habari

Mshukiwa Wa Ugaidi Ahukumiwa Miaka 20 Jela.

on

Mahakama jijini Brussels nchini Ubelgiji imemhukumu  Salah Abdeslam kifungo cha miaka 20 gerezani kwa kosa la jaribio la mauaji, baada ya kushiriki katika tukio la ufyatulianaji risasi na polisi mjini Brussels mwaka 2016.

Abdeslam mwenye umri wa miaka 28 raia wa Ufaransa, anaaminika kuwa mtu pekee aliyenusurika katika kundi la kigaidi, lililopanga na kutekeleza mashambulizi katika mji mkuu wa Ufaransa Paris mwezi Novemba 2015, ambapo watu 130 walipoteza maisha.

Hukumu hiyo dhidi yake imetolewa katika kesi ya nchini Ubelgiji ambayo ilijikita katika uvamizi wa polisi mwezi Machi 2016, ambapo mmoja wa washukiwa Mohamed Belkaid aliuawa huku maafisa kadhaa wa polisi wakijeruhiwa.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *