habari

Mlipuko Wa Volcano Guatemala Waua Watu 25.

on

Idara inayokabiliana na majanga nchini Guatemala humo imesema zaidi ya watu 25 wamepoteza maisha na 20 wamejeruhiwa, baada ya mlipuko wa volkano kutokea katika taifa hilo

Awali serikali ya Guatemala imesema kuwa majivu ya volkano kutoka mlima mmoja unaoendelea kulipuka, yamesababisha vifo vya watu saba na kuwajeruhi wengine ishirini.

Mlipuko wa Volkano ya Fuego (Volkano ya moto), inayopatikana kilomita 35 kusini-magharibi mwa mji mkuu wa Guatemala, umesababisha maelfu ya watu na kuhamishwa na uwanja wa ndege wa kimataifa umetakiwa kufungwa.

Serikali ya Guatemala inasema kuwa takribani watu milioni moja wameathirika kutokana na Volcano hiyo.

Hata hivyo ushauri umetolewa kwa raia kuvaa vifaa vya kuzuia pua zao kutokana na moshi na majivu yanayoendelea kurushwa kutokana na Volcano hiyo.

Mlipuko huo umeathiri hasa wilaya za vijijini zilizo karibu na volkano hiyo na mji wa kikoloni wa Antigua, eneo muhimu kwa utalii nchini Guatemala.

Kulingana na ripoti mpya, watu zaidi ya 25 ndio wamepoteza maisha, watoto kadhaa ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha, amesema msemaji wa idara ya ya kitaifa inayokabiliana na majanga (Conred), David de Leon.

Amesema kuwa watu 25 walioppteza maisha walipatikana katika maeneo mawili yalio karibu na volkano, El Rodeo na Las Lajas.

Rais wa taifa hilo Jimmy Morales amesema vikosi vya uokoaji vimeanza kazi na tahadhari imetolewa.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *