siasa

Mtulia Na Mollel Waapishwa.

on

Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia na mbunge wa jimbo la Siha Dkt. Godwin Mollel (Wote kwa tiketi ya CCM) Wameapishwa Leo April 3 bungeni mjini Dodoma. Kuapishwa kwa wabunge hao kulikofanywa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson  ni baada ya kufanyika uchaguzi mdogo wa marudio katika majimbo hayo mawili ambayo hapo awali yalikuwa hayana wawakilishi bungeni kutokana na viongozi wake kujiuzulu nyadhifa zao kwa kuhamia CCM.

Aidha, kiapo hicho cha leo kimeshuhudiwa na idadi ndogo ya wabunge wa upinzani kutokana na baadhi yao kuwepo katika mahakama ya mkazi Kisutu kusikiliza mwenendo wa kesi inayowakabili viongozi sita wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA miongoni mwao akiwa ni mwenyekiti wa chama hicho na mbunge wa jimbo la Hai, Freeman Mbowe.

Kutokana na kiapo hicho, Mtulia na Dkt. Mollel watakuwa wamekubali moja kwa moja kubeba mizigo ya matatizo kutoka kwa wananchi wao ambayo ilikuwa ikiwasumbua kipindi kirefu pamoja na kuwatekelezea ahadi walizokuwa wamezitoa kipindi walichokuwa wanaomba ridhaa ya kupigiwa kura ya ndio ili waweze kuwa Wabunge katika majimbo hayo.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *