habari

Nape Nnauye ajiuzulu uenyekiti wa kamati ya Bunge

on

Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai amethibitisha kupokea barua ya mbunge wa Mtama Mh. Nape Nnauye kujiuzulu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.
Kagaigai amesema jana Jumatatu Februari 04, 2019 Nape aliandika barua kwenda kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ya kujiuzulu nafasi hiyo na tayari spika amempatia nakala ya barua hiyo.
”Ni kweli nimeiona barua aliyomwamndikia Spika na mimi nimepata nakala yangu kwahiyo ni kweli amejiuzulu labda awe na mawazo mengine”, amesema.
Machi mwaka 2017, Nape aling’olewa kwenye nafasi ya Uwaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambayo sasa ipo chini ya Waziri Harrison Mwakyembe.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *