habari

Mzee Mwinyi: Rais Magufuli Mimi Nina Kuhusudu Kwasababu Unafanya Mambo Mazuri Kwa Wananchi

on

Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi hii leo October 2 alikuwa mmoja wa waalikwa kwenye Ikulu ya Rais Magufuli wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje sambamba na kuapishwa kwa mkuu wa Skauti nchini.

Mlezi huyo wa Skauti nchini Alhaj Ali Hassan Mwinyi akapewa nafasi ya kutoa neno kwa rais Magufuli.
Katita salamu zake fupi, Rais Mstaafu Mwinyi amesema kuwa aliomba kustaafu kuwa Mdhamini wa Skauti Tanzania ombi ambalo lilikataliwa na Rais Magufuli,na kusema kuwa bado vijana wana mambo mengi ya kujifunza kutoka kwake.
Pia Mzee Mwinyi amesema anamhusudu  sana Rais John Magufuli kwa sababu anafanya mambo mazuri kwa wananchi wa Tanzania  na yanamgusa sana.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *