michezo

Mwanariadha Aangua Kilio Baada Ya Kuwa Mshindi Wa Nne Michuano Ya European

on

Mwanariadha wa Israeli, Lonah Salpeter amejikuta akimwaga machozi hadharani mara baada ya kushika nafasi ya nne kwenye michuano ya European mbio za mita 5,000.

Mashindano hayo yaliyofanyika Berlin mashabiki wameshuhudia mwana dada, Salpeter ambaye ni mzaliwa wa Kenya anayeiwakilisha Israeli akipoteza matumaini ya ushindi hata wanafasi ya pili mara baada ya kujisahau na kuanza kusherehekea kabla ya raundi ya mwisho haijafikia kikomo na hivyo kujikuta akiangukia kwenyenafasi ya nne.

Siku ya Jumatano ya wiki iliyopita Lonah Salpeter aliweza kushinda mbio za mita 10,000 kabla ya kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho cha mita 50,000 na kujikuta akiambulia patupu kutokana na kuamini kuwa muda wa raundi hiyo umekamilika kumbe ulikuwa umebaki mzunguko mmoja.

About Innocent Chambi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *