habari

Ofisi za Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji Dodoma, Kuanza Kujengwa Rasmi.

on

Waziri wa mambo ya ndani, Dr Mwigulu Lamek Nchemba ametembelea eneo la Mtaa wa NCC lililopo katika Manispaa ya Dodoma mkoani humo ambapo ndipo zitajengwa Ofisi za makao makuu ya Idara ya uhamiaji.

Dr Mwigulu amemshukuru Mheshimiwa Rais, kwa kuwapa fedha za ujenzi wa mradi huo ambazo ni Sh bilioni 10 ambapo ujenzi huo utaanza hivi karibuni.

“Eneo limeshapatika kubwa la kutosha la kujenga ofisi ya kisasa kama ambavyo muheshimiwa Rais amesemea wakati anatuhaidi kutupa fedha hizi sasa tumepata eneo la kutosha ambalo lipo karibu na ofisi zote muhimu kama vitambulisho vya Taifa,zimamoto na ofisi zingine za serikali ambapo itasaidia kama mtu akifika uhamiaji anaweza kupata zingine ambazo zipo karibu”. Aliongeza waziri mwigulu.

Waziri mwigulu ametoa rai kwa idara ya uhamiaji kuendelea kuchapa kazi kwa bidii kwani kuchapa kazi kwao ndio kumefanya wao kupata fedha hizo za ujenzi kwa haraka na fedha za kununua nyumba za makazi ya askari Dodoma kwani kama wangefata kupata fedha katika bajeti ya wizara ingechukua mda mrefu kupatikana fedha hizo hivyo kufanya kazi kwao vizuri kunamfanya hata yeye kuwa waziri wa mamboya ndani mzuri.

Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dr Anna Makakala amemshukuru muheshimiwa Rais Dr John magufuli kwa kuwapa fedha hizo kujenga jengo la kisasa na mpaka sasa wameshapa eneo kubwa kabisa ambalo litawawezesha kupata mahitaji yote. “Sisi kama idara tunajukumu la kufata taratibu zote kwa haraka iwezeka nanvyo ili jengo hili ndani ya mwaka wa fedha ujao liweze kukamilika kwasababu kama fedha ni zipo”.alisema Dr Anna.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *