habari

Mzee wa miaka 53 ajitoa uhai kwa kutumia kisu Arusha

on

 

Na Mwandishi wetu Arusha

Katika hali iliowashanagza wengi mkaazi mmoja wa Mtaa wa Simanjiro, Kata ya Sombetini Mkoani Arusha ,Lazaro Kiolori(53) amechukua uamuzi wa kujiua kwa kutumia kisu kidogo huku chanzo kikielezwa ni ugomvi wa kifamilia.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,Jonathan Shanna amethibitisha kutokea kwa kifo hiocho na kusema kuw atukio hilo limeacha simanzi kubwa kwa ndugu na jamaa  wa marehemu huyo.

Amesema uchunguzi wa awali umeonesha chanzo cha marehemu kujitoa uhai wake ni mgogoro uliokuwepo kati yake na wake zake wawili.

Amesema licha ya uchunguzi huo kubaini taarifa hizo lakini kwa sasa asingekua tayari kuwataja watu hao ambao walikua na mgogoro na marehemu huyo kabla ya kifo chake.

Hata hivyo alisema kuwa jeshi la polisi liliwahi kufika eneo la tukio na jitihada za kumwokoa hazikufanikiwa na kumkuta mtu huyo akiwa tayari ameshafariki.

Hata hivyo kamanda aliwataka wananchi kuacha kuchukua hatua mikononi mwao hata ikitokea wana msongo wa mawazo au wametafautina kw anamna moja au nyengine.

 

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *