habari

Mshambuliaji Wa Kujitoa Muhanga Aua Watu 10 Somalia.

on

Jeshi la Polisi nchini Somalia pamoja na mashuhuda, wamesema kuwa Watu 10 wameuawa na wengine takribani wanane kujeruhiwa, baada ya Mshambuliaji wa kujitoa muhanga kutekeleza shambulizi katika soko lililoko wilaya ya Walayen, jimbo la Lower Shabelle kusini mwa Somalia.

Shambulizi hilo la kujitoa muhanga, lilifanyika baada ya mshambuliaji aliyekuwa akiendesha bajaji, kujaribu kuligonga gari la jeshi la Somalia. Afisa wa polisi Ahmed Ali ameliambia shirika la habari la DPA kuwa, inaonekana mshambuliaji huyo hakufanikiwa kulilenga gari hilo, na badala yake bomu hilo likawauwa raia waliokuwa katika soko lililopo karibu na eneo lilipokuwa gari hilo.

Pamoja na vifo na majeruhi, kumeripotiwa uharibifu mkubwa, na hakuna aliyejitokeza mara moja kudai kuhusika na shambulizi hilo, ingawa Ali amesema huenda limefanywa na wanamgambo wa Al-Shabaab.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *