habari

Mwili Wa Bilago Kuagwa Bungeni Mei 8.

on

Taarifa ya Spika wa Bunge, Job Ndugai inasema mwili wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Buyungu kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kasuku Bilago utaagwa Jumatatu Mei 28, 2018 bungeni mjini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa na kitengo cha habari, elimu na mawasiliano cha Bunge, imeeleza kuwa baada ya kuaga mwili huo utapelekwa Kakonko mkoani Kigoma kwa ajili ya mazishi.

Marehemu Bilago amefariki dunia jana saa tisa alasiri katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuhamishwa akitokea Hospitali ya DCMC iliyopo eneo la Ntyuka jijini Dodoma alikokuwa amelazwa.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *