habari

Museveni Aahidi Kufufua Shirika La Ndege.

on

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema taifa hilo la Afrika Mashariki litafufua shirika lake la ndege, ili nayo iweze kushiriki katika biashara ya anga inayozidi kukua katika eneo hilo, pamoja na kuimarisha sekta yake ya huduma.Museveni ameyasema hayo katika hotuba yake bungeni, lakini hakutaja ndege zitaagizwa kutoka kampuni gani.

Waziri wa usafiri na kazi aliwahi kuviambia vyombo vya habari kwamba serikali imeagiza ndege kutoka kampuni ya Canada ya Bombardier.Museveni amesema kila mwaka Waganda wanatumia dola milioni 430 katika safari za anga, hali inayopaswa kusitishwa. Uganda inajenga uwanja wa ndege wa pili wa kimataifa na uwanja wake wa ndege wa kwanza wa kimataifa uliopo mjini Entebbe, kusini mwa mjini mkuu wa Kampala unapanuliwa ili kuweza kuwapokea abiria wengi zaidi pamoja na usafirishaji wa mizigo. Mradi huo wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Entebbe unatumia fedha za mkopo kutoka China.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *