habari

Mripuko Wa Ebola Wachukua Sura Mpya.

on

Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Oly Ilunga Kalenga, amesema mripuko wa maradhi hatari ya Ebola nchini humo umechukua sura mpya baada ya kuenea hadi mjini Mbandaka. Jiji hilo lililo Kaskazini Magharibi mwa nchi lina wakazi takribani milioni moja.

Katika tangazo lililotolewa na Waziri Kalenga alisema baada ya kugundulika kwa Ebola katika jiji hilo, wataalamu wa afya wanafanya juhudi kuwatambua watu ambao wamekuwa karibu na wale waliothibitishwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo. Naibu Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO anayehusika na miripuko, Peter Salama, amesema zoezi la kutoa chanjo ya Ebola huko Kongo linakabiliwa na changamoto za kiufundi. Awali, WHO ilikuwa imeelezea wasiwasi kuhusu kuenea kwa Ebola hadi Mbandaka, ikisema hali hiyo ingezifanya juhudi za kuzuia mripuko mkubwa kuwa ngumu zaidi. Inaaminika kuwa mripuko mpya wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao ulianzia katika jimbo la Equateur tayari umeuwa watu 32.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *