habari

MTENDAJI WA KIJIJI KURUYA APEWA SIKU 19 KUREJESHA FEDHA ALIZOTAFUNA

on

Afisa utumishi Wilaya ya Rorya Mkoani Mara Peter Masanja akiongea na Wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kuruya kata ya Komuge Wilayani Rorya Mkoani Mara.
Wananchi wa kijiji cha Kuruya wakiwa katika Mkutano wa hadhara.
Wananchi wa kijiji cha Kuruya wakiwa katika Mkutano wa hadhara.
Mtendaji wa kijiji cha Kuruya Mwita Mangondi aliyesimamishwa Kazi katika Mkutano huo akijibu baadhi ya hoja za Wananchi zikiwemo tuhuma zake za ubadhilifu wa fedha.
Diwani wa kata ya Komuge William Nestory akiongea na Wananchi katika Mkutano huo ambapoameomba Afisa Utumishi kutilia Mkazo kufanyika kwa Vikao vya Kisheria ili wanaanchi wasomewe Mapato na Matumizi.
Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Wilayni Rorya Aloyce Marenge akitoa somo kwa wananchi hao ambapo amesema kuwa kutunza fedha za serikali katika akaunti ya binafsi ni kosa kisheria huku akihaidi wananchi hao kufuatilia suala la upotevu wa fedha zilizosababisha Mtendaji wa kijiji kusimamishwa kazi zinapatikana na kuchukuliwa hatua kali.
Kutoka kushoto ni Mtendaji wa Kijiji cha Kuruya Mwita Mangondi ambaye amesimamishwa kazi akiwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bernard Wambura ambaye pia wananchi wamemutupia lawama kuwa kiti chake kinapwaya naye amekuwa akikumbwa na tuhuma mbalimbali za ubadhilifu wa fedha za serikali japokuwa mpaka saas ameisha rejesha fedha hizo.
Na Frankius Cleophace, Rorya
SERIKALI imemsimamisha kazi Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kuruya katika Kata ya Komuge wilayani Rorya mkoani Mara Mwita Mangondi kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha Sh.1,960,387 ikiwa ni pamoja na kushindwa kusomea wananchi mapato na matumizi huku akipewa siku 19 kurejesha mara moja fedha hizo.
Ofisa Mtendaji huyo amesimamishwa kazi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kuruya baada ya wananchi kutoa kilio chao cha muda mrefu kuhusu kutosomewa mapato na matumizi tangu Mwaka 2012 mpaka sasa.
Ambapo wamezidi kutupia lawama viongozi waliopo kuanzia ngazi za Vijiji hadi kata.Ofisa Utumishi Wilaya ya Rorya Peter Masanja akiwa katika mkutano huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Charles Chacha amesema asimamisha kazi mtendaji huyo nakumpa siku 19 kurudisha fedha hizo. Pia anatakiwa kuripoti kila siku ofisi ya Mtendaji wa kata
Amesema kuwa kitendo cha Mtendaji huyo kufanya ubadhirifu wa fedha hizo kutokana na sheria za utumishi hawawezi kulifumbia macho hivyo amewataka wananchi kuwa wavumilivu kuhusu kumwondoa madarakani mwenyekiti wa Kijiji hicho kutokana na tuhuma walizozisema wananchi katika mkutano huo.
“Mimi Mamlaka niliyonayo ni ya kuondoa Mtendaji wa kijiji lakini sina mamlaka ya kuondoa Mwenyekiti nyie ndo wenye mamlaka mkifuata taratibu lakini kwa sasa mkimwondoa Halmashauri hautuafanya uchaguzi mpaka mwakani sasa baadhi ya maendeleo yatazidi kukwama niwasihi kuwa wavumilivu,” amesema.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Komuge William Nestory amesema kuwa endapo fedha hizo hazitarudishwa ataungana na wananchi kutoa taarifa eneo husika.
Huku akiomba Ofisa utumishi kutilia mkazo kufanyika kwa mikutano ya kisheria ili wananchi wasomewe mapato na matumizi kwani suala hilo limekuwa changamoto kubwa katika vijiji vinavyounda kata yake.
Amewataka wananchi kuendelea kujitoa katika suala la kuchangia maendeleo ikiwemo ujenzi wa maboma katika sekta ya elimu na afya ili Serikali iweze kumalizia.“Nikiwa katika Halmashauri fedha zinakuja naulizwa kama kuna maboma ili fedha zije kumalizia hakuna wananchi hawaji kwenye maendeleo viongozi wa vijiji ni mizigo sasa tumechoka kila sehemu napita lawama za fedha za wananachi,” amesema.
Kwa upande wa Kaimu Mkuu wa Takukuru wilayani Aloyce Marenge amesema fedha za Serikali kukaa mikononi mwa mtu na kuwekwa katika akaunti ya mtu binafsi na siyo akaunti ya Serikali ya kijiji ni kosa kisheria.
Pia akihaidi kafuatilia fedha hizo zinalipwa mara moja na kuchukua hatua kali dhidi ya kiongozi huyo.“Sisi Takukuru tutaendelea kufanya kazi yetu ikiwa ni pamoja na Kuhakikisha mtendaji huyo anarejesha pesa zote kama alivyoewa mwisho wa Mwezi na hatua nyingine zitaendelea kuchukuliwa,” amesema Aloyce.
Awali katika mkutano wa wananchi uliofanyika katika kijiji cha Kuruya kata ya Komuge Wilayani Rorya mkoani Mara wananchi wanatupia lawama viongozi wa Serikali za Vijiji akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji hicho Benard Wambura kuwa wamekuwa wakitunza fedha za Serikali mifukoni mwao na kushindwa kusoma mapato na matumizi na wakati mwingine kujikopesha wenyewe fedha hizo suala ambalo limewachosha wananchi.
Ili kikao kiweze kuendelea vizuri Mwenyekiti wa kijiji hicho Benard Wambura na Mtendaji aliyesimamishwa walipisha kiti Mpaka mkutano huo unamalizika kutokana na wananchi hao kuwatuhumu na kudai wakiendelea kuongoza kikao kuna baadhi ya wananchi wataminywa kuongea ukweli unaowahusu.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *