habari

Mwanasayansi Mashuhuri Stephen Hawking Afariki Dunia Leo March 14,2018

By

on

HAWKING, EINSTEIN Na GALILEO GALILEI
Je, wajua mwanasayansi mashuhuri Stephen Hawking aliyefariki dunia leo amefariki siku sawa na ambayo mwanasayansi mwingine maarufu Albert Einstein alizaliwa? Tarehe 14 Machi. Wote walifariki wakiwa na umri wa miaka 76. Prof Hawking pia alizaliwa siku ambayo mwanasayansi mwingine maarufu Galileo Galilei alifariki, tarehe 8 Januari.
Je, wajua leo pia ni siku ya Pi (alama yake ni π), namba ya duara ambayo ni maarufu sana katika sayansi na hesabu? Kwa waliosahau, Pi huanza 3.141592653589793238462643…. (na kuendelea) lakini haiwezi kuandikwa kamili kwa kuongeza tarakimu baada ya nukta maana hakuna mwisho wake. Siku ya Pi huadhimishwa leo kwa sababu tarehe ya leo huanza kwa kuandikwa 3.14 (Mfano, leo ni 3.14.2018)
Galileo Galilei (Kuzaliwa: 15 Februari 1564, Pisa, Italia
Kufariki: 8 Januari 1642, Arcetri, Italia)
Albert Einstein (Kuzaliwa: 14 Marchi 1879, Ulm, Ujerumani
Kufariki: 18 Aprili 1955, Princeton, New Jersey, Marekani)
Stephen Hawking (Kuzaliwa: 8 Januari 1942 Oxford, England
Kufariki: 14 Machi, 2018).

About mjengwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *