habari

Naibu spika wa Bunge TZ akerwa na wabunge wanaotumia simu kujirekodi

on

Na mwandishi wetu Dodoma

DTabia ya baadhi ya wabunge wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania kuingia na kutumia simu zao kama kifaa cha kujirikodia imezua mjadala mpya ndani ya Bunge hilo baada ha ya Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kuwataka kuacha mara moja  wanaofanya hivyo.

Amesema wapo  baadhi ya  wabunge hao huamua kufanya hivyo ikiwemo kurekodi  sauti hizo ambazo hazijaingizwa katika kumbukumbu za Bunge na kuzitumia maeneo mbalimbali na kuonekana ni kauli walizozitoa bungeni.

Alitoa  kauli hiyo  bungeni jijini Dodoma katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mwaka 2019/2020 baada ya mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kuendelea kuzungumza licha ya muda wake kumalizika.

Hata hivyo alisema ni lazima wabunge wafahamu kuwa kufanya hivyo ni kinyume na taratibu na kwamba imefika wakati wanaofanya hivyo kutovumiliwa.

“Halafu  anakuwa yeye mwenyewe, jirani yake au rafiki yake anachukua maneno hayo kama mchango wake bungeni wakati yeye ameshakatwa,nasisitiza ni vyema mzifahamu vizuri kanuni zetu hairuhusiwi kwa sababu si mchango uliotoka Bungeni.

 

Imehaririwa na Mohamed Khamis

 

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *