We have 446 guests and no members online

Na Magreth Kinabo- MAELEZO

Serikali imepiga marufuku tabia ya baadhi ya hospitali au taasisi binafsi za afya kuwapima wagonjwa wanaotoka hospitali za Serikali vipimo ambavyo hawakuagizwa kuvipima na madaktari kutoka hospitali hizo kwani kufanya hivyo ni kuiongezea Serikali gharama zisizo la lazima.

Tamko hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangala wakati alipofanya ziara ya kutembelea leo kwenye Taasisi ya Saratani ya Ocean Road iliyopo jijini Dares Salaam.

Waziri Kingwangala alitoa agizo hilo baada ya kukutana na mgonjwa ambaye alitakiwa kufanya kipimo cha MRI katika hospitali moja ya binafsi jijini Dar es Salaam, lakini hospitali hiyo ilimpima mgonjwa huyo vipimo vingine ambayo havikupaswa kupimwa.

Alisema fedha zilizotumika kulipia vipimo hivyo vya ziada vingetumika kununulia dawa na vifaa tiba ambavyo vingetumika kuwahudumia wananchi wengi zaidi.

Aidha Naibu Waziri huyo aliwataka watendaji wa afya kutumia utaalamu na ujuzi wao kuaanda mipango ya kuweza kukabaliana na changamoto za sekta ya afya nchini.

“Ni lazima tutumia utaalamu tulioupata katika kupunguza shida za watu katika sekta ya afya. Tumumie elimu tuliyoipata shuleni na vyuoni ili kuboresha maisha ya Watanzania na tumsaidie Rais John Pombe Mafuguli tusisubiri hadi tuambiwe tufanye nini,”alisisitiza.

Mgonjwa huyo ambaye matibabu yake yanalipiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Kitendo cha hospitali hiyo kilionesha kumsikitisha Naibu Waziri huyo kwa kuwa fedha za Serikali ndizo zinazotumika kugharamia vipimo ambavyo, taasisi hiyo haikumwandikia mgonjwa huyo.

“ Hospitali hii imetumia nafasi hiyo ya kupima mgonjwa huyo vipimo ambayo hakuandikiwa na daktari aliyemwona katika taasisi hii. Chakushangaza baadhi ya vipimo ambayo amepimwa vipo katika taasisi hiyo. Hospitali hii imetumia vibaya mfumo wa mfuko huo kwa kumpima mgonjwa huyo vipimo vya ziada,alisema Naibu Waziri Kigwangala.

Aliwataka watendaji wa afya kuhakikisha wanawapeleka wagonjwa wanaotakiwa kupimwa vipimo vya MRI na CT- Scan katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) kwa kuwa hospitali hiyo ina vifaa vya kisasa na vinafanya kazi vizuri kwa gharama nafuu.

Naibu Waziri huyo aliagiza uongozi huo kusitisha malipo ya vipimo hivyo vya ziada kwa kushirikiana na mfumo huo wa NHIF.

“Sitisheni malipo ya vipimo vya ziada katika hospitali hiyo, mgonjwa ni wa taasisi hii anaigiliwa na taasisi nyingine kwa kupimwa vipimo vingine ambavyo havikupaswa kupimwa, hivi ni vijipu vidoovidogo vinatumbuliwa hapahapa,” alisema Waziri huyo.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo alielezwa kwamba taasisi hiyo inakabiliwa na changamoto ya vipimo vya ugunduzi wa saratani na tiba ya satarani, dawa, ambapo alisema atashirikiana na uongozi ili kuweza kukabiliana na matatizo hayo.Pia aliutaka uongozi wa taasisi hiyo na watendaji wa afya pamoja na wizara kufanya kazi kama timu ili kuweza kutatua changamoto zilizopo.(P.T)

STARSNAUGANDA4 7517d

4-1 Unaonaje matokeo haya kwa timu ambayo tunaambiwa ni timu nzuri ina kocha mzuri na maandalizi ni mazuri, tumeshindwa World cup, tumeshindwa CAN na sasa CHAN, Jamani ndugu zangu watanzania tutaweza mashindano gani?

Nilisema toka awali ni vyema sasa tukajipanga upya kwa kuisuka timu yetu tukianzia na timu za vijana nashauri udhamini mkubwa kwa Taifa stars sasa upelekwe kwenye timu za vijana za mitaani ili kuweza kuibua vipaji ambavyo vitajenga timu zenye ushindani kwenye ligi zetu.

Hivyo kwa hatua hii ilivyofikia Timu ya Taifa nadhani ni wakati wa TFF kufanya maamuzi magumu ya kuivunja Timu hii na kuisimamisha kushiriki mashindano ya kimataifa hata kwa miaka miwili na kupeleka nguvu kwenye academy za soka zilizopo sehemu mbali mbali nchini kama hizo academy hazitoshi nadhani huu ni wakati wa wizara ya Elimu na wizara ya Michezo kuweza kushirikiana kuibua vipaji katika mashule nina hakika tukitumia mfumo huu baada ya miaka michache tutakuwa na Timu bora ya Taifa.

Capt Mkami Jr

KICHWA CHA MWENDAWAZIMU HADI LINI?

Published in Uchambuzi wa Mkami Jr

kibao c99db

Ni kama soka imeshindikana jamani, Siku zote nimekuwa nikisema ukweli na sitaweza kusifia kitu ambacho hakistahili sifa yoyote sioni sababu ya kusema safi kama sio safi sioni sababu ya kusema ndiyo kama jibu ni hapana siwezi sema one wakati ni ziro,

TFF mnayo majibu  juu ya kwanini soka letu halina radha , tukianza na ligi zetu bado hazijaonyesha sura ya kwamba siku moja timu yetu ya taifa itacheza soka lenye mvuto  ukitazama soka la leo pale taifa ni wazi kuwa  mchezo wa timu yetu umekuwa ni mchezo wa mchezaji mmoja mmoja sijaona soka la timu sijaona mchezo wa kitimu maana sijaona hata kama sub inaweza badili mchezo nimeona wazi kukosekana kwa fulani mchezo wa timu nzima unabadilika .

Natoa ushauri kwa TFF, na kama hamtasoma hapa basi namuomba Maggid  Mjengwa ambaye ni mjumbe wa mkutano mkuu akipata nafasi ya kuchangia katika mikutano yenu  naomba anisemee yafuatayo ..

  1.  Ipo haja ya kuangalia upya jinsi gani ya ligi zetu ziwe ligi zenye ushindani .
  2. Maboresho katika usimamizi katika Timu ya Taifa ya vijana
  3. Kusuka upya timu ya taifa ambayo itatafutiwa michezo mingi ya kirafiki na ikiwezekana tukasimama kushiriki mashindano ya kimataifa hata kwa miaka miwili .

Na kwako msomaji unaweza ongezea mengine unayodhani yanafaa ili tusiendelee kuwa kichwa cha mwehu...

Ingia hapo TUMA MAONI ili uweze kuongezea ya kwako

 Capt Mkami Jr

 

Tujikumbushe mawili matatu kutoka kwa Marcio Maximo

Published in Uchambuzi wa Mkami Jr

wachezaji taifa stars na malawi f8ac4

Ramadan Kareem ndugu zangu Waislam, niwatakie mwezi mtukufu mwema .

Ndugu zangu watanzania mashabiki wa soka mara nyingi naweza kuwa na mtazamo wa peke yangu na wakati mwingine nisiwe na mtu wa atayeona nipo sahihi  kwa mfano zipo njia mbili za kuishi. " Moja ni hakuna kitu kilicho miujiza na nyingine ni kwamba kila kitu ni miujiza"  sijui hapo katika soka leo tutumie njia ipi?

Mechi ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) kati ya Tanzania, Taifa Stars na Uganda, The Cranes itakayochezwa Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Mechi hii ni muhimu kwa timu yetu siombei tufungwe ila naona kabisa dalili za kufungwa sioni mipango yoyote madhubuti zaidi ya kusikia matangazo ya viingilio vya mlangoni kutoka kwa wenye mamlaka na soka la Tanzania .

Sina cha kumalizia, Niwatakie Siku njema

Capt Mkami Jr


ob9 8750b

Heshima kwako mheshimiwa Rais wa 44 wa Taifa kubwa duniani  la USA ,Ndugu Barack Hussein Obama, awali ya yote nilifurahishwa na maandalizi ya ujio wako na furaha ikatimia nilivyoona kupitia Televishen ya Taifa ukishuka kutoka kwenye Air Force One, tatu nikafurahishwa vile ulivyochangamka ukiwa pale uwanjani kama haitoshi nikavutiwa vile ukidance pale uwanja wa ndege na kama bado nikapendezwa na uwezo wako wa kujibu maswali ya wanahabari ingawa nilipenda yaendelee.

Mr President nasikitika sijasikia habari ya michezo ikipewa kipaumbele katika ziara yako nilitegemea kusikia katika miradi ambayo serikari yako inafadhiri nchi yetu basi angalau suala la kujenga shule za michezo kwa kasi lingekuwa linagusiwa ,

Mr President ajira imekuwa ni tatizo kubwa katika nchi yetu hasa kwa vijana na labda tulitegemea uwepo wa uwekezaji katika michezo ungesaidia kupunguza tatizo hili ila nalo limekuwa tatizo sugu, sasa kwa mtazamo wangu Capt Mkami Jr nilitegemea itaondoa tatizo hili japo si sana ila angalau michezo uleta watu karibu na uleta furaha na amani.

Mr President pichani nimevutiwa ukiwa na mpira wa mkipasiana na Mr President mwenzio bila shaka kuna chochote mlizungumza kuhusia na hicho mnachokifanya hapo pichani, pia hii picha  kwangu inanipa neno
Je Mr President wangu ndugu Jakaya , Uwanja wa taifa,Kocha, na Timu ya taifa vinatosha kutupeleka World Cup mimi nadhani ipo haja ya kuwekeza katika michezo kwa nguvu na kwa mipango hakika tutaweza?

Capt Mkami Jr

 

 

Taifa stars fanyeni kweli

Published in Uchambuzi wa Mkami Jr

GO9G9661 aff0fMechi ya marudiano ya ya Kundi C la kuwania kufuzu kushiriki fainali zijazo za Kombe la Dunia kati ya timu ya taifa ya Morocco (Simba wa Atlas) na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itachezwa Jumamosi usiku jijini Marrakech, Morocco, 

Tunaitakia kila la kheri timu ya Tanzania katika mchezo huo muhimu , tunaamini maandalizi yametimia na kikosi kipo tayari kwa mchezo huu muhimu na tuna imani kubwa kuanzia na benchi la ufundi na wachezaji wote kwa ujumla.

Kufanya vizuri kwa timu ya taifa ni mwanzo mpya wa taifa letu hasa katika kipindi hiki cha mchakato wa katiba mpya , Michezo uondoa tofauti zetu za kisiasa , kikabila nk hivyo kufanikiwa kupata ticket ya kwenda Brazil itatuunganisha watanzania katika kipindi hiki cha maandalizi ya kupata katiba mpya.

Mungu ibariki Taifa Stars ,Mungu ibariki Tanzania

Capt Mkami Jr

Ipo siku kila mtu atashabikia Yanga

Published in Uchambuzi wa Mkami Jr

mashabiki wa Yanga wakimtania Juma Kaseja 191fc

Mwenyekiti siku ya leo umenikwepa sana hata simu zangu umekuwa haupokei mwanzo nilidhani tatizo la network , ila sasa nimejua tatizo  pole sana.

Binafsi nasema ukweli na si ushabiki timu yenu inahitaji mabadiliko hasa sehemu ya ulinzi bado mna tatizo kubwa kwenye defence  bila ubora wa kipa wenu ambaye sasa anakuwa Tanzania 2 baada ya kipa ambaye alikuwa anamuweka benchi Simba , Ali Mustapha leo mbele ya kocha mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemuonyesha kuwa anafaaa kukaa langoni mechi inayofuata ya Taifa stars katika kuwania kufuzu Kwa kombe la dunia Hapa nani anabisha Ali Mustapha  ana uwezo sasa kuzidi Kaseja?

Najua Soka la Bongo bila Yanga na Simba halitanoga hivyo siwezi omba mabaya kwa simba nawaomba uongozi wa simba pamoja na benchi la ufundi mjipange kwa msimu ujao, na Ndugu zangu yanga mimi nimefurahi leo ila kesho mtanifanya niwe sina furaha tena maana nadhani kwenye klabu bingwa kama tutatolewa raund ya Kwanza hivi!...

Yanga msibweteke Viva Yanga fanyeni kweli mpaka mmchukue ubingwa wa Klabu Bingwa hapo sijui Maggid Mjengwa atajificha wapi? ha ha ha ha leo  Simba mngeshinda aisee Mwenyekiti ungeongea sana maana ushindi kwenu ulikuwa ni kwaajili ya kuwaponda Yanga haukuwa na manufaa maana hata Kombe la shirikisho hamna nafasi.

Nachukua nafasi hii kwa niaba ya mashabiki wa Yanga kutoa pole kwa Mashabiki wa Simba .

Capt Mkami Jr

 

 

Mashabiki 3bfde

Naungana na watanzania ambao hatukupata nafasi ya kwenda uwanja wa Taifa kushuhudia timu ya taifa ikitupa raha wengine  matokeo tumeyapata kupitia Facebook , tuseme ukweli hii ni aibu tena aibu kubwa kwa tukio hili muhimu ambalo mwisho wa siku linatuunganisha watanzania, kisha TFF na wizara yenye dhamana na michezo mmeshindwa kutuonyesha pambano hili live,

Kama hata mmeshindwa kulipia kurusha matangazo ya mpira kupitia vituo binafsi why Television ya taifa ambalo ina wajibu wa kuwatumikia watanzania, najua wengine watasema kwasababu maalumu labda luninga ya taifa leo ilikuwa na jukumu la kitaifa je hii mechi haikuwa ya kitaifa au kimataifa kama vyote vilikuwa na umuhimu basi sasa kuna umuhimu tukaiona station ya michezo na burudani ikifungulia ikawa stesheni maalumu kwaajili ya michezo na burudani hapa tuweze kuona mechi za kimataifa nchi yetu inavyocheza na mechi za ligi kuu.Kwa leo sina mengi najaribu kuwasamehe kwakuwa timu imeshinda ila next time tunaomba muige mfano hata wa timu Ya Azam ilipokuwa Sudan hivi majuzi tuliweza kuona mechi yao LIVE, faida zipo nyingi sana kuonyesha mechi live Mojawapo ni kuweza kutangaza nchi Yetu kwenye nyanja tofauti kimataifa,

Kuwatangaza wachezaji kimataifa ili angalau kuelekea brazil tuwe na kina samatta hata watano hivi na ni muhimu kama ni timu ya taifa si watu elfu 60 tu wanaotosha kujaza uwanja wa taifa ndio waweze kutazama mpira hata mtu wa bukoba ndanii huko anataka kuona timu yake pia nna hata mtanzania aliyeko kenya anatamani kuiona timu yake maana siku hizi vin'gamuzi kila kona naamini hata kurusha mpira online yawezekana pia ili hata watanzania walio hata bara la ulaya waone timu yetu ikifanya mambo dimbani.Hili ni funzo nadhani kama kuna muhusika wa TFF ameona hii kuna haja ya kuifanyia kazi.

 

Capt Mkami

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Taifa Stars- Tunakwenda Brazil 2014

Published in Uchambuzi wa Mkami Jr

starz 13daa

Ni kama utabiri wangu haukuwa mbali na ukweli Yes!.. tumeshinda kwa Goli 3-1 , ila mimi nilitabiri toka asubui ya leo tutashinda 2-1, sio mbaya hapa naona nimetabiri ukweli maana nimetabiri ushindi.

Kwakweli mmenipa raha Leo naamini bado tuna safari ngumu ila ushindi pia ni lazima. kwangu mimi wote ni bora si samatta  pekee nawapongeza wachezaji na benchi la ufundi maana hata angekuwa samatta peke yake asingetupa ushindi ila naamini kwa mchango wa wachezaji wenzake na benchi la ufundi ndio ushindi umepatikana hii ni chachu kwa wachezaji wanaocheza ligi ya hapa nyumbani.

Mwisho wa ushindi huu ni mwanzo wa maandalizi ya ushindi mwingine

Capt Mkami Jr

Taifa Stars ushindi leo ni lazima

Published in Uchambuzi wa Mkami Jr

images 2b08a

Taifa stars leo ina kibarua kigumu na muhimu, kwa maendeleo ya soka letu, binafsi nashawishika kusema Taifa stars haina sababu ya kushindwa siku ya leo naaamini maandalizi imepata ya kutosha hii inathibitishwa na mechi za kirafiki ilizocheza na hivi karibuni ilicheza na vigogo cameroon
na matokeo yanathibitisha kuwa timu iko tayari kuingia dimbani siku ya leo.

sitegemei sababu zozote za kushindwa  siku ya leo  kazi kwenu wenye dhamana ya soka tukianzia uongozi wenye mamlaka na usimamizi wa soka hapa namaanisha TFF, benchi zima la ufundi na wachezaji, matumaini yetu yapo kwenu wachezaji 11 ambao ni sehemu ya watanzania zaidi ya milioni 40 hivyo naomba muelewe kuwa mna dhamana kubwa kwa taifa letu.

Natumaini leo mtanifanya nijivunie kuzaliwa mtanzania, Yes ushindi ni lazima leo


Mimi natabiri tutashinda Goli 2-1

Capt Mkami JR

Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA