habari

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI AFANYA ZIARA MKOANI ARUSHA

on

 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia ng`ombe wa uhimilishaji katika kituo cha Taifa cha(NAIC) kilichpo Usa River jijini Arusha.
 Mkufunzi mwandamizi wa kitengo cha teknolojia ya maziwa,Theresia Teti  akimwelezea  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega namna ya usindikaji wa maziwa jijini Arusha.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia namna ya uhimilishaji unavyofanyoka katika kituo cha Taifa cha(NAIC) kilichopo Usa River jijini Arusha.Picha na Emmanuel Massaka,MMG Arusha)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akitembelea shamba la samaki Shazan lililopo jijini Arusha.
Na Kumbuka Ndatta,Arusha

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ulega ametembele taasisi za Serikali zilizopo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na wadau wengine wa sekta ya mifugo na uvuvi.

Akitoa taarifa fupi kwa Naibu waziri,Mkurugenzi wa Wakala wa vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) Kampasi ya Tengeru Joseph Msemwa amemweleza Ulega kuwa kazi kubwa ya LITA ni kutoa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi,kufanya utafiti na ushauri elekezi na uzalishaji Mali.

Pia mafunzo hayo yamejikita katika fani ya afya ya mifugo na uzalishaji.Aidha mafunzo hayo yanalenga kutoa watalaam wenye ujuzi wa hali ya juu katika fani za ufugaji.Amesema lengo ni kuwa na mtazamo wa Kujiajiri na kuendesha miradi mbalimbali ya kibiashara.

Msemwa amemwambia Naibu Waziri baadhi ya changamoto zinazoikabili Kampasi hiyo kuwa ni uchakavu wa majengo,huduma duni za maji,upungu wa watumishi na Muundo wa Wakala.Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa LITA (CEO)Magreth Pallangyo pamoja na kupokea maagizo kutoka kwa Naibu Waziri,ameahidi kuyatekeleza maagizo yote yaliyotolewa na kuyashughukia ipasavyo.

Akihutubia watumishi waliofika katika ukumbi wa Kampasi ya Tengeru Ulega amesema kuwa vyuo hivi vya mafunzo ya mifugo ndio nguzo mama katika kuchochea maendeleo ya uchumi wa Taifa letu.”Wakufunzi wa Vyuo hivi vya Mifugo jitahidi sana kuhusianisha kile mnachokifundisha darasani na mazingira halisi ya itanzania.

“Toeni elimu bora ili muweze kuwasaidia vijana hawa na taifa kwa ujumla.Vijana hawa wakitoka hapa tunataka waone kuwa wamezungukwa na fursa za kiuchumi,” amesema Ulega.

Pia Ulega amesema kuwa ni jukumu la vyuo hivyo kuhakikisha vinatoa vijana walioiva kitaaluma ili wakitoka hapo waweze kutoa elimu bora ya namna ya uchakataji wa nyama, maziwa,vyakula vya mifugo na namna bora ya uchunaji wa ngozi, kwani ngozi hizo ni malighafi ya Viwanda vyetu na itasaidia kuendana na soko la ndani ya nchi yetu na nje ya nchi.

Katika hatua nyingine Ulega amepata fursa ya kutembelea Kituo cha Uzalishaji Mifugo Kwa Chupa (National Artificial Insermination Centre) na kushuhudia baadhi ya madume ya ng’ombe yaliyopo kituoni hapo.

Mkurugenzi wa Kituo hicho Dk.Mollel amesema kituo hicho kwa sasa kinazalisha mbegu bora za ng’ombe na hewa baridi aina ya (Liquid Nitrogen) kwaajili ya kuhifadhia mbegu na kutoa vifaa vyote vya uhimilishaji ambayo ni mitungi ya kuhifadhia na Kusafirisha Mbegu.

Vilevile Dkt. Mollel amemueleza Naibu Waziri kuwa kwa mwaka 2018/2019 kituo hicho kimejipanga kuhimilisha ng’ombe takribani milioni tatu hivyo katika kipindi cha miaka mitano ng’ombe takribani milioni 10 watakuwa wameshahimilishwa.Amesema na hiyo ni kutokana na juhudi za Serikali katika kuboresha Sekta ya Mifugo hapa nchini.

Pia kituo cha NAIC kinatoa wataalam wa uhimirishaji ikiwa ni pamoja na watu binafsi wanaoteuliwa na vikundi vya wafugaji na vilele kukusanya na kutunza takwimu muhimu za himulishaji.

Awali Naibu Waziri Ulega alipata fursa ya kutembelea wadau mbali mbali wa mifugo na uvuvi mkoani Arusha ikiwa ni pamoja na kiwanda cha ngozi cha Salex LTD,Shamba la Ufugaji samaki la Shazain na Ezekiel Mhina.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *