habari

Necta Yafuta Matokeo Ya Darasa La 7 Kwa Shule Zote Za Chemba Na Baadhi Ya Shule Za Kinondoni, Ubungo, Mwanza Na Kondoa

on

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza kuyafuta matokeo ya mitihani ya Darasa la saba kwa shule za msingi zote zilizopo ndani ya Halmashauri ya Chemba, pamoja na baadhi ya shule katika halmashauri ya Kondoa, Kinondoni, Mwanza jiji na Ubungo kwa kosa la kuhusika kwa kuvujisha kwa mitihani ya darasa la saba ikiwa ni kinyume na taratibu na kanuni za mitihani nchini.

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Oktoba 2, 2018 amezitaja shule  zilizofutiwa matokeo ni za halmashauri ya Chemba, Kondoa mkoani Dodoma.

Zingine ni Hazina na New Hazina, Aniny Nndumi na Fountain of Joy za jijini Dar es Salaam na Alliance na New Alliance na Kisiwani zote za Mwanza.

Dk Msonde amesema baada ya uchunguzi shule hizo zimebainika kuvujisha mitihani hiyo iliyofanyika Septemba 5 na 6 wakishirikiana na waratibu wa elimu wa eneo husika.

“Kufuatia kuvunjwa kwa kanuni za mitihani baraza limeamua kufuta matokeo ya kumaliza shule ya msingi ya halmashauri ya Chemba pamoja na shule ya Hazina na Kinondoni, Anyindumina na Fountain of Joy za Ubungo, Alliance na New Alliance ya Mwanza jiji pamoja na Kondoa Integrity ya Kondoa Mjini, na watahiniwa wa mtihani hiyo watairudia tena oktoba 8 na tarehe 9 wiki ijayo” Amesema Charles Msonde.

Aidha baraza hilo limefuta vituo vya mitihani kwa shule nane ambazo zilihusika katika uvujishaji wa mitihani hiyo sambamba na kupendekeza kuondolewa kwenye nafasi za ajira kwa baadhi ya maafisa elimu kata na wilaya waliohusika kwenye udanganyifu huo.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *