habari

Milipuko Miwili Yaua Watu 21 Wakiwemo Waandishi Wanne.

on

Takribani watu 21 wakiwemo waandishi wa habari wane wameuwawa, baada ya kutokea milipuko miwili ya mabomu katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul. Katika tukio hilo, makumi ya watu wameripotiwa kujeruhiwa.

Milipuko hiyo imetokea jumatatu hii majira ya asubuhi katika eneo la Shashdarak, ambapo katika mlipuko wa kwanza, mshambuliaji wa kujitoa muhanga alitekeleza shambulio hilo karibu na kituo cha taifa kinachoshughulikia masuala ya Usalama. Ripoti zinasema mlipuko wa pili ulifuata dakika 20 baadae baada ya watoa huduma za dharura pamoja na wanahabari kufika eneo ulipotokea mlipuko wa kwanza.Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya afya, amesema shambulio hilo limeua karibu watu 21 na kujeruhi wengine 27.

Jennifer Glasse mwanahabari wa Al Jazeera ameripoti kuwa wanahabari wane waliokuwa wakiripoti tukio la kwanza wamepoteza maisha baada ya kutokea kwa mlipuko wa pili.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *