habari

Mwandishi Na Wahariri Gazeti La Raia Mwema, Kufikishwa Mbele Ya Kamati Ya Maadili.

on

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amemtaka mwandishi wa gazeti la Raia Mwema, Paschal Mayala na wahariri wa gazeti hilo kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya Bunge ili kuhojiwa kwa madai ya kulidhalilisha Bunge.

Wito huo wa Spika Ndugai ametolewa wito huo leo Aprili 12, 2018 Bungeni mjini Dodoma, wakati spika akitolea maamuzi mwongozo wa Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga, aliouomba Bungeni kulitaka lichukue hatua kwa kile alichokieleza kwamba gazeti hilo limechapisha makala yenye mlengo wa kulidhalilisha Bunge hilo.

Kuitwa kwa Mayala ni kutokana na kuandika makala kwenye gazeti hilo toleo la Aprili 9, 2018, ambayo Spika ameitaja kuwa iliandikwa kuwa “Bunge Linajipendekeza kwa Serikali.”.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *