habari

Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki Waahirishwa Kwa Mara Nyingine Tena

on

Hatimaye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imetoa taarifa rasmi  ya kuahirishwa mkutano wa 20 wa marais wa jumuiya hiyo uliokuwa ufanyike Desemba 27, 2018.
Taarifa hiyo imetolewa na mkuu wa mawasiliano kwa umma wa EAC, Richard Owora bila kufafanua sababu za kuahirishwa mkutano huo.
Mkutano wa awali ambao ulikua ufanyike Novemba 30 uliahirishwa dakika za mwisho wakati marais watatu wakiongozwa na Mwenyekiti wao Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na Rais wa Tanzania, John Magufuli walipokutana.
“Mwenyekiti (Rais Yoweri Museveni) anaendelea na mashauriano na marais wenzake juu ya hatua zaidi,” imesema taarifa hiyo.
Mkutano wa Novemba 30 haukufanikiwa baada ya nchi ya Burundi kugoma kutuma ujumbe kutokana na mgogoro wa kisiasa kati yake na jirani yake Rwanda.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *