habari

“Nyumba Yako Yenye ‘X’ Ya Kijani Hutakiwi Kubomoa Mpaka Ulipwe Fidia”-JPM.

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amewataka wananchi wa Tanzania kiujumla kutovunja nyumba zao zilizoweka alama X yenye rangi ya kijani bila ya kupatiwa fedha zao za fidia kama inavyopaswa kwa mujibu wa sheria. Rais amesema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mang’ula Mkoani Morogoro waliposimamisha msafara wake na kutoa kero zao mbalimbali zinazowakabili katika maeneo yao.

“Kuna nyumba zimewekwa alama ya X ya kijani, msibomoee. Nyumba yako yenye X ya kijani hutakiwi kubomoa, siku utakayobomoa lazima uwe umepewa hela. Nataka muwaelimishe watanzania wote kuwa ukikuta nyumba yako au ukuta wako umewekwa alama ya X ya kijani na kijani wote mnaifahamu kama kuna mtu hajui rangi ya kijani aende angalie hata nguo za kijani za CCM,”amesema Rais Dkt. Magufuli

Aidha, amesema kuwa mwananchi yeyote akikuta amewekewa alama ya X ya kijani hawatakiwi kujenga nyumba nyingine katika eneo hilo.

Hata hivyo, Rais Magufuli ameongeza kuwa atasimama pamoja na wananchi katika kuwapambania masuala ya maendeleo.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *