We have 314 guests and no members online

Kwa jambo hili tff, wizara ya habari na michezo mmechemsha na mnatakiwa mtuombe radhi mashabiki

Mashabiki 3bfde

Naungana na watanzania ambao hatukupata nafasi ya kwenda uwanja wa Taifa kushuhudia timu ya taifa ikitupa raha wengine  matokeo tumeyapata kupitia Facebook , tuseme ukweli hii ni aibu tena aibu kubwa kwa tukio hili muhimu ambalo mwisho wa siku linatuunganisha watanzania, kisha TFF na wizara yenye dhamana na michezo mmeshindwa kutuonyesha pambano hili live,

Kama hata mmeshindwa kulipia kurusha matangazo ya mpira kupitia vituo binafsi why Television ya taifa ambalo ina wajibu wa kuwatumikia watanzania, najua wengine watasema kwasababu maalumu labda luninga ya taifa leo ilikuwa na jukumu la kitaifa je hii mechi haikuwa ya kitaifa au kimataifa kama vyote vilikuwa na umuhimu basi sasa kuna umuhimu tukaiona station ya michezo na burudani ikifungulia ikawa stesheni maalumu kwaajili ya michezo na burudani hapa tuweze kuona mechi za kimataifa nchi yetu inavyocheza na mechi za ligi kuu.Kwa leo sina mengi najaribu kuwasamehe kwakuwa timu imeshinda ila next time tunaomba muige mfano hata wa timu Ya Azam ilipokuwa Sudan hivi majuzi tuliweza kuona mechi yao LIVE, faida zipo nyingi sana kuonyesha mechi live Mojawapo ni kuweza kutangaza nchi Yetu kwenye nyanja tofauti kimataifa,

Kuwatangaza wachezaji kimataifa ili angalau kuelekea brazil tuwe na kina samatta hata watano hivi na ni muhimu kama ni timu ya taifa si watu elfu 60 tu wanaotosha kujaza uwanja wa taifa ndio waweze kutazama mpira hata mtu wa bukoba ndanii huko anataka kuona timu yake pia nna hata mtanzania aliyeko kenya anatamani kuiona timu yake maana siku hizi vin'gamuzi kila kona naamini hata kurusha mpira online yawezekana pia ili hata watanzania walio hata bara la ulaya waone timu yetu ikifanya mambo dimbani.Hili ni funzo nadhani kama kuna muhusika wa TFF ameona hii kuna haja ya kuifanyia kazi.

 

Capt Mkami

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

HEADER

Guest
0Guest2013-03-24 22:07#1
Basi ni aibu kubwa sana kama hakuna kituo cha television kilichorusha huo mpira muhimu kwa waTz. Ila sie tuliopo nje ya nchi tumeweza kuuona live kabisa bila chenga kupitia mtandaoni (online). Tushukuru waarabu waliorusha mpira huo mtandaoni. Viva Taifa stars!
Mnukuu

Tuma Maoni


Security code


Anzisha upya


Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA