habari

Museveni Atangaza Siku Tatu Za Maombolezo.

on

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza siku tatu za maombolezi ya kitaifa, kufuatia vifo vya watu 22 baada ya ajali ya barabarani katika Wilaya ya Kiryandongo ijumaa ya wiki iliyopita.

Bendera zote nchini humo zinapepea nusu mlingoti kwa heshima ya watu hao. Ajali hiyo ilihusisha basi la abiria na Lori la mizigo.Aidha, serikali itatoa Shilingi za nchi hiyo Milioni 5 kwa kila Familia kuisadia katika shughuli za mazishi.

Takriban watu 22 wakiwemo watoto watatu waliuwa kwenye ajali ya basi lililogonga tingatinga ambayo ilikuwa ikiendeshwa bila ya taa usiku kwa mujibu wa msemaji wa polisi Emilian Kayima ambaye aliongea na shirika la habari la AFP.

Awali shirika la msalaba mwekundu lilisema kuwa jumla ya vifo ni 48 wakiwemo watoto 16. Uganda ina kati ya rekodi mbaya zaidi za usalama wa barabara ambapo kwa mujibu wa takwimu rasmi kati ya mwaka 2015 na 2017 Zaidi ya watu 9,500 waliuawa kwenye ajali za barabarani nchini humo.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *