekani. "Hayo yameshapita," Trump amesema. "Tangu siku hii ya leo, Marekani itapewa kipaumbele sawa na suala la biashara, viwanda, au uhamiaji", amebaini Bw Trump.

Donald Trump amehadi kuimarisha ushirikiano wa zamani na kujenga ushirikiano mpya. "Ugaidi wa Waislamu wenye msimamo mkali utatokomezwa," Bw Trump Ameonya.

Donald Trump, alimaliza hotuba yake kwa maneno haya: "Tutaifanya Marekani kuwa na nguvu zaidi, tutaifanya Marekani kuwa nchi tajiri zaidi, tutaifanya Marekani kurudi kuwa na sifa zake, tutaifanya Marekani kurudi kuwa na usalama wake. Kuifanya upya Marekani kuwa na nguvu “Make America great again”. Hii ilikuwa kauli mbiu ya kampeni yake.

Kabla ya kuapishwa kwa Donald Trump, Jaji wa Mahakama Kuu Clarence Thomas amemuapisha Mike Pence, mgombea mwenza wa Donald Trump, ambaye amekua rasmi makamu wa rais wa Marekani baada ya kuapishwa kwake.

Jackie Evancho, kijana wa miaka 16, amehitimisha sherehe hizo kwa kuimba wimbo wa taifa la Marekani.

Trump amechukua hatamu kutoka kwa Rais Barack Obama saa mbili usiku Afrika Mashariki. Amekula kiapo muda mfupi kabla ya saa mbili saa za Washington.RFI

SIMBU

Kutoka kulia ni kaimu mkurugenzi wa Multchoice tanzania, Baraka Shelukindo, Waziri wa habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, mh, Nape nnauye, mwanariadha wa Tanzania aliyeshinda medali ya dhahab katika mbio za marathon huko nchini India hivi karibuni, Alphonce Simbu na katibu mkuu wa shirikisho la riadha Tanzania “RT” william Gida Budai, wakati wa hafla ya kumpongeza mwanariadha huyoiliyofanyika jana Dar es salaam

Waziri Nape Nnauye akiwa na mwanriadha wa Tanzania Alphonce Simbu, wakati wa hafla ya kumkaribisha mwanariadha huyo

Mwanaridha Alphonce Simbu akiwa na katibu mkuu wa RT, Wilhelm Gidabuday

Meneja uhusiano wa Multchoice, Johnson Mshana akiongea katika hafla ya kumpongeza mwanariadha Alphonce Simbu

Alphonce Simbu akizungumza katika hafla ya kupongezwa baada ya kupata medali ya dhahabu katika mashindano ya mbio za marathon huko nchini India(P.T)

Read more...

Jammeh asema ataondoka madarakani

Published in Jamii

Jammeh alishindwa kwenye uchaguzi na Adama Barrow

Jammeh alishindwa kwenye uchaguzi na Adama Barrow

Kiongozi wa muda mrefu nchini Gambia Yahya Jammeh, anasema kuwa ataondoka madarakani baada ya kukataa kukubali kushindwa.

Katika tangazo kwenye runinga, Jammeh alisema kuwa hakuna haja ya hata tone moja la damu kumwagika.

Taangazo hilo linakuja saa kadha baada ya mazungumzo kati ya bwana Jammeh na wapatanishi wa Afrika Magharibi. Hata hivyo hakuna taarifa zaidi kuhusu yale yayoafikiwa.

Bwana Jammeh alishindwa kwenye uchaguzi wa mwezi Disemba na mrithi wake Adama Barrow tayari amesha apishwa.

Bwana Barrow amekuwa akiishi katika taifa jirani la Senegal kwa siku kadha.

Wanajeshi kutoka nchi za magharibi mwa Afrika ikiwemo Senegal wametumwa nchini Gambia wakitisha kumtimua bwana Jammeh madarakani.

Uamuzi wa bwana Jammeh kuondoka ulikuja kufuatia mazungumzo na marais wa Guinea na Mauritania.BBC

MUS

Na: Frank Shija – MAELEZO

ELIMU bure yaongeza idadi ya udahili wa wanafunzi wa shule za msingi nchini waongezeka kutoka 1,282,000 mwaka 2015 hadi kufikia 1,896,000 mwaka 2016 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 84.5.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais –Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe alipokuwa anaongea katika kipindi cha tunatekeleza kinachoratibiwa na Idara ya Habari – MAELEZO na kurushwa na Televisheni ya Taifa (TBC1) jana jijini Dar es Salaam.

Mhandisi Mussa Iyombe amesema kuwa dhamira ya Serikali nikuhakikisha inatoa huduma bora za kijamii ikiwemo elimu, afya, miundombinu na maji safi.

“Dhamira ya Serikali ni kutoa huduma bora za afya,elimu,maji na miundombinu ndiyo maana Serikali ya Awamu ya Tano ikaja na Sera ya Elimu bure ili kutoa fursa kwa wananchi wake kupata elimu,”alisema Mhandisi Iyombe.

Aidha Muhandisi Iyombe amebainisha kuwa kazi kubwa ya TAMISEMI ni kuratibu na kusimamia Mikoa, Wilaya na Halmashauri katika utoaji wa huduma bora za maendeleo kwa wananchi.

Aliongeza kuwa ili Serikali iweze kutimiza azma yake ya kuwapatia huduma za maendeleo wananchi wake imeweka mfumo dhatibiti wa ukusanyaji wa mapato katika halmashauri nchini ili kuhakikisha fedha inapatika kiwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

Mhandisi Iyombe amesema kuwa mapato yanayokusanywa na halmashauri nchini ni kwa ajili ya kutoa huduma za kimaendeleo ili wananchi wanufaike.(P.T)

DERO

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mabewani mjini Makete, januari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)(P.T)

Karibu Mjengwablog

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

Smartads